Rais afanya teuzi za Makatibu Wakuu na Wakuu wa Taasisi. Gerson Msigwa atolewa Ikulu, Dotto James ahamishwa. TPA, TCRA na TRA zapata wakuu wapya

Najua ni mahitaji ya lazima ya sasa ila naona kama NCHI, tunatumia muda mwingi kuteua, kuapisha na kujadili nyazifa za wanasiasa na watendaji wa serikali. Haya mambo ukiyatafakari sana utagundua hayatuongezei tija kihivyo na yanatupotezea muda na kutuingiza gharama nyingi zisizo na maana sana.

Ila huo ni mtazamo wangu tu.
Na mtazamo wako uko sahihi kabisa.ni mambo ya kipumbavu kabisa tunayokazana nayo
 
Watu wa clearing wanalia sana

Ova
Walibanwa Sana saizi zimebaki kampuni chache. Ukipita mitaa ya Clock Tower,Samora na Stesheni kumepoa huoni tena raia wakiwa wamevaa shati za light blue mikononi wameshika bahasha za documents wakikimbizana.
 
Wakati mwingine akili ndo inatakiwa kuongoza kichwa chako hv kuna jamii gani kwa Tanzania kwa sasa ambayo haina wasomi ?
Wapo ila sio wabobezi..tukubali tukatae kuna jamii ziko na wasomi wengi kuliko zingine hili huwezi pinga..mfano wahaya na wazaramo..lazima utapata wahaya wengi ni wasomi wabobezi wa ngazi za juu ukilinganisha na wazaramo..si leti ukabila ama udini ila ki uhalisia iko hivyo ukubali ukatae..chamsingi jamii zetu sasa zijikite kujipatia elimu ya kutosha.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wapo ila sio wabobezi..tukubali tukatae kuna jamii ziko na wasomi wengi kuliko zingine hili huwezi pinga..mfano wahaya na wazaramo..lazima utapata wahaya wengi ni wasomi wabobezi wa ngazi za juu ukilinganisha na wazaramo..si leti ukabila ama udini ila ki uhalisia iko hivyo ukubali ukatae..chamsingi jamii zetu sasa zijikite kujipatia elimu ya kutosha.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu yangu kwa Dunia ya sasa ni ngumu sana watu wameamka wanapeleka watu shule unaposema wabobevu unamaanisha nini? Nitajie wote waliochaguliwa kuanzia makatibu wakuu,wakurugenzi nitajie mmoja tu ambae utasema ni mbobevu ambapo huwezi kumpata katika jamii nyingine.
 
Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa makatibu wakuu, naibu makatibu wakuu na wakuu wa taasisi mbalimbali za serikali.

=======

Baadhi ya mabadiliko

- Alphayo Kidata ameteuliwa kuwa kamishna wa mamlaka ya mapato Tanzania, nafasi aliyowahi kuitumikia kabla na uteuzi wake kutenguliwa na Rais Magufuli.

- Erick Hamis ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya usimamizi wa bandari baada ya aliyekuwa mkurugenzi wake, Deusdedith Kakoko kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi

- Gerson Msigwa ameteuliwa kuwa mkurugenzi wa idara ya habari kuchukua nafasi ya Dkt. Hassan Abbas ambae amebakia na nafasi yake ya katibu mkuu wizara ya habari. Kabla Msigwa alikuwa mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais, Ikulu

- Dkt. Jabir Kuwe ameteuliwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Eng. Kilaba.

Japo mimi niko kwenye lile kundi linalosisitiza Samia asipangiwe, aachwe afanye vile anaona inafaa, lakini kuhusu huu uteuzi usiozingatia kabisa gender balance, honesty, I don't believe huyu ni Samia huyu niliye zungumza hapa!.

Jee inawezekana Tanzania ni hatuna wanawake wa kutosheleza gender balance?, au wapo wamesahaulika?.
P
 
Mara nyingi nimekuwa nikijiuliza swali moja tu, hao viongozi wetu wanao teuliwa ktk nafasi mbali mbali kama vile Mawaziri, Manaibu, wakurugenzi n.k wote wanaonekana wana faaa na wana ujuzi wa kutosha kufanya kazi kwa mafanikio makubwa, lkn mbele ya safari unaanza kusikia mtu huyu huyu anaanza kutuhumiwa kwa kashfa za UBADHIRIFU wa mali za umma na RUSHWA.
Swali;
1. Je? nini haswa kinacho wafanya baadhi ya wateuliwa kubadilika mbele ya safari na kupoteza Uaminifu na kuwa wabadhirifu wa mali za Umma?
 
Huyu daktari nina wasiwasi nae sana, kama nakosea Mungu anisamehe. Kwanza najiuliza alikuwa nani kabla hajawa daktari wa Rais?
Alikuwa Dr Bugando, akahamia Chato kumhudumia Rais ndipo akapanda kuwa Katibu Mkuu Afya kipindi Corona imeitandika nchi kwa mara ya kwanza akimtoa Mama aliyekuwepo na naibu Dr Ndugulile wakaondolewa, alibaki na Ummy
yeye alisema Corona ni mafua makali yataondoka kwa nyungu na ndiye aliyeratibu na kudai hata papai lina Corona
Maana yake angekuwa mkweli na kukemea km wenzake Rais wetu angevaa barakoa na kujikinga, huenda mzigo wote walimuacha peke yake ili athibitishe mpendwa hatunaye tena kwa ugonjwa
 
Nasubiria sasa list ifuatayo

1: RCs
2: Mabalozi
3: RAS
4: DCs
5: DAS
6: DEDs

Yaani hapo serikali itakaa safi kabisa.. Watu wenye sifa sifa kama Chalamila, Sabaya & wenye similar worst behaviours, wajiandae tu mapema. Huwezi kuwa na watu wa ajabu ajabu katika utumishi wa umma kama hao.
Exemplary correct. Tena hiyo list ina watu wabovu wengi mno.
 
Kiukweli Bado upande wangu Siamini kama Msemaji wa Ikulu Ofisi MOJA tu Anaweza kuwa Mkubwa kimamlaka na kimaslahi Kumzidi MSEMAJI MKUU WA SELIKALI. ninavyojua Mimi Msemaji wa Ikulu Hawezi kwenda kuongea Issue yoyote inayohusu wizara yoyote au Tukio lolote la Kitaifa Yeye Atasubiri issue ya Ikulu tu.
Msemaji Mkuu wa Serikali ni mtu mkubwa sana kuliko mnavyofikiria vijana.
Hiyo post ni imminent sana kwa exposure ya nchi na hata usalama wake. Msiichukulie poa kabisa
 
Back
Top Bottom