PAZIA 3
JF-Expert Member
- Jan 30, 2018
- 1,070
- 1,842
Hii ni turufu nzuri kwa mwanasiasa, natamani kusikia Mgombea yeyote wa Urais akilizungumzia hili, licha ya baadhi ya maeneo kukosa maji, haiwezi kuhalalisha maeneo yenye maji ya bomba kuuziwa Tsh 1200/= kwa unit ilhali tukijua maji ni uhai lazima yatumike Kila muda. Rais ajae alimulike hili kwani kuna maeneo fulani watu wamefungia bomba za maji na wakazi wa maeneo Yale hawaishi kulumbana na kuuziana maji kwa Bei kubwa.
Kitu kingine kwa kuongeza, Rais ajae arekebishe mfumo wa matumizi na ugawaji wa hela za TASAF. Sijawahi kuunga mkono namna ya utoaji wa pesa za TASAF kwa kuwapa pesa mkononi wananchi maskini.
Kwa kuhitimisha, nashauri Raisi ajae, akatae mfumo wa ukandamizaji wa TCU kwa wahitimu was fomu 6 kuomba kuchaguliwa kujiunga na vyuo vikuu kwa kulipia Tsh 10000/=kwa Kila chuo unachoomba. Kuna vijana mpaka Sasa wametumia zaidi ya elfu 70 kuomba kuchaguliwa kujiunga na chuo kikuu. Hili silisikii likizungumziwa na wanasiasa kabisa.
Naomba kuwasilisha