Rais akiliweka suala la wawekezaji kama 'fungulia mbwa', sijui nini kitatokea

Baada ya kampuni ya Airtel kuwarudishia hisa zenu bei ya bando imeshuka??
Mama anajaribu kutuliza huku na kule, anatukiza kelele za mitandaoni, na kujaribu kulinda sera ya CCM. Ila akuwe anachokoma mitandaoni, akigawe mara laki moja ndio atakuwa ukubwa wa tatizo lenyewe, maana mitandao inakuza jambo ambalo halina uhalisia.

Ni ujinga kumlaumu JPM kwenye swala la kodi na uwekezaji, wakati aliikuta nchi ikiwaimeoza. Kumbuka kampuni ya simu Airtel walivyotuzulumu hisa zetu, Zanzibar walikuwa hawalipi umeme, Mashamba ya mkonge waliuawa baada ya kujimilikisha kinyemela ili tu walete katani ya bei chini kutoka nje. Mzee Abood Morogoro na sarakasi zake, mashirika ya umma kuwekaza fedha benki binafsi na benki hizo zinaikopesha serikali fedha zake zenyewe. mifano ni mingi sana, bila kusahau misamaha ya kodi iliyozidi ukubwa uchumi wetu.

Mama lazima awe makini, tunataka wawekezaji lakini sio kwa gharama ya kipato chetu na maendeleo yetu.
 
Baada ya kampuni ya Airtel kuwarudishia hisa zenu bei ya bando imeshuka??
Gharama za uendeshaji kampuni ya mawasiliano sio mdogo. Kila baada ya miezi 18 teknolojia ya mawasiliano inabadilika, na wao inabidi wajipange kwenda na wakati. Lasivyo usingepata fursa ya kujibu nilichoandika hapa kwa kukosa mtandao wenye uhakika.
 
Tangu lini Chadema wakaitakia mema ccm hadi wajipe kazi ya kumsifia rais Samia?.

Kazi ya kumsifia rais Samia ni ya MATAGA siyo ya chadema
 
Hao wawekezaji mnaombiwa Walikimbia nchi Walikimbilia Mozambique,zambia or Uganda , all corrupted countries, waambieni wakimbilie Kenya kama hawaja nyooshwa na kodi, mwekezaji aje lakini ambae analipa kodi ili nchi iweze kujiendesha, hivi jamani mwekezaji au mfanya biashara hataki EFD huyu ni mfanya biashara kweli? tusijidanganye kurudi kule tulikotoka ni kubaya, TRA watoe tu elimu ya kutosha kwa wafanya biashara tuendelee kulipa kodi.
 
Huu muda uliopoteza kuandika ngonjera ungekunywa hata mbege. Uko nyuma sana ya muda, Amka.
Bado naomboleza kifo cha Jemedari Dkt. John Pombe Magufuli, Mzalendo wa KWELI asiye na UNAFIKI katika maslahi na ustawi wa watu wake na upendo kwa nchi yake, yaani Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mtu aliyejipambanua kwa nia ya dhati akihimiza kwa vitendo juu ya miradi ya kimkakati. HAKUNA AMBAYE ANAWEZA KUFUTA REKODI YAKE DAIMA!

1. MVUTO KWA WAWEKEZAJI

JPM alipokuwa akiingia madarakani Tz tulikuwa tunanuka ufisadi, kila kona ufisadi, UFISADI! Alipoingia na kulala nayo mbele, tena leo tunaanza kuonyesha dalili ya kubembeleza wawekezaji mafisadi fisadi kwa mbali...... Mwekezaji ambaye anakuja kutunyonya huyo hatuna haja ya kusumbua TRA yetu pendwa kumrejesha, apotelee mbali tena ikiwezekana hata kuzimu aingie. Watanzania tumelia sana kwa machozi hata kujitoa uhai kwa kuondokewa na JPM! HAKUKUWA NA NAMNA NYINGINE ISIPOKUWA SAFISHASAFISHA NDIPO TUANZE KWENDA SAWA! JPM ndiye aliyeanzisha Wizara ya Uwekezaji, alijua baada ya kuweka misingi mizuri na kusafisha, sasa ni wakati wa kuvutia wawekezaji wa kweli! SASA tukitaka tuipe TRA kazi ya kurejesha hata wawekezaji wa hovyo tutapotea.

Kosa ambalo ninaliona HUENDA limefanyika sasa na kipindi kilichopita ni kumteua Professor Mkumbo kusimamia masuala ya biashara na uwekezaji kama Waziri. Binafsi namwona kama aina ya wasomi ambao wanafanya vizuri wanapotumwa siyo wanapoambiwa wabuni mawazo mapya. Ndiyo sababu tangu ateuliwe na Hayati Magufuli hajafanya lolote kwenye Wizara ya Uwekezaji, hajatoa mwongozo wa kiuongozi kuifanya Wizara kuanza kufanya kile kinachotarajiwa! Nachelea kusema siyo combination sahihi ya kiuongozi kati ya Mwambe na Kitilya kwenye eneo la Biashara na Uwekezaji! Lakini, muda utasema wenyewe!

2. SUALA LA KUFUNGA AKAUNTI ZA WAFANYABIASHARA

Pamoja na kuwepo task force lakini TRA hawakurupuki katika kufunga akaunti za biashara za watu kwa uzoefu mdogo nilio nao. MAUMIVU YA MAZOEA YA UFISADI YA HUKO NYUMA NDIYO YANAYOTUFANYA LEO TUSIKIE KILIO CHA KUFUNGA AKAUNTI ZA WATU! Siku za huko nyuma kulikuwa na mchezo ambao pengine Mhe. Samia hajapata kudokezwa. Kwa mfano, mfanyabiashara amekata wafanyakazi mishahara kwa PAYE kwa miaka mingi, amelipwa pesa na wateja wake ikiwemo VAT na amejaza Ritani zake kwamba anatakiwa apeleke VAT ambayo tayari amelipwa. Vitabu vyake vinaonyesha hana pesa anazodai nyingi kutoka kwa wadeni wake na anazo pesa benki na ukiangalia anajilipa na kufanya mambo mengi tu kwa fedha ya umma ambayo amekata bila kupeleka TRA. SASA KWA NINI MTU WA NAMNA HII ASIFUNGIWE AKAUNTI YAKE NA PESA ZICHUKULIWE??????? YAANI MTU AMEKATA WAFANYAKAZI PESA AU AMELIPWA VAT kwenye MAUZO na anadaiwa ambayo siyo pesa yake, HATAKI KUPELEKA TRA HALAFU TUANZE KUMBEMBELEZA KISA NI MWEKEZAJI????? KWA NINI ASIITWE MHUJUMU UCHUMI HUYO?

-Mahali fulani hapa Tz kuna kampuni ambayo ilikuwa na madeni makubwa ya VAT na makato ya PAYE kwa wafanyakazi lakini wakurugenzi wake wanajilipa fedha nyingi (mamia ya mamilioni) kwa mkupuo kama bonasi na mengineyo. Wakati huo wana pesa ya serikali ya miaka kadhaa mamia ya mamilioni hawajapeleka TRA! - VAt na PAYE! TRA wakafunga akaunti zao mpaka waonyeshe kuanza kulipa deni na kuingia nao mkataba. Sasa hapo tuwalaumu TRA kwa lipi? Tuseme TRA ni wababe?

3. UNAFIKI UNAOWEZA KUTUGHARIMU VIBAYA!

Rais Samia atafanya vizuri akiendeleza pale alipoishia Magufuli, akitaka kwenda haraka haraka kuchimba madini maeneo ya hifadhi ambako tembo hawali madini, nachelea atakamatwa na wawekezaji matapeli na mafisadi haraka sana! Mama tunayo hamu kubwa kuona akituongoza vyema, asisahau kwamba Watanzania, na hasa wanaomzunguka MFALME ni wazuri sana kupongeza, kiasi ambacho wapo tayari kulamba miguu! Leo Rais ameeleza hadharani kwamba pamoja na ulinzi uliopo wa vymbo vyetu pale MERERANI bado Tanzanite yetu inatoroshwa chini ya ulinzi mkali. Nyingine ametuambia inapitishwa chini kwa chini, hatujui mahandaki yametobokea nchi gani ambako vyombo vyetu havioni. NI HABARI YA KUSHITUA SANA HII! Tanzania tumejivunia jeshi letu la wananchi kwa miaka mingi katika nyanja ya UADILIFU na UZALENDO tangu tupate UHURU na kuwa Jamhuri ya Muungano! Tamko kama hili la leo linaibua maswali mengi! Je! walinzi hawatoshi? Je! Teknolojia ya ulinzi katika eneo lile ni duni? Je! aliyetajwa analinda pale amepoteza uadilifu na uzalendo? Ni nini hasa kimetokea? Maswai mengi kweli kweli! Mhe. Rais ana vyombo vingi vinavyofanya kazi kwa weredi hali vikimshauri vyema, LAKINI USHAURI tu ni kwamba aangalie wasaidizi wake wasijipendekeze kupitiliza kiasi cha kujikuta wanaibua taarifa za uchonganishi na mvutano baina ya vyombo vyetu vyenyewe vinavyomsaidia! Na mengine, yashughulikiwe ndani na wayamalize na kuelekezana huko ndani si lazima wananchi tuyasikie.

4. MISAMAHA YA MADENI YATOKANAYO NA TAX COMPLIANCE PROCEDURES

Kumekuwa na mwitikio mkubwa kwa Watanzania kufungua biashara na hasa makampuni ndani ya nchi yao. Lakini upana wa elimu inayotolewa kwa mfanya biashara anapoanzisha biashara yake na hasa makampuni ni mdogo sana sana. Sasa makampuni yana matakwa mengi sana ya kisheria ambayo lazima kufuata (tax compliance matters). Sasa, kinachotokea, ambach ndiyo ukweli ambao pengine Rais hajaufahamu ni kwamba, kutokana na uelewa mdogo wa elimu ya kulipa kodi kwa mlipa kodi, unakuta mlipa kodi pengine amewasilisha malipo ya kodi fulani TRA lakini kwa uelewa mdogo anajikuta hajapeleka ritani ya kodi husika kwa wakati. Faini (fine) na penati (Penalties) zinakuwa ni kubwa mno ambazo ndiyo kilio kikubwa kwa watu wengi.

Mwaka 2018 ulipita msamaha kwa faini na penati na riba kwa kuchelewesha ritani za kodi na malipo husika. Lakini hakuna mfumo ambao unamsaidia mwekezaji hasa kujua kwamba kwa aina ya biashara anayofanya ni ritani za namna gani na malipo yapi anapaswa kuwa anafanya na kwa muda gani. Wawekezaji ambao ni wadogo au wa kati pia wanaweza kuwa wasiwe na uwezo wa kuajiri Mshauri/ Consultant kutokana na gharama. Kwa hiyo wanapokuja kutafuta mshauri pengine kipindi cha kufunga hesabu za mwaka mzima anajikuta amekosea vitu vingi sana ambavyo tayari vimemwingiza kwenye fines na penalties kubwa kuliko hata pengine mauzo yake yote ya mwaka. Na mfanyabiashara anajikuta amepigwa riba na penalti hata katika kipindi ambacho amewajulisha TRA kwamba anachangamoto fulani za kibiashara. Kwa hiyo, hata anapotaka kurejea kwenye biashara tena atakutana na mzigo wa penati na riba ambazo ni za masuala ya compliances hata katika kipindi ambacho alikuwa pengine amesimama biashara.

KWA BAHATI MBAYA, Kanuni za msamaha wa penati na riba za 2020 (THE TAX ADMINISTRATION (REMISSION OF INTERESTS AND PENALTIES) REGULATIONS, 2020) hazitoi nafasi kwa mfanyabiashara kuomba kufutiwa madeni ya penati na riba hata kama hakuna kodi ya msingi (principal tax) anayodaiwa. Kuna haja ya kuipitia upya Tax administration act, ili tax compliance provisions zisiwe kama KUKOMOANA NA KUZINGUANA! Pia tumwombe Mheshimiwa Rais kutoa tena msamaha wa malimbikizo ya panalties na interests kwa wafanyabiashara. Hili itaamsha BIASHARA nyingi sana nchini. TRA kuwe na dawati la kuelimisha wafanyabishara ili wapate kuelewa matakwa mbalimbali ambayo yanaweza kuwakabili wanapoendesha biashara zao ili wasijikute wanalia baadaye badala ya kunawili na TRA kuchekelea kukamua maziwa mengi!

Mtanikumbuka kwa mazuri, siyo mabaya! Pumzika baba yetu, pumzika Mzalendo na Mfia nchi yako JPM.
Inasikitisha sana.Mbaya zaidi hayo mambo si muhimu kuyaweka hadharani kuna mambo mengine yalipaswa kuzungumzwa ofisini maana ukiweka hadharani yanabomoa zaidi kuliko kujenga na ndiyo maana JPM siyo kwamba hakutambua bali alitambua kuwa kuweka kila kitu hadharani itampotezea focus yeye pamoja na serikali yake.Lakini huyu mama hajatambua hilo bado.

Pumzika kwa amani JPM
 
Watanzania kwa bahati mbaya sana tumekosa uadilifu wa nafsi, ndiyo maana kuna wakati tunasifu tulipostahili kulaumu, na tunalaumu wakati tulipotakiwa kusifu.

Kwa vigezo vyote vya kiuchumi na kiuongozi, awamu ya 4 ilifanya vizuri zaidi kuliko awamu ya 5. Awamu ya 5 ilizizidi awamu zote kwa kujitangaza, na kuyatangaza mafanikio madogo sana ili yaonekane ni makubwa sana.

Tukienda kwa takwimu, ni awamu ipi kati ya hizi 2 nilizozitaja iliongeza kwa kiasi kikubwa pato la Taifa na wastani wa pato la mwananchi?

Katika awamu hizi 2, ni awamu ipi sekta za uchumi (kiimo, madini, viwanda, utaii, n.k) zilikuwa na ukuuaji mkubwa zaidi?

Katika hizi awamu 2, ni awamu ipi ukuaji wa uwekezaji ulikuwa mkubwa zaidi?

Kwa vyovyote ni awamu ya 4. Yawezekana mtu anaweza asimpende Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, lakini tuwe wakweli wa nafai zetu katika yale ambayo aliyafanya vizuri.

Katika ulimwengu wa leo, ni uchumi wa kisasa tu ndio unaoweza kuhimili ushindani wa Dunia. Na kwa mwelekeo wa Rais wa sasa, anataka kujenga uchumi wa kisasa, kutoka rudimental economy iloyoegemea zaidi kwenye primitive means of collecting government revenue. Maendeleo, ni lazima yawe maendeleo ya watu. Huwezi kusema eti nchi yangu inaendelea wakati unawanyang'anya fedha watu, unawaweka watu mahabusu miaka kwa tuhuma za ufisadi, unashindwa kithibitosha ni kwa nna gani wanahujumu uchumi. Baadaye wanalazimishwa wakiri tuhuma, wanyang'anywe pesa, kisha wawe huru.

Hata kama tukajenga flyovers toka Duniani mpaka mwezini lakini kama watu wetu hawatendewi haki, hawaoni wapo huru na amani kwenye nchi yao, flyovers hizo hazitakuwa na maana yoyote. Maendeleo ypyote yanaym
Unapozungumzia hizo awamu ukumbuke kwamba awamu ya Nne ilikuwa na miaka Kumi na awamu ya Tano ilikuwa na miaka Sita tu!
 
Eeh Mungu Mwenyezi, tunaomba utuhurumie tena Tanzania😭😭😭! Lisiwe tena pango la wanyamg'anyi🙏🙏🙏! Tunaomba eeh Mwenyezi Mungu!
Wanyang’anyi walikuwa Magufuli na vijana wake kina Sabaya. Na Mungu ameshstusaidia kwa kumfutilia mbali huyo Magufuli kwenye uso wa dunia
 
Mama anajaribu kutuliza huku na kule, anatukiza kelele za mitandaoni, na kujaribu kulinda sera ya CCM. Ila akuwe anachokoma mitandaoni, akigawe mara laki moja ndio atakuwa ukubwa wa tatizo lenyewe, maana mitandao inakuza jambo ambalo halina uhalisia.

Ni ujinga kumlaumu JPM kwenye swala la kodi na uwekezaji, wakati aliikuta nchi ikiwaimeoza. Kumbuka kampuni ya simu Airtel walivyotuzulumu hisa zetu, Zanzibar walikuwa hawalipi umeme, Mashamba ya mkonge waliuawa baada ya kujimilikisha kinyemela ili tu walete katani ya bei chini kutoka nje. Mzee Abood Morogoro na sarakasi zake, mashirika ya umma kuwekaza fedha benki binafsi na benki hizo zinaikopesha serikali fedha zake zenyewe. mifano ni mingi sana, bila kusahau misamaha ya kodi iliyozidi ukubwa uchumi wetu.

Mama lazima awe makini, tunataka wawekezaji lakini sio kwa gharama ya kipato chetu na maendeleo yetu.
Kama alikuta nchi imeoza yeye amefanya nini??? Mbona uwekezaji ndo umekufa??? Watu hawana ajira kwa sera zake mbovu??? Makampuni yamefunga biashara na kuondoka??? Mbaya zaidi kwa miaka 5 tu aliyokaa madarakani akakopa kuliko miaka 10 yote ya mtangulizi wake??? Alifanya lipi la maana????
 
Kwendeni zenu ilani ya chama ni ile ile Mama anatembea nayo, hata wakati anaondoka JK mabadiliko ya hapa na pale yalikuwepo tuvumiliane kaeni SUB hapo benchi kwanza ili mambo mengine yaendelee.
 
Unapozungumzia hizo awamu ukumbuke kwamba awamu ya Nne ilikuwa na miaka Kumi na awamu ya Tano ilikuwa na miaka Sita tu!
halafu leo mtu anakwambia eti jpm amefanya nini?!!...tofauti ni kubwa sana kati jpm na jk ...jpm vitu vingi vya maendeleo vinaonekana kwa macho bila hata kuuliza ndani ya miaka 5 tu .jk miaka 10 tunaambiwa nchi haina uwezo,umeme hkn,watu wanagawana pesa kwenye masandarusi,rais full kutembea ulaya leo yupo america anapiga picha na boyz to men kesho yupo sijui wapi,ujambazi ukashamiri,madawa ya kulevya eti leo turudi huko thubutu !!! ...wauza ngada na watu wenye maslahi yao ya kuliangamiza taifa kwa manufaa yao binafsi kamwe hawataweza na hata huyo mama akielekea huko atakumbana na nguvu ya umma tu
 
Umakini unahitajika sana katika maamuzi ya mambo makubwa na yenye maslahi kwa Taifa kama ulipaji kodi na Issue ya wawekezaji, vinginevyo tutarudi kule kule kwenye SHAMBA LA BIBI aka BUSINESS AS USUAL.
Tukumbuke, JPM amejitahidi sana kulinda, kutetea na kuendeleza rasilimali za Taifa hili. Amejitahidi sana tena sana.
 
Unataka kutuambia unajua mengi mno kupita Rais Mama Samia? basi ni Maajabu na dunia inaelekea mwisho yaani fukara wa mtaani kama wewe ni zaidi ya Rais?
Mwehu huyo, walitaka kupiga wao kwa kisingizio cha mwekezaji wa ndani. Majangili wakubwa hao. Shubaaamit
 
Kama alikuta nchi imeoza yeye amefanya nini??? Mbona uwekezaji ndo umekufa??? Watu hawana ajira kwa sera zake mbovu??? Makampuni yamefunga biashara na kuondoka??? Mbaya zaidi kwa miaka 5 tu aliyokaa madarakani akakopa kuliko miaka 10 yote ya mtangulizi wake??? Alifanya lipi la maana????

Ukiunda biashara ambayo iko kwenye misingi ya kukwepa kodi na kilaghai mapato yake unategema hiyo biashara itadumu ndani ya mfumo wa kulipa kodi halali na kupata leseni kihalali?
 
Back
Top Bottom