Rais ajaye afanye maamuzi magumu

Mkumbwa Jr

JF-Expert Member
Mar 23, 2016
2,370
3,148
Baada ya Rais kuapishwa na kulifungua bunge, jambo la msingi ili kutengeneza usawa afanye yafuatayo
Apunguze maslahi ya wabunge
Darasa la saba wasiingie bungeni
Abadili sheria viti maalum vifutwe
Walipwe kutokana na elimu zao
Walipwe mafao yao baada ya kutimiza miaka 60. Hapa watapigania fao la kujitoa

Hatua hiyo itatengeneza usawa na wabunge watawapigania wananchi wao na wao wenyewe
 
Bahati mbaya sana hakuna atakayepitisha muswada kama huo.

Siyo wabunge wa upinzani wala CCM.
Waambiwe wakigoma bunge livunjwe ili warudi kwetu wananchi Tena wapige kura ya wazi katika kuafiki au kutoafiki. Hawawasemei wananchi ipasavyo kwakua wao wanavimbiwa.

Pia maslahi yakiwa madogo wanasiasa wenye nia ya dhati watajulikana na wale wa maslahi yao watajulikana
 
Wazo zuri lakini sidhani kama kuna kiongozi wa siasa nchini anauchungu na wananchi kiasi hiki. Wao wanakubali mtu apewe mafao akifikisha miaka 60 lakini wao wanatka mafao yao baada ya miaka mitano. So sad
 
Nakubaliana wewe, kupunguzwa kwa maslahi yao, ila kulipwa kutokana na elimu zao, hapo sikuliani na wewe. kazi ya bunge ni moja, kule hawafanyi kazi kutokana na elimu zao wala taaluma, walizonazo.

kama kuna hoja ya kuijadili wote wataijadili, hebu fikilia wasomi waluopo bungeni wamelisaidia nini bunge. Utofauti ninaouona bungeni bila kujali elimu ya mtu kwenye kuchangia/kuwasilisha ni yuko mlengo gani basi.
 
Tatizo Rais Magufuli akitaka kufanya wabunge wa Chadema wataenda kushtaki kwa Robert
 
Walipwe kulingana na elimu?Ipi hiyo?Kwa hiyo hapo Mwakyembe alitakiwa kulipwa zaidi kwa kuwa na shahada nne?

Haya ni mawazo ya mwendokasi haya.Watu mnasoma mivyeti miingi mikubwa mnasubiria serikali ndiyo ilipe vyeti vyenu?

Mmeshindwa kufanya mapinduzi Kutokana na vyeti vyenu kwa kuwa kuna tofauti kubwa kati ya kuwa na elimu na kuwa na vyeti.Kuna tofauti kubwa sana kati ya kuwa na elimu na kuwa na akili.

Wengi hamna akili ndio maana mmeshindwa kuwa wabunifu ila mna uwezo wa kukumbuka vitu tu.Hata kasuku anakumbuka.Sasa mnataka mkalipwe pesa za bure huko bungeni baada ya kupigika huku mtaani?
 
Nakubaliana wewe, kupunguzwa kwa maslahi yao, ila kulipwa kutokana na elimu zao, hapo sikuliani na wewe.
kazi ya bunge ni moja, kule hawafanyi kazi kutokana na elimu zao wala taaluma, walizonazo.
kama kuna hoja ya kuijadili wote wataijadili, hebu fikilia wasomi waluopo bungeni wamelisaidia nini bunge.
Utofauti ninaouona bungeni bila kujali elimu ya mtu kwenye kuchangia/kuwasilisha ni yuko mlengo gani basi.
Mbona huko maofisini na makazini watu wanafanya kazi zinazofanana lakini mishahara tofauti mfano jeshi,walimu
 
As
Walipwe kulingana na elimu?Ipi hiyo?Kwa hiyo hapo Mwakyembe alitakiwa kulipwa zaidi kwa kuwa na shahada nne?

Haya ni mawazo ya mwendokasi haya.Watu mnasoma mivyeti miingi mikubwa mnasubiria serikali ndiyo ilipe vyeti vyenu?

Mmeshindwa kufanya mapinduzi Kutokana na vyeti vyenu kwa kuwa kuna tofauti kubwa kati ya kuwa na elimu na kuwa na vyeti.Kuna tofauti kubwa sana kati ya kuwa na elimu na kuwa na akili.
Wengi hamna akili ndio maana mmeshindwa kuwa wabunifu ila mna uwezo wa kukumbuka vitu tu.Hata kasuku anakumbuka.Sasa mnataka mkalipwe pesa za bure huko bungeni baada ya kupigika huku mtaani?
Asante kwa mchango wako mkuu,upo vizuri kwa kuwasilisha mawazo yako
 
QUOTE="Bia yetu, post: 37093219, member: 591117"]
Tatizo Rais Magufuli akitaka kufanya wabunge wa Chadema wataenda kushtaki kwa Robert
[/QUOTE]
Kwanini amuogope sasa
 
Nakubaliana wewe, kupunguzwa kwa maslahi yao, ila kulipwa kutokana na elimu zao, hapo sikuliani na wewe.
kazi ya bunge ni moja, kule hawafanyi kazi kutokana na elimu zao wala taaluma, walizonazo.
kama kuna hoja ya kuijadili wote wataijadili, hebu fikilia wasomi waluopo bungeni wamelisaidia nini bunge.
Utofauti ninaouona bungeni bila kujali elimu ya mtu kwenye kuchangia/kuwasilisha ni yuko mlengo gani basi.
Walipwe kulingana na elimu zao Mkuu, mbona mwalimu wa shule yamsingi, mwalimu wa form one mpaka four(diploma) na mwalimu Mwenye shahada mishahara inatofautiana Mkuu?. Posho ndio ziwe sawa lkn mishahara itofautiane.
 
Baada ya Rais kuapishwa na kulifungua bunge, jambo la msingi ili kutengeneza usawa afanye yafuatayo
Apunguze maslahi ya wabunge
Darasa la saba wasiingie bungeni
Abadili sheria viti maalum vifutwe
Walipwe kutokana na elimu zao
Walipwe mafao yao baada ya kutimiza miaka 60. Hapa watapigania fao la kujitoa

Hatua hiyo itatengeneza usawa na wabunge watawapigania wananchi wao na wao wenyewe
Uzi bora kabisa huu, big up mkuu
 
Nakubaliana wewe, kupunguzwa kwa maslahi yao, ila kulipwa kutokana na elimu zao, hapo sikuliani na wewe.
kazi ya bunge ni moja, kule hawafanyi kazi kutokana na elimu zao wala taaluma, walizonazo.
kama kuna hoja ya kuijadili wote wataijadili, hebu fikilia wasomi waluopo bungeni wamelisaidia nini bunge.
Utofauti ninaouona bungeni bila kujali elimu ya mtu kwenye kuchangia/kuwasilisha ni yuko mlengo gani basi.
Hapa ndipo wengi sana mnapobugi eti kudhani kwamba mbunge kama Kibajaji anauwezo wa kutekeleza effectively majukumu ya kibunge, hasa kujadili miswaada, hotuba za mawaziri na kutunga sheria. Elimu is everything, ndiyo maana tukasema elimu ni ufunguo wa maisha. Hoja yako kwamba waliosoma wamefanya nini bungeni jibu lake ni kwamba kwanza huko bungeni kwa sasa vilaza ndiyo wengi (la saba, na form 4) wenye degree ni wachache..... Sasa hawa wasomi wachache wanaburuzwa na vilaza kama akina Msukuma, Kibajaji etc kwa sababu wanajua kubwabwaja na kutukana wapinzani. Angalia walivyofanya Prof Muhongo, Tibaijuja etc
 
Walipwe kulingana na elimu?Ipi hiyo?Kwa hiyo hapo Mwakyembe alitakiwa kulipwa zaidi kwa kuwa na shahada nne?

Haya ni mawazo ya mwendokasi haya.Watu mnasoma mivyeti miingi mikubwa mnasubiria serikali ndiyo ilipe vyeti vyenu?

Mmeshindwa kufanya mapinduzi Kutokana na vyeti vyenu kwa kuwa kuna tofauti kubwa kati ya kuwa na elimu na kuwa na vyeti.Kuna tofauti kubwa sana kati ya kuwa na elimu na kuwa na akili.
Wengi hamna akili ndio maana mmeshindwa kuwa wabunifu ila mna uwezo wa kukumbuka vitu tu.Hata kasuku anakumbuka.Sasa mnataka mkalipwe pesa za bure huko bungeni baada ya kupigika huku mtaani?
Wewe unasumbuliwa na wivu tuu, wenzio walipokuwa wakienda shule wewe unakimbilia vijiweni. Angalia mchango wa wanasheria bungeni kama akina Lissu, marehemu Deo filikunkombe, Hussain Bashe, Mdee etc kwenye kujadili miswaada migumu ulinganishe na akina Msukuma, halafu eti unataka walipwe sawa? Mbona hushangai kwamba madaktari bingwa mishahara yao siyo sawa na ya manesi au madereva??
 
Wasilipwe mshahara wa kila mwezi kama wafanyakazi bali walipwe posho wanapohudhuria vikao au shughuli za kibunge kwenye kamati zao. Huo mshahara wanaopewa kila mwezi hawaustahili na ni rushwa.
Hii nayo ni hoja nzuri sana
 
Baada ya Rais kuapishwa na kulifungua bunge, jambo la msingi ili kutengeneza usawa afanye yafuatayo
Apunguze maslahi ya wabunge
Darasa la saba wasiingie bungeni
Abadili sheria viti maalum vifutwe
Walipwe kutokana na elimu zao
Walipwe mafao yao baada ya kutimiza miaka 60. Hapa watapigania fao la kujitoa

Hatua hiyo itatengeneza usawa na wabunge watawapigania wananchi wao na wao wenyewe
Huko ndio kutumia madaraka vibaya na kutokuheshimu mihimili ya nchi hii ambayo kwa Magufuli WaTz wanachukulia ni sawa. Udikteta ndio huo!
 
Back
Top Bottom