Netanyahu
Senior Member
- Oct 2, 2008
- 147
- 22
Ni muda mrefu sikuweko nchini niliporudi kwa likizo nilishangaa kukuta Benki ya CRDB ambayo niliicha ikiwa ni shirika la umma iliyokuwa hatarini kufa wakati naondoka ikiwa benki imara ya ajabu ambayo ilikuwa na uwezo wa kushindana na mabenki makubwa ya nje kwa huduma za kisasa za kibenki.
Benki ile ingekuwa imekufa na si siri .Nilipouliza ni wazungu gani wameifikisha hapo katika mafanikio yake nikaambiwa hakuna mzungu bali kuna Managing Director Mswahili anaitwa Charles KImei ndiye kaifikisha hapo ilipo.
Huyu kaitoa CRDB iliyokuwa imechoka ikichungulia kaburi hadi hapo ilipo .Sioni sababu ni kwa nini Mtanzania aliyefanya maajabu ya kuifanya iwe ya faida ya kisasa asipewe nishani na Raisi.Ni msomi aliyebaki nchini wa kupigiwa saluti.Wasomi wengi watanzania walipewa mashirika ya UMMA zaidi ya mia nne karibu mia nne yote yamekufa mikononi mwa wasomi hao uchwara yaliyonusurika yamenusurikia mikononi mwa ma-managing directors wageni.CRDB imenusikia mikononi mwa Managing Director Mtanzania ni kwa nini asipewe nishani na Raisi? Kwa maoni yangu napendekeza akumbukwe ni symbol muhimu ya wasomi wa Tanzania kuiga kuwa msomi anayejua kazi yake hata akipewa shirika la umma linalokaribia kufa kama kichwa chake kiko fit na hakusoma kukariri notes na kununua mitihani aweza lifanya lizae faida na likashindana na mashirika ya kimataifa bila woga.