Rais aliyeshea mkewe na Rais wa Ufaransa

KIBESENI

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
339
268
Jean-Bédel Bokassa; Rais wa Afrika ya kati Mjinga na Kituko cha Karne ya 20

_Aliruhusu Rais wa Ufaransa kulala na mke wake kila alivyotembele nchi yake_

_Alibadili dini na kuwa muislamu ili apate misaada kwa Muamari Gaddafi_

_Aliua wanafunzi wote walioshindwa kununua uniform zilizoshonwa na mke wake_

_Alipiga marufuku ndoa za wake wengi lakini yeye alioa 17_

________________________________________

Safari ya Bokassa ilianza vibaya ikaisha vibaya. Kwanza alikuwa yatima katika umri mdogo, akawa mtu mkubwa jeshini, akawa Rais wa nchi, akala, akanywa, akaiba, akaoa, akazaa, akafukuza, akatesa, akaua, akapinduliwa, akakimbia nchi, akarudi, akafungwa, akaachiwa, akafa ni mzee wa miaka 75, tena lofa!

Akiwa na umri wa miaka 6, alishuhudia baba yake akipigwa mpaka kufa na wakoloni na wiki moja baadaye mama yake alijiua. *1927 ulikuwa ni mwaka wa shetani kwa Bokassa!* Hata hivyo hakufa moyo, alifurukuta mpaka kuibukia jeshi la Ufaransa na kupigana vita ya pili ya Dunia!

Baada ya vita Bokassa aliishi Ufaransa akifanya kazi jeshini! Lakini Januari 1, 1962, alirudi nyumbani baada ya kuitwa na cousin wake Rais David Dacko, wajenge nchi, yeye akabomoa nchi. Alitumia nafasi yake ya Ukuu wa Jeshi kumpindua Rais siku ya 31 Disemba 1965 na kumsweka jela miaka mitatu! Hakumuua kwa sababu ya zimwi likujualo.

Bokassa akaingia Ikulu kula, kunywa, kuua, kuoa na kuzaa. Alioa 17 na watoto zaidi ya 50 achilia mbali wale wa michepukoni! Alikuwa na kila sampuli; Mchina, Mjerumani, Mswidishi, Mtunisia, Mromania Mvietnamu, Mlebanoni na wengine siwajui! Alimaliza mabucha yote kumbe nyama ni ileile! Mpaka mabinti wa kizungu walizaa na Bokassa! *Hapo ndo ujue pesa haidanganyi*.

Unajua wazungu bana, *kama huna hela wanakuita nyani, ukiwa nazo watakuzalia mpaka watoto*. Anakabinti kamoja karembo kweli, kanaitwa Kiki Bokassa! Ni kachoraji kazuri tu. Google utakaona!

Safari za kila siku kwenda kwa wake zake zilisumbua sana mji kwa foleni ndefu! *Wake zake waliishi mbalimbali ili wasidundane.* Siunajua mambo ya uke wenza? Omba yasikukute, timbwili lake hiiii, la mchepuko cha mtoto!

Bokassa alikuwa mwizi na muuaji lakini yeye hakupenda wengine waibe! *Aliamuru wezi wakatwe maskio na mikono!* Wakati mwingine walipigwa nyundo kichwani huku akishuhudia wanavyokufa. *Waliokufa aliwafanywa kitoweo cha wageni wake!* Hata siku amepinduliwa walikuta mabaki ya binadamu kwenye jokofu!

*Aliua wanafunzi wote walioshindwa kununua uniform kwa dola za Marekani 100,sawa na laki mbili za Tanzania, tena zilizoshonwa na mke wake.* Kipindi hicho pato la mtu wa kawaida lilikuwa dola 150 kwa mwaka! Hapo hata mie angeniua tu!

April 1969 alimchinja waziri wake wa Afya; Alexandre Banza, kwa tuhuma za kutaka kumpindua. *Bokassa mwenyewe ndo alimfunga kamba na kumchinja kwa kisu,* baadaye askari waliuchukua mwili wa waziri na kuuzungusha jeshini kama fundisho kwa wengine! *Askari huwa ni watu wa ndio mzee lakini wakikugeukaaaaa*

*Wakati baba yake Bokassa aliutoa uhai wake kwa ajili ya wengine, mtoto alitoa uhai wa wengine kwa ajili yake!* Hapo ndo ujue kumbe *nyoka anaweza kuzaa kenge!*

Mkoloni alimuamrisha Baba Bokassa akusanye manamba kijijini wakahenyeke kiwandani, akagoma; wakamuua, mke wake naye akajiua kwa uchungu wa mume. Mapenzi yalikuwa zamani, *siku hizi mapenzi ni kama siti ya daladala, unashuka wengine wanakaa, unakufa leo kesho gap linazibwa, hajiui mtu. Loh!*

Bokassa alitumwa na Wafaransa kumpindua Rais Dacko kwa sababu aliwazuia kuchota diamond na uranium kwa ajili ya vinu vyao vya nyuklia! Akaanzisha mahusiano na wakomunist wa Uchina. Hivyo ndivyo Rais alivyolikoroga, akenda kulinywea jela!

Bokassa alivyoingia Ikulu tu aliwatimua raia wote wa Uchina na kuvunja mahusiano aliyoyaanzisha Dacko. Wafaransa wakampa big sana!

Bokassa akapitisha sheria ya kila mtu kupiga kazi, *huna kazi ni faini au jela*. *Ombaomba marufuku! Burudani zote usiku tu! Tohara kwa wanawake mwiko. Akazuia kuoa wake wengi lakini yeye alikuwa nao 17!* Na kali kuliko yote, alizuia mahali. Waliokiuka walifanywa chakula ya mamba na simba aliowafuga nyumbani kwake! Mchizi alizingua balaa.

*Ukitaka mabeberu wakutafune jifanye kama unajikuna kuzungumzia mambo ya kuungana.* Bokassa alipoungana na Chad na Congo katika shirikisho la uchumi Ufaransa walimunia!

Mwaka 1969 akabinafsisha Kampuni ya Diamond. Mahusiano na Ufaransa yakaingia doa lakini yakasafishwa mwaka 1970 Bokassa alipohudhuria mazishi ya Generali de Gaulle, Rais wa Ufaransa kuanzia 1958 mpaka 1969. Bokassa alilia sana pale makaburini kwamba *baba yake mzungu* kamuacha. Wafaransa wakajua kumbe huyu ni mtu wetu.

*Kuna jambo la faraja Bokasa alifanya mpaka nikafurahi lakini likaisha vibaya nikachukia.* Aliwahi kuzaa na binti wa Kivyetnamu wakapotezani. Mwaka 1970, maisha yamenyoka akamkumbuka mwanaye. Akaomba Ufaransa imsaidie kumtafuta maana alipewa uraia wa Ufaransa! Ufaransa wakampata, Bokassa akafurahi sana.Akatuma tiketi ya pipa kutoka Vietnam. Binti akapokelewa Bangui na bendi ya jeshi huku redio ya taifa ikirusha live.

Baada ya mwezi mmoja, ilibainika yule binti hakuwa mwanaye. Bokassa akamtia selo binti na kupanga kumrudisha kwao. Mara mwanaye halisi akafika. Bokassa akashangaa na kusema ni mapenzi ya Mungu. Akawakaribisha kwenye familia yake na kuishi nao wote!

Akawa na watoto wawili wenye jina moja; Martine. Yule halisi akaitwa Big Martine na mwingine Litle Martine. Aliwanunulia kila kitu sawa kama mapacha!

Mwaka 1973 wakiwa na miaka 18 waliolewa kwa pamoja. Litle Martine aliolewa na Fidel Obrou, mkuu wa kikosi cha ulinzi wa Rais na Big Martine akaolewa na Dr. Dèdèvodè, daktari wa Binandamu.

*Mwaka wa shetani bwana ukafika*. Fidel Obrou, mume wa Martine Feki na wenzake wakafanya jaribio la kumpindua Bokassa, likashindikana, Bokassa akawaua na pia akaapa kulipiza kisasa kwa ndugu zao.

Wakati Fidel anakufa, mke wake yuko leba akijifungua, tena chini ya uangalizi wa shemeji yake Dr. Dèdèvodè. Alizaliwa mtoto wa kiume. Bokassa akaagiza damu ya Fidel ife. *Kitoto kidogo, kikachomwa sindano ya sumu, kikabadilika rangi na kuwa bluu kikafa, mama akalia, kitoto kidogo kikabeba dhambi ya daddy wake!*

Martine akarudi kwa Bokassa kuendelea na maisha. Hana mume, hana mtoto, anaishi kwa muuaji. Baada ya mwaka mmoja Martine akaamua kutoroka arud kwao Vietnam. *Njiani kuelekea Airport, alipigwa risasi, akafa, akazikwa kando ya barabara.* Njia ya muongo kweli ni fupi; maana alidanganya yeye ni mtoto wa Bokassa, akavuna kifo.

Mwaka 1971 Bokassa akawatibua tena Wafaransa kwa kutaka kuanzisha Benki Kuu na sarafu yao ili kuachana na sarafu ya Ufaransa!Mwaka 1972 akajitangazia Urais wa Maisha. Mwaka 1974 akapiga marufuku magazeti ya Ufaransa kuingia nchini.

Duh! Wafaransa wakaona huyu mbweha kaishakata kamba huyu, tukimuacha itakula kwetu! Mwaka 1975, Rais wa Ufaransa alitinga nchini na kamati yake ya fitina. Sijui walimlisha nini Bokassa maana ghafla aliachana na mipango yake ya kiuchumi na kuibukia kwenye mambo ya ufalme!

Mwaka uliofuata akabadili jina la nchi kuwa *Central Africa Empire!* Disemba 4,1977 alijitawaza kuwa Mfalme. *Alifanya sherehe moja matata sana!* Alitumia bilioni 32 za Kitanzania.

Kamati ya usafiri iliagiza benzi 60 kutoka Ujerumani kwa ajili ya kupokea wageni waalikwa. Mji wote wa Bangui ulipambwa, maskini wote waliondolewa mjini, nyumba zilipigwa rangi na nyingine zilijengwa kwa ajili ya kupokea wageni waalikwa 2500 kutoka nje lakini wakafika 6000. *Wote walikula, kunywa na kulewa kwa gharama ya serikali*. Hata waliofanya dhambi siku ile serikali ililipa!

Mshenzi aliagiza shampeini na wine chupa 60,000 kutoka Ufaransa. Maua fresh yalitoka Ufaransa kwa ndege kukodi.

*Kiti cha Mfalme kilidizainiwa kwa bilioni 2.5* na wapambaji walitoka Ufaransa. *Vazi la mfalme liligharimu bilioni saba*, taji bilioni tatu! Farasi waliovuta gari la Mfalme walitoka Uberigiji na askari waongoza farasi waliopata mafunzo nje!

Mke wake Catherine ndo alikuwa Malkia sijui wake wengine walifichwa wapi. *Wivu sina lakini roho inauma* Siku chache Catherine alitoroka na wanaye saba na kumuacha Mfalme solemba! Alikimbilia nje kufanya biashara za madini!

Wafalme wote aliowaalika Bokassa walimdisi. Hakuna Rais hata mmoja aliyefika!
*Hata rafiki zake Mobutu, Bongo na Idi Amin walimtosa, Bokassa akasema wivu tu ndo uliwasumbua hawakuwa na lolote.* Hata Rais wa Ufaransa Valery Giscard d’Estaing, hakufika.Hata Papa alialikwa hakwenda! Badala yake walimponda kwamba ni kituko cha karne ya 20!

Kadili siku zilivyozidi kwenda, ndivyo Bokassa aliendelea kukosolewa vikali. *Mwaka 1976 akamteua Dacko kuwa mshauri wake pengine amsaidie kuzima moto yeye akaongeza petroli kwenye moto wa mabua ya kiangazi. Mwee!* Akasuka mipango ya kumpindua cousin wake! Wafaransa wakamsaidia Bokassa akapinduliwa Dacko akarudi Ikulu!

Dacko bwana! Alivyokalia kiti akaendeleza ule msimamo wake wa kulinda rasilimali za nchi zisiporwe na Wafaransa! Wafaransa wakamuondoa tena kwa mapinduzi yaliyoendeshwa na André Kolingba. Kolingba akawa Rais, akaweka vizuri mapito ya wafaransa kula na wao kumlinda!

*Mabepari wako tayari kushikana mikono hata na shetani ilimradi kuna ulaji,* ndiyo maana walimlinda Bokassa pamoja na fujo zake. *Hivi unajua hata ile sherehe ya bilioni 32 iligharimiwa na Ufaransa?* Lengo ilikuwa kumsahaulisha ile ajenda yake ya kumbana Mfaransa!

*Bokassa aliua, alikula rushwa, aliiba, alivuruga uchumi lakini bado wakamlinda.* Hata kupinduliwa kwake alijichanganya mwenyewe! Kitendo cha kujiunga na Chad na Congo, wazo la kuanzisha benki na sarafu yake, kubinafsisha kampuni ya diamond na urafiki wake na Wachina vilikuwa ni sawa nakujipiga za uso!

Hivi unajua Bokassa alirudisha mahusiano na Wachina? Hata lile wazo la uniform unadhani alilipata wapi? Si kipindi ameenda kuomba China mwaka 1979? Akiwa huko aliwaona wanafunzi wa kichina walivyopendeza akataka maskini wake wapendeze. Akamrisha na iwe kumbe usione vya elea vimeundwa. Aliishia kuua watoto wetu bure maana hakuna aliyeweza kuafford! Aliuwa zaidi ya mia, tena watoto wenye miaka 8 mpaka 16.

Wafaransa wakapata sababu elfu za kumpiga na kweli wakapiga! Wakamuweka Dacko madarakani alinde maslahi yao!

Walisubiri Bokassa hayupo wakatia timu! Kama kawaida yake alikwenda kuomba kwa mwanaume mwenzake Gaddafi! Halafu alimpenda sana Gaddafi siujui kulikuwa na nini. Aliwahi badili dini na kuwa muislam ili tu apate njuru kwa Gaddafi. Alipewa jina la kiislam, akaitwa *Salah Eddine Ahmed Bokassa.* Gaddaf huko ulipo unajua Mungu anakuona.

Sasa akiwa Libya ndo yakamkuta! Akapinduliwa. Gaddafi akamnyima hifadhi kwa sababu tayari alimpa Idd Amin aliyepinduliwa juzi kati. Akakimbilia Ivory Coast *baada ya Ufaransa kumwambua asitie pua nchini kwao!* Alikaa huko miaka minne na kwenda Ufaransa!

Ufaransa aliishi kwenye jumba lake la kifahari lisilo na umeme wala maji maana alikatiwa kwa kushindwa kulipa bili. Pensheni ya jeshi haikitosha! Pesa alizoficha Ufaransa zilipigwa! Alipata taabu sana huyo Mfalme wa mwendo kasi!

*Hao ndo wazungu, ukiishiwa utamu, wanakutema kama bigjii!*
Yaani *pamoja na kuwakarimia Wafaransa mpaka vya chumbani kwake bado walimkatia umeme na maji.* Hivi unajua kama alishea mapenzi na Rais wa Ufaransa na wakati vitu vya kushare siyo mapenzi? *Mara zote Rais alipokwenda Afrika ya Kati aliwinda tembo, akalala na mke wa Bokassa* na safari za Afrika zilikuwa haziishi. *Kumbe alijua siri ya urembo. Loh! Kweli tembea ule!*

Bokassa aliwapa, pembe za ndovu, urani na shaba wao wakampa silaha akaue ndugu zake! *Bora babu zetu waliopewa shanga wakaenjoy, siyo huyu risasi akaua!* Hapa kati ya babu zetu na Bokassa nani alikuwa na akili? *Mie naona wote tu walikuwa mburula!*

Baada ya kuona mambo yamemdodea *akaamua kumwaga mboga za Rais wa Mfaransa*. Si akafukunyua madhambi yake yote na kuyamwaga gazeti. Mwe! *Alisimulia alivyoshare mke na Rais, alivyomuhonga diamond yenye thamani ya dola za Kimarekani 250,000 wakati ni waziri*. Rais akachafuka mpaka kupoteza Urais wake katika uchaguzi uliofuata!

Akiwa Ufaransa alilindwa asijerudi nyumbani kuharibu. Hata hivyo mwaka 1986, aliwatoroka walinzi na kurudi Afrika kwa lengo la kupindua nchi. Akafikia jela! *Akasomewa hukumu ya kifo, akalia kama mtoto*. Baadaye hukumu ya kifo ikabadilishwa na kuwa kifungo cha maisha!
*Alifungwa kwenye chumba chenye giza tena peke yake kwa miaka sita.* Alikuja kutoka kwa msamaha wa Rais.

*Alitoka jela amechanganyikiwa kabisa akijiita mtume wa Yesu*. Biblia ndo ilikuwa mfariji wake, maana kule kitaa hakuwa na rafiki wala ndugu. Bokassa alikufa kwa ugonjwa wa moyo akiwa na umri wa miaka 75 tena lofa.

Safari yake ya hapa duniani iliyoanza tarehe 22 Februari1921 ikawa imefika ukomo siku ya tarehe 3 Novemba1996!

Asanteni! nchi yake_

Asanteni!in
 
Mmmmh Duniani humu !. kuna mijitu ni hatari sana lakini unashangaa inapata nafasi, Mungu ni wa ajabu tunaambiwa tushukuru kwa kila jambo.
 
Nzuri imenifunza, zaidi wafaransa wanavyowatumia waafrika kwa maslahi yao...

Afrika kusimama kwa miguu yetu itachukua karne nyingi sana.!
 
badae mtu kama wewe unapewa udiwani/ubunge/uwaziri alafu watanzania tunashangaa uliwezaje saini mkataba bila ya kusoma

kama kurasa hizi 3 za kiswahili umeona ndefu utaweza kurasa 100 za lugha ya malkia.

ujinga wa viongozi wetu ulianza kama wewe hivi.
Hatari sana mkuu.
 
Mimi nimesoma yote bila kuruka hata nukta,hongera mtoa mada kwa bandiko hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom