Rais ajaye baada ya Magufuli atalipa madeni mengi sana

Kuna maamuzi mengi yanayofanywa kwa ubabe na Serikali ya Awamu ya 5 ambayo yanakiuka sheria sana. Yana athari kubwa sana kwa wananchi wanao tendewa. Rais ajaye baada ya JPM ajiandae kutumia makusanyo ya TRA kulipia madeni yafuatayo;

1. Deni la la Taifa linapanda kila kukicha kwa kuwa miradi mingi kama SGR na STIGLERS. Miradi hii itakuwa itakamilika kati ya 2023 na 2025, hivyo repayment period itakuwa ndiyo inaanza. Kwa hiyo Asilimia kubwa ya makusanyo ya TRA itaelekezwa kulipa deni

2. Fidia kwa waliobomolewa Ubungo-Kibamba huku wakiwa na zuio la Mahakama. Kwa wakati huu Mahakama ziko mfukoni mwa JPM ndiyo maana Serikali haijatoa fidia na imekaidi zuio la Mahakama. Itakapo kuja Serikali inayo jali haki za binadamu, wale wote wenye nyaraka zao sahihi za Kimahakama au hati za umiliki watafidiwa tu. Hata kama watakuwa wamefariki, warithi wao watapata haki zao.

3. Mafisadi wa kutakatisha fedha feki. Watu wengi amewatupa rumande kwa kudai kuwa ni mafisadi na wametakatisha fedha lakini miaka 3 kesi haziendelei kwa kuwa bado uchunguzi unaendelea. Ukiacha hawa walioingia plea bargain na wakatoka, wale waliobaki watadai fidia tu na watapata.

4. Wafanya biashara ambao wananyang'anywa mali zao kwa sababu ya chuki binafsi tu.

Ushauri wangu kwa Wa Tanzania ni kwamba watunze rekodi tu, hii hali ya dhuluma haiwezi kuwa ya kudumu. Ipo siku utakuja utawala unaojali utawala wa sheria utawafidia
Utabiri umetimia
 
Back
Top Bottom