Rais akemea mawaziri kutoa ajira kwa kujuana

Kwa Ufupi:

Rais wa JMT mh Samia Suluhu Hassan amewataka Mawaziri na Viongozi wengine wa serikali kutoajiri Marafiki au Ndugu katika Taasisi za serikali.

Source: TBC
 
Wateule waishaambiwa kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake wasisumbuliwe tafadhali
 
Rais Samia amewakemea mawaziri na manaibu Waziri kuajiri ndugu au marafiki zao katika taasisi za wizara wanazozisimamia kwa kuwa zinaua taasisi

Aidha amewataka kuondoleana ‘muhali’ kwa maana ya kutooneana haya kuambiana inapotokea mtu amekosea katika utendaji wake

Rais amesema muhali na ajira za kujuana zinaua taasisi na kuwataka mawaziri wazingatie hilo
Yeye amejaza wazaramo kwenye cabinet yake ikiwa ni pamoja na mkwewe
 
Tatizo ajira hazitoshi. Ndiyo maana zinatoka kwa kujuana. Chanzo cha tatizo ni sera za ujamaa na kujitegemea ambazo zinafilisi sekta binafsi. Matokeo yake ajira zinabakia serikalini halafu ni chache kukidhi haja za ajira za mamilioni ya Watanzania.
 
Rais anaehamasisha ufisadi kwenye nchi hana credibility ya kukemea mawaziri wanaotoa ajira kwa kujuana.
 
KUMBE SIKUHIZI AJIRA HAZIFANYWI KUPITIA TUME YA AJIRA
Hapa nakumbuka alisema hakuna mkamilifu, na anayomafaili ya mapungufu ya Kila mmoja, pia hakuna mkamilifu ila kunakupishana Kwa viwango vya ukamilifu tu. Hivyo ni kuangalia mapungufu ya kiongozi yanaathiri vipi utendaji wa majukumu yake ya msingi/kazi yake🤔.
 
Tatizo ajira hazitoshi. Ndiyo maana zinatoka kwa kujuana. Chanzo cha tatizo ni sera za ujamaa na kujitegemea ambazo zinafilisi sekta binafsi. Matokeo yake ajira zinabakia serikalini halafu ni chache kukidhi haja za ajira za mamilioni ya Watanzania.
Huo ndio ukweli wote
 
Back
Top Bottom