Rais alisaini sheria ya kuunganisha mifuko, Wataalam yaani SSRA wakatengeneza Kanuni za kuendesha mifuko

Queen Esther

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
2,195
1,417
Ndg zangu Great Thinkers wa JF

Nimeona wadau wengi wanashindwa kutofautisha Sheria na Regulations au kanuni zinazosimamia sheria husika. Pia wameshindwa kuelewa kuwa Rais anasaini mabadiliko ya sheria husika baada ya kupitishwa na Bunge.

Baada ya hapo Wataalamu wanakaa kutengeneza kanuni ambapo kwa Hifadhi ya Jamii ni kazi ya Regulator yaani SSRA.

Kama huelewi jambo ni vizuri ukauliza maana Sheria ya kuunganisha Mifuko ipo palepale kama Rais alivyoeleza. Kilichobadilika ni kanuni za kikokoteo. Wakati wowote kanuni zinaweza kuendelea kubadilika hata kabla ya 2023 iwapo Wataalamu watamaliza kazi yao mapema bila kusahau uimara wa mifuko kifedha.

WALE AMBAO MNAPOTOSHA ACHENI KUTAFUTA KICK! SHERIA INATANGULIWA NA KUSAINIWA NA RAIS NDIPO KANUNI ZINAFUATA. SIO KAZI YA RAIS WA NCHI KUANDAA KANUNI AU REGULATIONS HIYO NI KAZI YA WATAALAMU.

UFAFANUZI KUHUSU FAO LA KUJITOA KATIKA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA MIFUKOYA HIFADHI YA JAMII.

Ufuatao ni ufafanuzi mfupi kuhusu marekebisho ya Sheria za Mifuko hasa kuhusu fao la kujitoa.

1. Kama mtakumbuka Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili, 2012. Sheria hiyo tayari imeshasaininiwa na Mheshimiwa Rais na imeanza kutumika rasmi. Marekebisho haya yanawahusu wafanyakazi wote nchini mwetu bila kubagua sekta yoyote ile.

2. Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa (withdrawal benefits) yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko atapata mafao yake pale atakopfikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55) au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu.

3. Kwa kuzuia fao la kujitoa mwanachama anapata fursa ya kupata mikopo ya nyumba kwa kutumia dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa kwenye Sheria ya SSRA kipengele cha 38.

4. Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya uzeeni wakati ambapo nguvu ya kufanya kazi tayari imeshamwishia. Mafao ya kujitoa yanapunguza na hata kuondoa kabisa kinga ya mfanyakazi pale anapoumia kazini au anapofika uzeeni.

5. Tunawaomba muwaelimishe wafanyakazi umuhimu na madhumuni ya mafao ya hifadhi ya jamii. Hifadhi ya jamii ni nyenzo mahususi iliyowekwa kuwasaidia wafanyakazi kuendesha maisha yao wakati wanapokuwa wameishastaafu tayari. Umasikini wa kipato wakati wa uzee ni mojawapo ya changamoto ngumu kukabiliana nazo kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Tunawasihi tena muelimishe wafanyakazi kuhusu jambo hili. Tafadhali msisite kuwasiliana na Mamlaka pale ufafanuzi zaidi utakapohitajika

6. Kwa kuwa marekebisho hayo yamesainiwa na kuanza kutumika rasmi kama sheria, mafao ya kujitoa hayawezi kutolewa tena na wafanyakazi watakaoacha kazi kwa sababu ya marekebisho ya kipengele hicho watakuwa hawajaijitendea haki wao wenyewe na pia itakuwa ni kunyume cha Sheria. Mamlaka inaandaa kanuni za mafao ambayo lengo lake ni kuboresha maslahi ya wanachama, kanuni hizo zitajadiliwa na wadau wakiwemo vyama vya wafanyakazi na waajiri ili kupata maoni yao.

7. Tafadhali muwaelimishe wafanyakazi kwamba pamoja na kuzuia fao la kujitoa, mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya Madini yataendelea kutolewa kama kawaida. Mafao hayo ni Kama vile kuumia kazini pamoja na fao la ulemavu.

8. Tumesikia kwamba tayari kuna hofu imejijenga kwa wanachama kuhusiana na fao la kujitoa. Ikumbukwe kwamba baadhi ya Mifuko ilikuwa inatoa fao hilo kinyume cha Sheria kwani katika Sheria zao hakuna fao la kujitoa. Tunapenda kusisitiza kwamba wanachama wawe watulivu wakisubiri miongozo.

9. Tunapenda kuwahakikishia kwamba katika hili maslahi ya wanachama yatalindwa na hakuna mwanachama atakayepunjika kutokana na utaratibu huo.

Tunatanguliza shukrani za dhati kwa ushirikiano.

Wenu.

Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA)

Irene Isaka
MKURUGENZI MKUU
 
Hahaha inasaidia nini kwa sasa. Watu hawataki kujua kanuni za kuendesha mfuko au mifuko. Wananchi hasa wafanyakazi walitaka kufahamu WANAPA 50% au Hawapati.
Kwasababu wameshafahamu wanapata 50%, Hizo kanuni fanyeni mnavyotaka ila KIKOKOTOO MSIKIGUSE.
 
Queen Esther,

na Rais wako walikua kasafiri kwenda sayari nyingine wakati mchakato wa kanuni hadi kupitishwa mwezi wa nane ulipokua unaendelea siyo? hakujisumbua kabisa kujua kinachoendelea?

alipoingia madarkani tu alifuta fao la kujitoa lililokua linategemewa sana na wafanyakazi wa ajira za mikataba. watu waliojaribu kuandamana na kupiga kelele walinyamazishwa. Ila leo yeye huyohuyo anahoji tena kwamba kwa nini mtu afanye kazi mwa miaka mwili au mitatu (katoa mfano wa kibarua wa stigila joji na darasaja na salenda) mradi unapokwisha angoje hadi uzee ndio aje alipwe mafao yake? hivyo na hiki ni ugunduzi mpya kaugungua leo baada ya kuwasikiliza wawakilishi wa vyama vya wafanyakazi pale ikulu?

nadhni inahitaji mtu awe kwenye hisia zingine kwanza ili apate uwezo kama huu wako wa kutetea matendo ya JPM
 
Saa hii ndio mnajiffanya mnatoa ufafanuzi baada ya kuanza kushikana uchawi? Kabla ya hapo mlikuwa mnajibu kwa nyodo. Ni hivi toka mwanzo hiyo sheria lengo ilikuwa ni hicho kilichoamuliwa na hizo kanuni. Siku hizi kumekuwa na tabia ya kutunga sheria yenye nia ovu, inapambwa pambwa kisha inawekwa mwanya wa kutengeneza kanuni kwa waziri, eti waziri atatengeneza kanuni kwa jinsi atakavyoona inafaa. Ni hivi, ubovu wa sheria ndio umetoa mwanya wa kanuni kutekeleza nia ovu. Hayo mengine sijui nani alisaini kabla ya nani na nani akatunga kanuni mtajua nyie.
 
Saa hii ndio mnajiffanya mnatoa ufafanuzi baada ya kuanza kushikana uchawi? Kabla ya hapo mlikuwa mnajibu kwa nyodo. Ni hivi toka mwanzo hiyo sheria lengo ilikuwa ni hicho kilichoamuliwa na hizo kanuni. Siku hizi kumekuwa na tabia ya kutunga sheria yenye nia ovu, inapambwa pambwa kisha inawekwa mwanya wa kutengeneza kanuni kwa waziri, eti waziri atatengeneza kanuni kwa jinsi atakavyoona inafaa. Ni hivi, ubovu wa sheria ndio umetoa mwanya wa kanuni kutekeleza nia ovu. Hayo mengine sijui nani alisaini kabla ya nani na nani akatunga kanuni mtajua nyie.
Mkuu umesema kweli kabisa..
Ona hivi sasa Sheria ya Vyama cha Siasa inavyopigiwa kelele..
Wameweka pamba masikioni na wanaenda kuipitisha na ubovu wake pale Bungeni..
Huko mbele ya safari atajifanya anaitafutia muafaka.
 
Hivi mleta mada kwa akili zako unadhani raisi alikuwa hajui kuhusu hizi kanuni au wameona sasa kuwa wamegusa pasipogusika kwa hiyo wamebacktrack?

Kwa taarifa yako, Raisi yuko well informed kuhusu mambo ya nchi kuliko mtu yoyote maana ana tools za kumpa taarifa ya kinachojiri kila siku!

Waziri wake, Jenister kila wakati alikuwa akikitetea kikokitowo, unadhani huo ulikuwa msimamo wake binafsi au wa serikali nzima?

Kama kuna nia njema ya hicho kikokotowo kwa nini power apewe waziri za kukiweka kwenye kanuni badala ya kukaa kwenye sheria mama?, Huoni hapo Wanasiasa wanaweza kuwa wanakibadirishabadirisha tu kusuit ajenda zao kila wakati
 
Wabunge wa ndiyooo pamoja na sipika Ndungai waliopitisha muswada walipoulizwa walisema kuwa wakati wanapitisha kikokotoo cha asilimia 25 hakikuwepo wakati wanapitisha na wakasema kuwa kitakuwa kimechomekwa na serekari baada ya bunge kupitisha,sasa katika uchomekwaji huu sijui jiwe anaponaje wakati yeye ndiye mwenye serekali.
 
3. Kwa kuzuia fao la kujitoa mwanachama anapata fursa ya kupata mikopo ya nyumba kwa kutumia dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa kwenye Sheria ya SSRA kipengele cha 38.

yaani mimi na tumilioni tano kangu NSSF nitapata mkopo wa nyumba?
 
Mleta mada ana mpeo mdogo sana.
Muswaada wa hiyo sheria na kanuni za kikokotoo zote zimetengenezwa na serikali ya CCM ya awamu ya Tano chini ya usimamizi wa John Pombe Magufuli kwa 100%. Hivyo rais anahusika na kila kitu. Vitu vyote hivyo vimepitia baraza la mawaziri na kamati kuu ya CCM ambalo Magufuli ndio mwenyekiti wake.

Huwezi kusema nyama ya kitimoto ni haramu lakini mchuzi wake ni halali.
 
Mleta mada ana mpeo mdogo sana.
Muswaada wa hiyo sheria na kanuni za kikokotoo zote zimetengenezwa na serikali ya CCM ya awamu ya Tano chini ya usimamizi wa John Pombe Magufuli kwa 100%. Hivyo rais anahusika na kila kitu. Vitu vyote hivyo vimepitia baraza la mawaziri na kamati kuu ya CCM ambalo Magufuli ndio mwenyekiti wake.

Huwezi kusema nyama ya kitimoto ni haramu lakini mchuzi wake ni halali.
Mkuu nimeipenda hiyo. Huwezi sema mnofu ni haramu huku unabugia mchuzi eti ni halali. Hawa watu ni vilaza mbaya zaidi wanatulazimisha tuwe kama wao. Aibu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
naona imeandikwa na Irene Isaka, vipi alikua bado hajapata memo kukoka kwa msigwa? tena naona aliendelea kujifanya anajua saaana yaliyo mema kwa wafanyakazi kuliko hata wafanyakazi wenyewe! ni vema ameondolewa hapo huyo binti alikua jeuri, watu wanalalamika yeye anakuja na elimu uchwara kuwalazimisha watu wapende maelezo yake.
nae magufuri awe anawatumia hata sms mapema hawa watu kabla ya kuwatumbua basi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom