Rais alishawahi kusema ukitajwa kwa rushwa unaondoka hapo hapo hakuna kuunda tume

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Wakati wa hotuba yake Mh Rais aliwahi kusema kua mtumishi wa umma akitajwa kwa ufisadi tayari ana doa atawajibishwa hapo hapo hakuna mambo kuunda tume.Sasa waziri Kitwanga anatajwa sana kuwa na maslahi kwenye hili sakata, sasa kinachosubiriwa ni nini?

Uchunguzi Mara nyingi ni kujiridhisha na uhusika wa mtu katika sakata flani ili kukwepa mishale ya kisheria maana kumshutumu mtu bila ushahidi mwisho wa Siku ataidai haki yake Mahakamani.Kuunda tume ni kuujua ukweli wa jambo na ikithibitika ni kweli basi mtu achukuliwe hatua za kisheri bila kumuonea haya mtu.

Waziri Kitwanga akae pembeni kupisha uchunguzi maana kampuni zake zimetajwa na kuunganishwa na mnufaika mkuu kampuni ya LUGUMI.Ni swali la kijiuliza ni kwanini mtu anakua waziri katika wizara ambayo tayari anafanya biashara nayo? hivi hakuna mgongano wa kimaslahi hapa? Sheria ya maadili ya utumishi wa umma inasemaje?

Kiukweli Kitwanga mpaka sasa kwa maoni yangu hatakiwi kua waziri wa mambo ya ndani,kama sivyo basi ni bora kumhamisha wizara. Kampuni zake kuhusishwa kufanya biashara ndani ya wizara hiyo tayari ni tatizo kwake.
 
Wakati wa hotuba yake Mh Rais aliwahi kusema kua mtimishi wa umma akitajwa kwa ufisadi tayari ana doa atawajibishwa hapo hapo hakuna mambo kuunda tume.Sasa waziri kitwanga anatajwa sana kua na maslahi kwenye hili sakata, sasa kinachosubiriwa ni nini?

Uchunguzi Mara nyingi ni kujiridhisha na uhusika wa mtu katika sakata flani ili kukwepa mishale ya kisheria maana kumshutumu mtu bila ushahidi mwisho wa Siku ataidai haki yake Mahakamani.Kuunda tume ni kuujua ukweli wa jambo na ikithibitika ni kweli basi mtu achukuliwe hatua za kisheri bila kumuonea haya mtu.

Waziri kitwanga akae pembeni kupisha uchunguzi maana kampuni zake zimetajwa na kuunganishwa na mnufaika mkuu kampuni ya LUGUMI.Ni swali la kijiuliza ni kwanini mtu anakua waziri katika wizara ambayo tayari anafanya biashara nayo? hivi hakuna mgongano wa kimaslahi hapa? Sheria ya maadili ya utumishi wa umma inasemaje? Kiukweli Kitwanga mpaka sasa kwa maoni yangu hatakiwi kua waziri wa mambo ya ndani,kama sivyo basi ni bora kumhamisha wizara.Kampuni zake kuhusishwa kufanya biashara ndani ya wizara hiyo tayari ni tatizo kwake.
Sasa Lugumi mesheni town tu aondeke aende wapi?
 
CCM inajua inachofanya.

Huyo waziri si ajabu kupewa wizara hiyo ni mkakati wa mtandao wao.
 
Rais wetu magu macho na masikio yetu ni juu ya said lugum, charlz kitwanga na wengne wote waliyotajwa na kuhusika na ujambazi, ukiwatumbua wote na tena mh rais uwechelewa sana kigugumizi chanin?
 
Mheshimiwa waziri hana directly relationship na hiyo tender

1. Mkataba ni kati ya Lugumi na jeshi la polisi
2. Infosys na Mheshiwa ni two different person (refer to separate legal entity concept). Mheshiwa ni mmoja kati ya shareholders wa Infosys ambayo ina share holders zaidi ya wa nne
3. Iliyo-sign mkataba ni Infosys na sio waziri na Infosys imepewa kazi na Lugumi na sio Wizara
4. Tender ilitolewa kipindi cha awamu ya nne ambapo Wizara haikuwa chini
 
Suala je alinufaika na fedha za serikali alizolipwa na Lugumi?
Je kampuni yake ilifanya kazi iliyolipwa?
Tuanzie hapo
 
magufuli hakiishi kile anacho kihubiri,,,ni ccm ni ile ile na usanii ni jadi yao tutegemee miaka mingine mitano ya maigizo.
 
Mheshimiwa waziri hana directly relationship na hiyo tender

1. Mkataba ni kati ya Lugumi na jeshi la polisi
2. Infosys na Mheshiwa ni two different person (refer to separate legal entity concept). Mheshiwa ni mmoja kati ya shareholders wa Infosys ambayo ina share holders zaidi ya wa nne
3. Iliyo-sign mkataba ni Infosys na sio waziri na Infosys imepewa kazi na Lugumi na sio Wizara
4. Tender ilitolewa kipindi cha awamu ya nne ambapo Wizara haikuwa chini
CCM ni ileile we unaona umeandika facts kumbe wizi mtupu eti infosys na kitwanga Ni two different person! Hivi unaelewa ulichoandika? Afu unasema kitwanga Ni mmoja wa shareholders zaidi ya wanne! So unataka shareholders wengine watajwe ili iweje!

3&4 hueleweki. Anza upya.
 
Wakati wa hotuba yake Mh Rais aliwahi kusema kua mtimishi wa umma akitajwa kwa ufisadi tayari ana doa atawajibishwa hapo hapo hakuna mambo kuunda tume.Sasa waziri kitwanga anatajwa sana kua na maslahi kwenye hili sakata, sasa kinachosubiriwa ni nini?

Uchunguzi Mara nyingi ni kujiridhisha na uhusika wa mtu katika sakata flani ili kukwepa mishale ya kisheria maana kumshutumu mtu bila ushahidi mwisho wa Siku ataidai haki yake Mahakamani.Kuunda tume ni kuujua ukweli wa jambo na ikithibitika ni kweli basi mtu achukuliwe hatua za kisheri bila kumuonea haya mtu.

Waziri kitwanga akae pembeni kupisha uchunguzi maana kampuni zake zimetajwa na kuunganishwa na mnufaika mkuu kampuni ya LUGUMI.Ni swali la kijiuliza ni kwanini mtu anakua waziri katika wizara ambayo tayari anafanya biashara nayo? hivi hakuna mgongano wa kimaslahi hapa? Sheria ya maadili ya utumishi wa umma inasemaje? Kiukweli Kitwanga mpaka sasa kwa maoni yangu hatakiwi kua waziri wa mambo ya ndani,kama sivyo basi ni bora kumhamisha wizara.Kampuni zake kuhusishwa kufanya biashara ndani ya wizara hiyo tayari ni tatizo kwake.
Tatizo kuwa Hilo Dili limejaa list ndefu ya wajanja wengi ambao hawataki waumbuke wanafanya juu chini JIPU lisitumbuliwe , wanajua wakimwaga Ugali lazima Kitwanga atamwaga atamwaga mboga, maji ya kunywa mpaka ya kunawa na tishu atazitupa zikiwa mpya, Said mwema ambaye ni IGP mstaafu amedhibiti kote kwenye vyombo vya Uchunguzi na anahakikisha kuwa Lugumi hatatoa Siri zozote juu ya list Yao yote .( kufa kufaana ) wabunge wengi wanakula pesa za kitwanga ili wamtetee pindi sakata likitinga bungeni .
 
Mheshimiwa waziri hana directly relationship na hiyo tender

1. Mkataba ni kati ya Lugumi na jeshi la polisi
2. Infosys na Mheshiwa ni two different person (refer to separate legal entity concept). Mheshiwa ni mmoja kati ya shareholders wa Infosys ambayo ina share holders zaidi ya wa nne
3. Iliyo-sign mkataba ni Infosys na sio waziri na Infosys imepewa kazi na Lugumi na sio Wizara
4. Tender ilitolewa kipindi cha awamu ya nne ambapo Wizara haikuwa chini
Acha kuona watu wote ni wajinga
 
CCM ni ileile we unaona umeandika facts kumbe wizi mtupu eti infosys na kitwanga Ni two different person! Hivi unaelewa ulichoandika? Afu unasema kitwanga Ni mmoja wa shareholders zaidi ya wanne! So unataka shareholders wengine watajwe ili iweje!

3&4 hueleweki. Anza upya.
Kitwanga anatumia Rushwa kukwepesha JIPU lisitumbuliwe na Sasa kamati ya Bunge wameshiba pesa wapo busy kuandaa reports ya Ajabu ya kumsafisha hiyo report itawashangaza watanzania na huenda ikasababisha watu kuwachukia wabunge milele.
 
Back
Top Bottom