Rais ajaye na hatima ya Gas iwe hivi..

MkamaP

JF-Expert Member
Jan 27, 2007
8,140
3,209
Nafikiri Rais ajaye si lazima sana awatoze kodi wachimbaji wa madini ama gas.
Ila kwa vile watanzania wengi ktk nyadhifa zao wamekuwa wapiga madili naamini hata hiyo kodi itapigwa dili tu. Ningeshauri rais ajaye afanye hivi, ila huu ni muono wangu tu.

1. Machimbo ya madini nayapa jina A, wapewe ila masharti watujengee miundo mbinu ya uhakika ya umeme, bila umeme kukatika kwa kipindi cha miaka 50. ukikatika ni maintanance ya kawaida.
2. Machimbo ya madini nayapa jina B, wapewe bila kukata kodi, ila watujengee miundo mbinu ya reli kuunganisha mikoa yote hadi mipakani mwa nchi jirani kwa standard gauge kama za ulaya. Na train zenyewe ziwe zinatumia umeme usiokatika kutokana kwa sababu point A imekamilika.
3. Machimbo ya madini nayapa jina C, wapewe bila kukata kodi ila watujengee bandari za standard za kimataifa pale Bagamoyo, Mtwara na Tanga na barabara pia.
4. Machimbo ya madini nayapa jina D, wapewe bila kukata kodi lakini waturekebishie shule zetu zote ziwe na vitendea kazi na kuongeza zingine na vyuo vikuu kila mkoa angalau vyuo viwili kila mkoa.
5. Machimbo ya madini nayapa jina D, wapewe waturekebishie miundo mbinu yetu ya afya nk.

Sasa Serikali watachofanya, kwenye bandari zetu ni kushusha ushuru wa kuingiza bidhaa hadi 20%, yani mass bussiness, unahakikisha bidhaa karibu zote za afrika zinapitia hapa bongo.

Unahakikisha kila anayetumia barabara zetu na reli zetu wanalipia kwa vile waafrika wengi watakuja kuchukua mizigo yao.
Unahakikisha Reli zetu zinatumiwa na mashirika tofauti tofauti yani kama barabara, mtu anayetaka kuleta mabehewa yake na train ruhusa kutumia reli, ila tu alipe ushuru. Hivyo, Train za nchi jirani ziruhusiwe kuingia kutumia reli zetu kusiwepo na monopoly ya kimizengwe.

Wakafanya hivyo naamini ajira zitakuja nyingi by DEFAULT na hawatahangaika sana kuwapiga ushuru wafanyakazi na wafanya biashara wa karanga.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom