Rais ajaye aongezewe nafasi 20 zaidi za teuzi za Wabunge, Bunge lijalo litajaa vihiyo wengi, tukifuata Demokrasia ya Kura za Maoni

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,753
7,075
Baada ya vita kati ya wasomi na wajumbe kuisha, inaonekana wajumbe kushinda kete ya kuwaingiza wenzao kwenye bunge. Inaelekea wasomi hawajaleta tija kwao kutokana na kupwya kwa bunge lililopita. Kwa ufupi wa kulaumiwa ni hawa viongozi yani Ndugai na tulia walivyoshindwa kusimamia hhoja wakasimamia viroja.

Imefika sasa bunge litajaa watu wengi wasio na weredi, kwa kuliona hilo naona bora rais aongezewe watu wa akiba wataoweza kumsaidi kwenye shughuli zake kwani atashindwa kuteua wabunge imara wa kuzikabili wizara zake ziweze kufanya kazi walizotumwa kwa weledi.

Tumeona mshike, shike wa wajumbe wakitegemea sana hongo kutoka kwa wenye nazo, wengine wakitegemea zaidi ushwahiba na kuleta chuki sana zidi ya wasomi. Pengine kwa sasa wasomi kukimbilia siasa wameona ndio mtoko sahihi kwa vile wanapata mshahara mdogo ilihari wasiosoma wabunge wengi wanawazidi ukwasi.

Bunge lijalo litakuwa la miemuko zaidi kwani wabunge wengi wako katika hali mbaya kifedha hivyo watakuwa wanajipendekeza sana kwa Serikali kuliko wananchi ili wapate teuzi.

Tumeanza kuwaona wakifikia kusema rais aongezewe muda wakati yeye anasema imetosha,
 
Wabunge wapi wenye hali mbaya kifedha si bado hatujachagua? au unadhani wote watarejea bungeni
 
Trend ni kupungaza wateule wa Raisi au viti maalum. Kama bado huchagui the right candidate imekula kwako.
 
Trend ni kupungaza wateule wa Raisi au viti maalum. Kama bado huchagui the right candidate imekula kwako.
wapunguze viti maalum vya NEC waweke vya Rais maana mwakani atakosa wa kuteua maana wabunge wengi watakuwa vilaza
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom