Rais aagiza gereza la Songwe lihamishwe ili kuchimbwa madini ya bati

Madini yaliyopo pale ni madini yenye thamani sana na hutumika kama raw materials za kujenga ndege. Ni madini adimu sana na hupatikana Australia tu. Kampuni ya Afrika Kusini ndio yenye leseni pale Songwe. Wamefanikiwa kumshawishi Rais kuhamisha gereza?..................... haya tusubiri tuone!

Mhe. kwanza nikusaidie, maana wengi wanafikiri umesema Aluminium, hata mimi nilifikiri hivyo kumbe siyo,

madini yanayopatikana pale ni Niobium kuna tani kati ya 85-100 million za Niobium, haya ni madini ambayo hayapatikani kirahisi, Hili ni eneo la Panda hill (kaskazini) mwa eneo hili

Jirani (kusini)na madini haya kuna Aluminium, coal, gypsum, marble na mengine mengi.

Kampuni ninayofanya nayo kazi ndiyo iliyofanya EIA maeneo hayo.

Mkuu uko sahihi, ili ni kosa ambalo wengi huwa wanafanya. si kosa la Zitto tu, wametaja Aluminium kwa sababu may be ni familiar

Ninachoona kuna compound(muunganiko), Aluminium inaweza ikawa pamoja na madini mengine, yote yanaweza yakawa na thamani. Kutokana na kutokujua basi inapelekea wengi kutaja jina la aina moja tu ya madini ambayo yanajulikana.

is very common mistake, ndio ikaleta hata yale matatizo ya mchanga kupelekwa Asia, watu hawajui , wanajua dhahabu, kumbe kuna madini mengi ndani yake, ambayo hayawezi kusafishwa hapa Tz.

Nadhani Ngeleja anaweza akawa anajua vizuri zaidi jina la hiyo compound

Waseme vizuri basi, kwa sababu katika zama hizi za ufisadi, hata an honest mistake inaweza kutafsiriwa kwamba kuna mlungula unatembea na viongozi wanauza madini mengine -pengine hata uranium- na kusingizia aluminum.
 
Ni Uranium sio Aluminium! Janja janja hii ililanza zamani. Kule Buhemba Nyerere alijua kuna Dhahabu na akaweka Jeshi pale ili kusubirisha uvamizi wa wageni ambao alihofu wangewazidi Watz kete wakati ule. Kama mnavyojua Buhemba JKT ilitolewa na miradi mikali mikali ya Meremeta, Tangold nk ilianzishwa kwa taswira tunayoijua wote. Pale Songwe na eneo lingine tena kwenye mkondo huo(some tourist attraction, Daraja LA Mungu), serikali iligundua enzi hizo madini hasa Uranium ( msinidai data source, tafuta geological map ya Tanzania) na kama ilivyokuwa Buhemba walijenga magereza lakini kwa sababu za ajabu Warusi walipewa eneo pale wakajenga kambi ya Jeshi, tuanzie hapo, tuone kama Muungwana kweli ana usongo wa maendeleo au anatafaka kufumua na yeye meremeta yake kama aliyemtangulia.

Nchi hii!!! Eti wabunge wanapewa posho mbilimbili, kamata wahoji, kwa nini usitoe amri kwa mashirika wakome kutoa posho yakaisha...madini ya Songwe ni muhimu lakini ni lazima kuwepo na subira ya kiuwekezaji, serious investors au businessmen hakimbilia kuvuna na kuuza bila ya kufikiria na kesho. Ingekuwa tulikuwa serious huko nyuma kama ninavyopenda ingekuwa, ile almasi na dhahabu kule kanda ya magharibi, TZ ingekuwa tajiri MNO KULIKO ILIVYO.
 
Waseme vizuri basi, kwa sababu katika zama hizi za ufisadi, hata an honest mistake inaweza kutafsiriwa kwamba kuna mlungula unatembea na viongozi wanauza madini mengine -pengine hata uranium- na kusingizia aluminum.

Mkuu uko fast sana!

Nataka niedit post yangu umeshajibu, sikutaka kuweka wazi, ila sijajua faida ya kuficha ukweli.

madini yanayopatikana pale ni Niobium kuna tani kati ya 85-100 million za Niobium, haya ni madini ambayo hayapatikani kirahisi, Hili ni eneo la Panda hill (kaskazini) mwa eneo hili

Jirani (kusini)na madini haya kuna Aluminium, coal, gypsum, marble na mengine mengi.

Kampuni ninayofanya nayo kazi ndiyo iliyofanya EIA maeneo hayo.

JK hajakurupuka, kuhusu kuhamishwa gereza yalikuwa moja ya mapendekezo, na si mzigo wa serikali ni mwekezaji ndiye anatakiwa kufanya hivyo.

Uchunguzi umefanyika miaka kama minne iliyopita na kulikuwa na amend nyingi.

Nakumbuka siyo gereza tu, kuna vitu vingi sana vitahamishwa hamishwa

kuna tofauti sana ya rais kusema jukwaani na hali halisi, sijajua kwa nini, sentensi yake ni kama vile serikali itajenga kwa gharama zake! hii naona imekaa kisiasa zaidi.
 
Mkuu wa idara Magezi,
Inaonekana wewe unajua sana mambo ya mawe je unaweza kutuelimisha hiyo Niobium inatumika kwa shughuli gani na thamani yake ni ipi?
Amani
 
Unaniuliza mimi au weberoya?? angalia vizuri mkuu
 
[ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Niobium"]http://en.wikipedia.org/wiki/Niobium[/ame]

Wikipedia utapata kila kitu

au http://niobium.totallyexplained.com/

kuhusu price search tu utapata pia inaitwa colombium, Ikija kwenye kuuza madin yetu inauma sana, hatuuzi kwa bei unazozifahamu kwenye soko la dunia, soko liko monopoly, na ndio maana ni makampuni makubwa yenye majina ndiyo yanayouza, as the case kwenye Tanzanite.

This needs one crazy president to overcome this, ukiwatetemekea wazungu utauza kwa bei usiyoipenda!

Price;http://www.ferroalloynet.com/catelogs/012000000/price.html
 
  1. Kwa nini amri inapewa Serikali ya Mkoa na si idara husika ya Serikali ambayo ni Magereza? Tangu lini TAMISEMI imekua ikiongoza Magereza?
  2. Kama ni suala la kuwepo madini, je madini ambayo tunayachimba, yameliingizia Taifa letu mapato gani ya kimsingi ambayo yametuondolea Umasikini? Ikiwa mikataba ya uchimbaji Dhahabu na Tanzanite na madini mengine bado ina matatizo na mapendekezo ya Tume ya Bomani hayajafanyiwa kazi, kwa nini Songwe wahamishwe na kule Singida na Dodoma wananchi walazimishwe kukubali uchimbaji wa Dhahabu na Uranium?
  3. Je Serikali (Taifa) itamiliki kwa asilimia ngapi miradi mipya ya uchimbaji madini na hivyo kuondokana na kudhulumiwa na makampuni wekezaji?
  4. Je kuna ulazima gani au haraka gani ya kuchimba madini haya ambayo sisi kama Taifa hatuyatumii kiuzalishaji kupitia viwanda vyetu na kuishia kuyauza nje ya nchi?
  5. Kwa nini tusibuni mfumo mpya ambao hautaishia kwa Tanzania kuchimba madini pekee bali hata kuyatengeneza katika mfumo na bidhaa ambazo zitauzika nje, hivyo kuongeza ajira, kuongeza viwanda na kuongeza pato la Taifa kwa kuuza bidhaa kamili na si mali ghafi?
  6. Gharama za uhamishaji huu, zitachukuliwa na nani?
 
http://en.wikipedia.org/wiki/Niobium

Mkuu wa idara Weborya,
ASante kwa data.
 
Weberoya, asante sana. Jf ina watu muhimu na mmojawapo ni wewe. Asubuhi nilishtuka sana nilipoona amri ya rais. Nikajua sio aluminium. Nikajua sio uranium. Umetegua mapema kweli. Nimefurahi sana. Mjadala uendelee
 
  1. Kwa nini amri inapewa Serikali ya Mkoa na si idara husika ya Serikali ambayo ni Magereza? Tangu lini TAMISEMI imekua ikiongoza Magereza?
  2. Kama ni suala la kuwepo madini, je madini ambayo tunayachimba, yameliingizia Taifa letu mapato gani ya kimsingi ambayo yametuondolea Umasikini? Ikiwa mikataba ya uchimbaji Dhahabu na Tanzanite na madini mengine bado ina matatizo na mapendekezo ya Tume ya Bomani hayajafanyiwa kazi, kwa nini Songwe wahamishwe na kule Singida na Dodoma wananchi walazimishwe kukubali uchimbaji wa Dhahabu na Uranium?
  3. Je Serikali (Taifa) itamiliki kwa asilimia ngapi miradi mipya ya uchimbaji madini na hivyo kuondokana na kudhulumiwa na makampuni wekezaji?
  4. Je kuna ulazima gani au haraka gani ya kuchimba madini haya ambayo sisi kama Taifa hatuyatumii kiuzalishaji kupitia viwanda vyetu na kuishia kuyauza nje ya nchi?
  5. Kwa nini tusibuni mfumo mpya ambao hautaishia kwa Tanzania kuchimba madini pekee bali hata kuyatengeneza katika mfumo na bidhaa ambazo zitauzika nje, hivyo kuongeza ajira, kuongeza viwanda na kuongeza pato la Taifa kwa kuuza bidhaa kamili na si mali ghafi?
  6. Gharama za uhamishaji huu, zitachukuliwa na nani?

Maswali haya na hasa lile la uharaka wa kuyachimba walafi CCM na JK hawataki kusikia haya maana wanataka kuchota mapema na wakae pembeni .
 
  1. Kwa nini amri inapewa Serikali ya Mkoa na si idara husika ya Serikali ambayo ni Magereza? Tangu lini TAMISEMI imekua ikiongoza Magereza?
  2. Kama ni suala la kuwepo madini, je madini ambayo tunayachimba, yameliingizia Taifa letu mapato gani ya kimsingi ambayo yametuondolea Umasikini? Ikiwa mikataba ya uchimbaji Dhahabu na Tanzanite na madini mengine bado ina matatizo na mapendekezo ya Tume ya Bomani hayajafanyiwa kazi, kwa nini Songwe wahamishwe na kule Singida na Dodoma wananchi walazimishwe kukubali uchimbaji wa Dhahabu na Uranium?
  3. Je Serikali (Taifa) itamiliki kwa asilimia ngapi miradi mipya ya uchimbaji madini na hivyo kuondokana na kudhulumiwa na makampuni wekezaji?
  4. Je kuna ulazima gani au haraka gani ya kuchimba madini haya ambayo sisi kama Taifa hatuyatumii kiuzalishaji kupitia viwanda vyetu na kuishia kuyauza nje ya nchi?
  5. Kwa nini tusibuni mfumo mpya ambao hautaishia kwa Tanzania kuchimba madini pekee bali hata kuyatengeneza katika mfumo na bidhaa ambazo zitauzika nje, hivyo kuongeza ajira, kuongeza viwanda na kuongeza pato la Taifa kwa kuuza bidhaa kamili na si mali ghafi?
  6. Gharama za uhamishaji huu, zitachukuliwa na nani?

Ni athari za ukoloni mkuu, unajua India inasifika duniani kwa uuzaji wa vito vya Tanzanite na hawachimbi Tanzanite kule, sehemu nyingine utakuta matajiri wa Tanzanite dunia hii ni Toronto, inahuzunisha sana

Serikali ina uwezo kabisa wa ku-control haya madini, na hata kuwa wanunuzi wa haya madini na kutengeneza products.

Ten percent wapate wapi??

Nafikiri kuna haja ile sera ya majimbo ya CHADEMA kuwa applied , kama hawa jamaa watashika nchi.

Naamini mikoani kuna watu wenye akili zao ambao wanaweza ku-control madini kama wakipewa chance
 
hizo ni porojo tu !!! Aluminium ni madini yanayo chimbwa sehemu nyingi tu duniani !!! gabon ndo inayoongoza kwa uzalishaji... hapa tanzania yapo mbeya,na tanga lushoto....je kunafaida gani kuukalia uchumi wakati wananzengo wanatokomea kwa umasikini ?? do not be negative for verything guys!!!!

Tanzania will never develop under ccm

Mkuu Mzee wa Usafi,

Ni kweli si busara kukalia madini ambayo yangeweza kuchimbwa na kuisaidia nchi na wananchi wake kuondokana na umasikini. Lakini kwa bahati mbaya this is not the case. Madini yanawafaidisha hao wawekezaji wenyewe na Watanzania wachache wenye uchu wa kujilimbikizia mali. Na kutoka na uzoefu ambao tayari tumeupata kwenye maeneo mengine nchini kunakochimbwa madini, ndio maana watu wanahoji uchimbaji huu wa aluminium utaisaidia vipi nchi hii au ni yale yale ya kuja kutuacha na maandaki wakati wageni na mafisadi wakiendelea kuneemeka?

Kwa kuhoji haya, nafikiri tuko sahihi na wala sio kuwa negative!!!!

Tiba
 
Laini mimi kwa maoni yangu kuchimba siyo tatizo tatizo ni mikataba ambayo haizingatii maslahi ya wananchi/nchi. Namshauri JK kabla hawa watu hawajachimba basi wajenge sekondari za hadhi 5, shule za msingi za hadhi 10, wajenge hospitali kubwa 1 mjini mbeya na ndogo hapo hapo songwe, wahakikishe umeme wa gridi unaletwa eneo hilo na wajenge bara bara za lami maeneo yote ya mbeya.

Haya mambo lazima yawe kwenye mkataba

Ni kweli ulivyosema, kama tungekuwa tunanufaika na uchimbaji wa madini kusingekuwa na kelele nyingi, tatizo ni suala la nchi kuishia na mrahaba wa asilima 3 huku watu wachache na hao wawekezaji wakiendelea kutanua na kutuachia mashimo. Kama hakuna faida kwa nchi, hakuna haja ya kuendelea kufungua migodi mipya. Kwanza turekebishe mikataba ya uchimbaji madini - maslahi ya nchi yawekwe mbele.
 
LOL! umenisababishia kikohozi mkuu, mbavu sina! I got your message!

Kesho zamu ya hospitali ya Muhimbili, nchi tajiri hii

unajua hawa jamaa wanavyowalegezea wawekezaji wangekuwa na uwezo wangewahamisha watanzania wote ili wawekezaji wapewe raslimali zetu!
 
Mwanakijiji,
The next venue ni Serengeti. Kule kumejaa dhahabu na kila aina ya madini.
Bado wanatafutia mikakati ya kuwarubuni Watanzania ili waingize wawekezaji kule.
 
Back
Top Bottom