Rais alizindua Mradi wa Maji Hewa Sengerema!? Wizara yatoa ufafanuzi...

English Learner

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
355
355
Siku chache zilizopita, Rais wetu kipenzi alifika Sengerema kwa ziara iliyoambatana na uzinduzi wa mradi maji.

Katika hotuba na tambo za sherehe ya uzinduzi, Rais aliambiwa mradi umekamilika kwa asilimia 100. Kwa uzi huu napenda kumjulisha Mh. Rais Dr. Magufuli kuwa yamkini alizindua maji hewa maana toka ameondoka hatujawahi kuona hata tone la maji.

Kuanzia Busisi kwa Ngeleja, kwenda Bomani, Nyampulukano mpaka Misheni hakuna bomba linalotoa maji. shida ya maji iko palepale na kwa sasa Sengerema ni jua kali hivyo visima na chemichemi zinakauka.

Ndugu yangu Kitila Mkumbo, Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, usijekuangushiwa jumba bovu, fuatilia mradi huu na ujiridhishe juu ya taarifa yangu.

=======
UFAFANUZI TOKA WIZARANI:

Naomba nifafanue ili kuepusha upotoshaji. Huu ni mradi halisi na ndio mradi mkubwa wa maji kuliko yote hapa nchini katika ngazi ya Halmashauri.

Katika ujenzi wa miradi ya maji kuna hatua nne kubwa. Kwanza, ni kutambua chanzo cha maji. Pili ni kujenga miundo ya uzalishaji na kuzalisha maji. Tatu ni kutibu maji na kuyasafirisha kwenda katika matanki. Nne ni kuyatoa maji katika matanki na kuyasambaza kwa wateja/wananchi.

Hatua zote hizi zimefanyika na zinaendelea kufanyika katika mradi huu. Kwanza, tumeongeza uzalisha wa maji. Kabla ya mradi huu uwezo wa kuzalisha maji Mjini Sengerema ilikuwa ni lita chini ya milioni mbili na wananchi asilimia 30 pekee ndiyo waliokuwa na fursa ya kupata maji safi na salama. Kufuatia kukamilika kwa mradi huu sasa tuna uwezo wa kuzalisha maji zaidi ya lita milioni 15 kwa siku wakati mahitaji halisi ni lita milioni sita kwa siku.

Kwa mradi huu tuna uwezo wa kuhudumia wananchi wa Sengerema hadi mwaka 2030 ambapo inakadiriwa kutakuwa na watu wapatao 138,000. Kwa hiyo mradi huu umekamilika kwa asilimia 100.

Kazi ya usambazaji ni endelevu na wateja huunganishwa katika mtandao hatua kwa hatua. Kwa sasa tumesambaza mabomba yenye jumla ya KM 54 Sengerema Mjini na kata zote za Jimbo hili zinapata maji isipokuwa baadhi ya vitongoji ambapo utaratibu wa kuunganishwa unaendelea. Kazi ya haraka kabisa ni kukamilisha kipande cha KM 2 cha eneo la Bukala ambalo gharama yake ni TZS 14 milioni tu. Tumewaagiza Mamlaka ya Maji Jijini Mwanza (MWAUWASA) ambao ndio wamepewa kazi ya usimamizi kwa sasa kukamilisha kazi hii mapema iwezekanavyo.

Sisi kama wizara na Mhe Mbunge wa Sengerema na uongozi wote wa Halmashauri ya Sengerema tunafuatilia kwa karibu utekelezaji wake. Mbali na Sengerema mjini, tunaendelea kukamilisha taratibu za kupeleka maji kutoka katika mradi huu kwenda vijiji sita vya Jimbo la Buchosa ambavyo vipo karibu na Jimbo la Sengerema.

Taarifa kwamba Mhe Rais alizindua mradi hewa sio za kweli na zinastahili kupuuzwa kwa uzito wote.
 
Back
Top Bottom