Rais amesaini sheria mpya ya mafao ya nssf bila kujadiliwa bungeni?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais amesaini sheria mpya ya mafao ya nssf bila kujadiliwa bungeni??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bwegebwege, Jul 23, 2012.

 1. bwegebwege

  bwegebwege JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 30, 2010
  Messages: 1,031
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  [FONT=&quot]Jamani nimesikia kuwa Rais Kikwete amesaini muswada wa kufanyia marekebisho ya Sheria ya Mafao (NSSF etc) na kwamba sasa ni rasmi wafanyakazi hawatalipwa mafao yao hadi watakapofikia umri wa kustaafu[/FONT]

  [FONT=&quot]a. [/FONT][FONT=&quot]Kwa hiari (Miaka 55) [/FONT]

  [FONT=&quot]b. [/FONT][FONT=&quot]Kwa lazima (Miaka 60)[/FONT]
  [FONT=&quot]Katika sheri hii wafanyakazi watalipwa mafao yao pale tu wanapopatwa na ajali kazini au kifo….Je jambo hili limethibitishwa?[/FONT] Kama ni kweli.....

  [FONT=&quot]MSAWALI [/FONT]
  [FONT=&quot]1) [/FONT][FONT=&quot]Hivi muswada huu ulijadiliwa na Bunge na kupitishwa? Lini?[/FONT]
  [FONT=&quot]2) [/FONT][FONT=&quot]Kama haukuwahi kujadiliwa na Bunge, Je, Rais anayo mamalaka ya kupitisha sharia bil achombo husika cha kutunga sharia (Bunge) kujadili ?[/FONT]
  [FONT=&quot]3) [/FONT][FONT=&quot]Je, Sheria hii inamsaidiaje Mfanyakazi??[/FONT]
   
 2. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Bwegebwege uko wapi hii issue toka majuzi inajadiliwa hapa. Hii sheria ilipitishwa kwenye bunge la April na JK kama kawaida yake sheria zenye ulaji huwa anasaini chapchap.
   
 3. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  UFAFANUZI KUHUSU FAO LA KUJITOA KATIKA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA MIFUKOYA HIFADHI YA JAMII.

  Ufuatao ni ufafanuzi mfupi kuhusu marekebisho ya Sheria za Mifuko hasa kuhusu fao la kujitoa.


  1. Kama mtakumbuka Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili, 2012. Sheria hiyo tayari imeshasaininiwa na Mheshimiwa Rais na imeanza kutumika rasmi. Marekebisho haya yanawahusu wafanyakazi wote nchini mwetu bila kubagua sekta yoyote ile.


  2. Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa (withdrawal benefits) yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko atapata mafao yake pale atakopfikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55) au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu.


  3. Kwa kuzuia fao la kujitoa mwanachama anapata fursa ya kupata mikopo ya nyumba kwa kutumia dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa kwenye Sheria ya SSRA kipengele cha 38.


  4. Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya uzeeni wakati ambapo nguvu ya kufanya kazi tayari imeshamwishia. Mafao ya kujitoa yanapunguza na hata kuondoa kabisa kinga ya mfanyakazi pale anapoumia kazini au anapofika uzeeni.


  5. Tunawaomba muwaelimishe wafanyakazi umuhimu na madhumuni ya mafao ya hifadhi ya jamii. Hifadhi ya jamii ni nyenzo mahususi iliyowekwa kuwasaidia wafanyakazi kuendesha maisha yao wakati wanapokuwa wameishastaafu tayari. Umasikini wa kipato wakati wa uzee ni mojawapo ya changamoto ngumu kukabiliana nazo kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Tunawasihi tena muelimishe wafanyakazi kuhusu jambo hili. Tafadhali msisite kuwasiliana na Mamlaka pale ufafanuzi zaidi utakapohitajika


  6. Kwa kuwa marekebisho hayo yamesainiwa na kuanza kutumika rasmi kama sheria, mafao ya kujitoa hayawezi kutolewa tena na wafanyakazi watakaoacha kazi kwa sababu ya marekebisho ya kipengele hicho watakuwa hawajaijitendea haki wao wenyewe na pia itakuwa ni kunyume cha Sheria. Mamlaka inaandaa kanuni za mafao ambayo lengo lake ni kuboresha maslahi ya wanachama, kanuni hizo zitajadiliwa na wadau wakiwemo vyama vya wafanyakazi na waajiri ili kupata maoni yao.


  7. Tafadhali muwaelimishe wafanyakazi kwamba pamoja na kuzuia fao la kujitoa, mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya Madini yataendelea kutolewa kama kawaida. Mafao hayo ni Kama vile kuumia kazini pamoja na fao la ulemavu.


  8. Tumesikia kwamba tayari kuna hofu imejijenga kwa wanachama kuhusiana na fao la kujitoa. Ikumbukwe kwamba baadhi ya Mifuko ilikuwa inatoa fao hilo kinyume cha Sheria kwani katika Sheria zao hakuna fao la kujitoa. Tunapenda kusisitiza kwamba wanachama wawe watulivu wakisubiri miongozo.


  9. Tunapenda kuwahakikishia kwamba katika hili maslahi ya wanachama yatalindwa na hakuna mwanachama atakayepunjika kutokana na utaratibu huo.

  Tunatanguliza shukrani za dhati kwa ushirikiano.


  Wenu.


  Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA)

  Irene Isaka
  MKURUGENZI MKUU
   
 4. E

  Eddy GEng Member

  #4
  Jul 23, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hiyo imekula kwetu...huo ni mpango wa kukusanya pesa za uchaguzi 2015,Nyiyiemu ina hali mbaya ,sasa wanaanza kukusanya mapema,wafanyakazi tuamke sasa.
   
 5. m

  markj JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  wakuu! hili jambo tayari liko mahakamani!:spy:
   
 6. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Mhakama ipi?
   
 7. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Ni kwanini wenye fedha tusishirikishwe either tukubali au tukatae?kwani si pesa zetuwenewe tunazozitumikia nakukatwa mimi hiyo hela inaniuma sana maana heri usingeiweka hapo ndipo ninapochukia akili nyepesi wewe unaanguka tu sign bila kujali waathirika?
   
 8. S

  SUWI JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Sijui niache kazi kabisa.................. dah!!!!!!
   
Loading...