Rais achia mikutano ya hadhara, tushindane kwa hoja

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,379
MIKUTANO IACHIWE, TUSHINDANE KWA HOJA.

Mikutano ya Vyama vya Siasa iachiwe huru na vyama vyote vishindane kwa hoja. Kitendo cha kuzuia ni ishara upande mmoja au mwingine hauwezi kujenga hoja. Mikutano inasaidia kupata mikakati mipya ya kujenga Nchi.

Ni vyema kila chama kikajiandaa kwa kuweka watu makini watakao pambana kwa hoja na sio kuwa waoga, kwa nidhamu ya woga. Nawatakia mihadhara safi. Kuzuia mikutano wakati mwingine kunaweza kusababisha Vurugu na damu kumwagika.

Deogratius Kisandu
13.Jan.2017
 
Nchi gani baada ya uchaguzi bado kampeni zikaendelea ?uchaguzi umeshakwisha sasa waacheni mliowachagua wawafanyie kazi mliyowatuma na ww Deogratius Kisandu tafuta kazi ya kufanya siasa inawakati wake miezi 3 ya kufanya siasa ilkwisha tarehe 25 Oct 2015 maana mnatangaza operation tu Last time I checked wanaofanya operation ni hospital na vyombo vya ulinzi na usalama sijawai kusikia vyama vya siasa vinafanya operation na kazi ya vyama vya upinzani ni kuishauri serikali iliyo madarakani tu, mapambano ni kazi ya taasisi za kianaharakati au NGo
 
Acha kwanza tutafute ugali, hiyo mikutano, operation na maandamano iruhusiwe kwenye vipindi vya uchaguzi tu.
 
Kama issue ni kushindanisha hoja, nafasi wanayo bungeni na kwenye vikao vya madiwani
 
Acha kwanza tutafute ugali, hiyo mikutano, operation na maandamano iruhusiwe kwenye vipindi vya uchaguzi tu.

Mbona mnakwenda mpirani na kwenye matamasha inawazuia kufanya kazi? Hiyo ni hoja dhaifu, mikutano ni nafasi ya kuwaeleza wananchi wafanye nini kwa maendeleo yao ndio maana imeruhusiwa kikatiba.
Au unataka kusema waliotunga katiba walikuwa wajinga kuliweka hilo? Na kama walikuwa wajinga kuliweka hilo kwa nini ujinga huo usiwe katika na mambo mengine yakiwemo uwezo na mamlaka ya viongozi?
 
Nchi gani baada ya uchaguzi bado kampeni zikaendelea ?uchaguzi umeshakwisha sasa waacheni mliowachagua wawafanyie kazi mliyowatuma na ww Deogratius Kisandu tafuta kazi ya kufanya siasa inawakati wake miezi 3 ya kufanya siasa ilkwisha tarehe 25 Oct 2015 maana mnatangaza operation tu Last time I checked wanaofanya operation ni hospital na vyombo vya ulinzi na usalama sijawai kusikia vyama vya siasa vinafanya operation na kazi ya vyama vya upinzani ni kuishauri serikali iliyo madarakani tu, mapambano ni kazi ya taasisi za kianaharakati au NGo
Pelekeni mswada bungeni wa mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa ili mpate uhalali wa kuzuia kikatiba na sio kufanya vitisho eti kisa mna dola
 
Nchi gani baada ya uchaguzi bado kampeni zikaendelea ?uchaguzi umeshakwisha sasa waacheni mliowachagua wawafanyie kazi mliyowatuma na ww Deogratius Kisandu tafuta kazi ya kufanya siasa inawakati wake miezi 3 ya kufanya siasa ilkwisha tarehe 25 Oct 2015 maana mnatangaza operation tu Last time I checked wanaofanya operation ni hospital na vyombo vya ulinzi na usalama sijawai kusikia vyama vya siasa vinafanya operation na kazi ya vyama vya upinzani ni kuishauri serikali iliyo madarakani tu, mapambano ni kazi ya taasisi za kianaharakati au NGo
yy mbona anafanya siasa....si akae magogoni afanye kazi wananchi tutakiona kilichofanywa.......
 
Nchi gani baada ya uchaguzi bado kampeni zikaendelea ?uchaguzi umeshakwisha sasa waacheni mliowachagua wawafanyie kazi mliyowatuma na ww Deogratius Kisandu tafuta kazi ya kufanya siasa inawakati wake miezi 3 ya kufanya siasa ilkwisha tarehe 25 Oct 2015 maana mnatangaza operation tu Last time I checked wanaofanya operation ni hospital na vyombo vya ulinzi na usalama sijawai kusikia vyama vya siasa vinafanya operation na kazi ya vyama vya upinzani ni kuishauri serikali iliyo madarakani tu, mapambano ni kazi ya taasisi za kianaharakati au NGo
Huna unalojua kuhusu siasa na maendeleo ya nchi. Kwa kukusaidia sana itafute hotuba ya juzi tu ya Rais Barack Obama wakati akiaga Taifa lake... Kama lugha tatizo tafuta mtu akufafanulie kwa lugha yako neno kwa neno.
Ikiwa Nchi zilizoendelea zinatambua Demokrasia na Uhuru wa kusema husaidia maendeleo ya nchi itakuwa kwetu tunaopewa hadi msaada wa dawa za malaria?
 
Be loyal to the truth, be loyal to your country. Siasa inatuathiri wakati wote wa maisha yetu, na ndio maana kuna watu KAZI YAO NI SIASA. Kazi ya vyama vya upinzani YES ni kuikosoa serikali, na hayo hufanyika jukwaani sio chumbani.

Bwana izzo wa 'middle class $2', katiba ya Tanzania inavitambua vyama VYA SIASA na sio VYAMA VYA UPINZANI. Hakuna chama kilichosajiliwa kama CHAMA CHA UPINZANI, vyama vimesajiliwa kama VYAMA VYA SIASA vikiwa na malengo ya kufanya siasa na moja kati ya majukumu yake ni KUTOA ELIMU YA URAIA na vina kazi ya KUJIIMARISHA KWA KUJIONGEZEA WANACHAMA kupitia mikutano ya kisiasa, kampeni na makongamano.

Mkuu izzo wa 'middle class $2', unafiki ni maradhi mfano kansa. Miaka ya 90, vyama vya upinzani (ambalo ni jina variable) vilikuwa ni vyenye kulaumiwa, vikiitwa VYAMA VYA MSIMU, yaani vinaonekana wakati wa uchaguzi tu. Sasa tupo kwenye era nyingine ya Watanzania wenye utashi wa kujua na kujifunza, elimu inapigwa marufuku, je katiba inasemaje?

Unaposema kazi ya vyama vya upinzani kazi yake ni kuishauri serikali TU, hiyo ni kwa mujibu wa katiba ipi? Siasa inapozuiliwa jukwaani, ina madhara yake. Kama mwanasiasa mbunge akizuiwa kufanya siasa jukwaani, si ndio mwanzo wa kutuletea siasa bungeni?
 
deo inawezekana una akili lakini siku chache chache unakuwa unavuta bangi kama mwenzako Andrea nyerere
 
Acha kwanza tutafute ugali, hiyo mikutano, operation na maandamano iruhusiwe kwenye vipindi vya uchaguzi tu.
Kwa kauli hii tu inaonesha ugali unaokula anatafuta baba au shemeji yako. Ungekuwa unatafuta ugali wako, hakika ungeona namna harakati za kuutafuta zinavyoathiriwa na political imbalance.

Shemeji yako ana kazi sana.
 
Huna unalojua kuhusu siasa na maendeleo ya nchi. Kwa kukusaidia sana itafute hotuba ya juzi tu ya Rais Barack Obama wakati akiaga Taifa lake... Kama lugha tatizo tafuta mtu akufafanulie kwa lugha yako neno kwa neno.
Ikiwa Nchi zilizoendelea zinatambua Demokrasia na Uhuru wa kusema husaidia maendeleo ya nchi itakuwa kwetu tunaopewa hadi msaada wa dawa za malaria?
Inawezekana ww ndo huna unalojua tofautisha freedom of speech na Democracy nadhani ungefahamu maana ya Democracy =Democracy is a system of government based on the principle that the state's power is vested in the people and may be used by the people or their elected officials under a system of free elections. sasa Niambie maana nyingine ya Democracy mnayoitaka wana ukawa pia freedom of speech sijui mnataka ya aina gani nyinyi kila siku mnasema na kutukana mitandaoni Prophet mpya wa ufipa anafikia mpaka ya kuita watu dictator uchwala lakini mpaka leo yupo uraiani tu na kwake analala vizuri kabisaaaa sasa cjuh mlitaka freedom gani of speech wakt kila mtu anauhuru wa kusema chochote pia sidhani kama FS inaruhusu matusi na kashfa

Pia sijasikia baada ya uchaguzi wa US Democrat au Clinton baada ya kushindwa wakaanzisha operations dhidi ya Trump au Republican ? au ukasikia mikutano ya kisiasa ?
 
Back
Top Bottom