Rais ambaye hajawahi kugombea, ilitokea Marekani, itatokea tena huku

Tumia akili

Member
Apr 1, 2013
63
400
Wakuu,

Mwaka 1973 Spiro Agnew alijiuzulu nafasi ya makamu wa Rais wa Marekani kufuatia skendo ya rushwa na matumizi mabaya ya ofisi ikiwemo kukwepa kodi alikofanya wakati ni governor wa Maryland. Rais Richard Nixon akamteua Gerald Ford kuchukua nafasi yake.

August ya mwaka 1974, Rais Richard Nixon alijiuzulu kufuatia skendo ya Watergate. Hapo ikabidi makamu wa Rais, bwana Gerald Ford aapishwe kuwa Rais wa Marekani.

Unaweza kuona jinsi Ford alivyokuwa na bahati. Hakuwahi kugombea umakamu wa Rais au Urais wenyewe lakini alishika vyeo vyote hivyo kwa nyakati tofauti zinazofuatana.

Nimeandika hii habari kuonyesha yanayokuja soon.

Endelea kusubiri!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom