Rais ajaye huenda akawa mwenye uoga mwingi

MWONA MBALI

JF-Expert Member
Oct 7, 2016
460
610
Nikiangalia kwa aina ya viongozi tulio nao wakati huu, ni uwazi kuwa wengi hawajiamini katika kutekeleza majukumu yao, wamejawa na uoga mwingi tena wasio jiamini.

Na kwa kuwa sasa ni Tanzania ya Kijani sina mashaka kabisa kuwa ni mwana CCM tena atakae kuwa rais wetu ajae. shida inayo nijia kichwani ni juu ya aina ya viongozi tulio nao sasa, wengi ni wakujipendekeza, anayo yazungumza ukimwangalia kabisa sio anayo yaamini, wamejawa hofu hivi. kuna kaugonjwa kwa viongozi wa kisiasa wa kijani kamewakuta, inasemekana hata kualikana kwa mazungumzo wanahofu, hawaziamini hata simu zao,

Kwa ugonjwa huu ulioingia kwa wanasiasa wetu wa KIJANI, TUJIANDAE HUENDA TUKAPATA RAIS MUOGA MWENYE HOFU NYINGI, ANAEWEZA KUBADILIKABADILIKA IKAWA TUMEPATA HASARA.

NATAFAKARI.
 
Ukiwa kiongozi ambaye upo chini ya kiongozi mwingine lazima uwe Kama maji yaani nazungumzia FLEXIBILITY Hivyo Basi uongozi hubadili mtu, leo mpole kesho mkali
 
Nikiangalia kwa aina ya viongozi tulio nao wakati huu, ni uwazi kuwa wengi hawajiamini katika kutekeleza majukumu yao, wamejawa na uoga mwingi tena wasio jiamini...
Pamoja na "MATAGA" wa marekani kuandamana wakitaka bwana "TRUMP" asalie madarakani pamoja na kushindwa, ila hujasikia IGP wakule akisema watapigwa kipigo cha mbwa koko, makamo wa raisi Mike Pence yani mama Samia Suluhu Wakule kasema "MATAGA" hao wanaiaibisha MAREKANI.

Ccm na vibaraka wenu mna la kujifunza.
 
Ukiwa kiongozi ambaye upo chini ya kiongozi mwingine lazima uwe Kama maji yaani nazungumzia FLEXIBILITY Hivyo Basi uongozi hubadili mtu, leo mpole kesho mkali
Sema tupate mtu ambae ni civilized educated na matured ambae atokuwa muoga
 
Sidhani kabisa kama Rais ajaye wa JMT Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na Waziri Mkuu wake Mtarajiwa Waziri Jaffo watakuwa na huu Uwoga wako.
Kama kuna kiukweli hapa ila naamini ikitokea hivi mambo yatakuwa safi saana.
 
Sema ajae ajiandae kulipa mafidia kibao kesi zitakuwa nyingi Sana na zitaigharimu Sana serikali ijayo kulipa fidia watu walioumizwa na awamu isiyopenda haki.Ikiwemo watu waliobomolewa nyumba zao itabidi kuwalipa fidia inastakiwa serikali na sio mtawala rejea kesi ya mzungu aliyekamata ndege enzi za Nyerere
 
Sidhani kabisa kama Rais ajaye wa JMT Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na Waziri Mkuu wake Mtarajiwa Waziri Jaffo watakuwa na huu Uwoga wako.
Hii combination imekaa poa Sana.. sema kale kamchezo kao pale lumumba ka mkristo mwislamu and vise versa ndo kanaweza kakakwamisha hlo wazo lako
 
Kuna uzi humu (ulipostiwa 2013) uliwahi kutolewa utabiri wa utawala wa Rais wa sasa ambapo huo utabiri ni wa kweli kwa asilimia karibia zote.

Ngoja tuone na huu.
 
Hata Magufuli kipindi kile cha mwanzoni mwa urais wake alikuwa ana uoga uoga hadi watu wakawa wanasema nchi inaongozwa na JK kwa remote,ila sasa tunaongea vingine kabisa.
 
Kwa katiba hii hakuna uwezekano wa kuwa na rais anayewaogopa wananchi wake.
Tatizo si katiba. Tatizo ni uwezo wa kuchukua hatua iwapo katiba itavunjwa.
Ijapokuwa yeyote mwenye hofu ya MUNGU atakuwa na hofu wananchi wake wakiwa na matatizo hata kwa katiba hii iliyopo.
 
Tatizo si katiba. Tatizo ni uwezo wa kuchukua hatua iwapo katiba itavunjwa.
Ijapokuwa yeyote mwenye hofu ya MUNGU atakuwa na hofu wananchi wake wakiwa na matatizo hata kwa katiba hii iliyopo.

Unachukuaje hatua kwa rais ambaye hashitakiwi akiwa au ametoka madarakani?
 
Back
Top Bottom