Ochu
JF-Expert Member
- May 13, 2008
- 975
- 47
Na Hawa Mathias, Mbeya
RAIS Jakaya Kikwete ameitaka serikali mkoani Mbeya kufanya uwezekano wa kuhamisha gereza la Songwe na kulibomoa ili kuanza uchimbaji wa madini ya alminium ambayo yamebainika kuwepo katika ardhi ya gereza hilo.
Kikwete alisema hayo juzi katika ikulu ndogo mkoani Mbeya mara baada ya kutoka katika ziara ya kutembelea kata ya Ilembo mkoani humu.
Alisema ni kitu kisichowezekana kama uchumi wa wananchi kushuka wakati kuna rasilimali nyingi za madini ambayo yanaweza kuinua uchumi wa wananchi wa mkoa huo, hivyo wafungwa waliopo wahamishwe katika magereza mengine na kutafuta eneo la kujenga gereza hilo.
''Ni muhimu viongozi wa serikali ya mkoa kuchukua jukumu la haraka kutekeleza hili na si kuacha rasilimali za kukuza uchumi zikakaa bila kuzalisha na kubaki kwenye ardhi,'' alisema Kikwete.
Aliongeza kuwa; ''Kwa sasa tunapaswa kufanya mikakati ya kubomoa gereza la Songwe na kujenga eneo lingine kisha kuanza uchimbaji rasmi kutokana na eneo hilo kuonekana kuwa na madini mengi ambayo yanaweza kuongeza pato la nchi na kukuza uchumi''.
Aidha alimwagiza Mkuu wa Mkoa , John Mwakipesile kuanzisha mradi wa matunda aina ya 'apple' yanayolimwa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na si kutegemea yanayozalishwa kutoka nje wakati nchi ina uwezo wake binafsi.
Wakati huo huo Rais Kikwete alisema serikali imesitisha ununuzi wa magari na badala yake fedha hizo zitatumika kununua vifaa vya kilimo ili kuboresha sekta hiyo.