Rais 2015

Tunko

Senior Member
Dec 24, 2013
181
225
Kwa mwelekeo uliopo 2015 Rais atakua PINDA mkubali mkatae ndio maana watu wenye fedha zao ndani ya CCM wanatumika kumchafua katika jamii ili aonekane hana uwezo wa kuongoza.NAWASILISHA
 

NJUGHU

JF-Expert Member
Aug 16, 2013
380
500
Kwa mtazamo wa sasa,ukihoji mbona hiki kibaya Tanzania,majibu utaambiwa CCM.Tukumbuke aslimia yetu wengi wote tulikuwa wanaCCM hivyo tunajilaumu wenyewe.
Vimekuja vyama vingi, tukaipa imani NCCR, imepotea maana haikuwa na wanachama bali washabiki.Kwa kosa hilo CHADEMA wakajifunza wakawa na wanachama uchaguzi uliopita.
CDM nao wanavurugana kwa uchu wa madaraka, ilikuwa imani yetu kiwe na nguvu kuinyoshea kidole chama tawala lakini lahasha.
Kuondoa hivi viburi vya vyama inabidi watanzania tusiwe wanachama ili vyama vijue Kuwa ridhaa ya kuongoza si ya kutabirika ili kutimiza malengo ya sera zao wakijua fika kura watapata kwa Yale waliyotufanyia.
Na hii itasaidia tuwe na serikali ya mseto ambayo kwa Nchi kama yetu ni suluhu la uwajibikaji.
Tusiishie Kuwa watumwa wa vyama bali wazalendo tuijenge nchi yetu, namalizia tusiwe wanachama na mashabiki wengi wetu ili taasisi hizi z-sijiamini na kupuuza tunachokitaka.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom