Raila Odinga amtaka Kikwete abadili katiba ya Tanzania haraka

Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,326
974
Source: The East African,
Date: November 29-December 5, 2010,
Page: 46
Headline: {A new constitution would do wonders, govt advised}

Kenya’s prime minister Raila Odinga was in Mwanza last week urging the Tanzanian government to fast track the new constitution writing process.

“This”, he argued, “would help the country achieve its growth priorities”.
He was speaking at the launch of new Kisumu-Mwanza flight by Jetlink Express
 

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,005
7,180
Odinga badala ya kuharakisha kuwafikisha walioshiriki mauaji ya Kenya mahamani, anajidai kujali zaidi growth ya Tanzania.
Siungi mkono hii tabia mpya ya viongozi wa kitaifa wa kenya kujifanya wadau wa uongozi wa Tanzania.
 

BABA JUNJO

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
241
14
Big up man. You must apriciate some other businesses and advice others for prosperity cause you dont knwo you 2morrow.
 

Omuregi Wasu

JF-Expert Member
May 21, 2009
749
142
Odinga badala ya kuharakisha kuwafikisha walioshiriki mauaji ya Kenya mahamani, anajidai kujali zaidi growth ya Tanzania.
Siungi mkono hii tabia mpya ya viongozi wa kitaifa wa kenya kujifanya wadau wa uongozi wa Tanzania.

Tatizo siyo kukataa tu kila kinachotoka kwenye vinywa vya viongozi wa Kitaifa wa Kenya ila nionavyo mie ni ujumbe ulioko kwenye hayo wanayoyasema. Naunga mkono kauli ya Ondiga kwa kuwa ninahitaji hiyo katiba. Ebu jaribu kufikiria hivi, Odinga amesema hayo kwa sababu tuna viongozi wajinga wasioelewa mahitaji ya Watanzania na njia sahihi za kuleta ustawi wa jamii ya watanzania.... Serikali imeshatoa tamko kupitia kwa waziri Kombani.... Odinga anajaribu kushauri au kusema kwa niaba ya watanzania akiwa kama mtu aliyelelewa Tanzania kwenye Ikulu ya Tanzania.
 

boma2000

JF-Expert Member
Oct 18, 2009
3,285
307
yeye si m-tz wala hana mamlaka juu wa tz. tutayamaliza wa-tz peke yetu muda ukifika ambao nasema itakuwa ni 'point of no return' either serikali itake au iwe haitaki katiba itapatikana tu muda huo
 

Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
19,612
4,182
Raila Amolo Odinga ni Waziri mkuu mwenye mamlaka nchini Kenya.
then Kenya ni nchi jirani mwa Tanzania na kwa hakika Kenya ni watu wa karibu sana na Tanzania, nahisi hili liko wazi pia.

So Kiongozi yule wa Kenya anapotoa ushauri kwa mwenzie wa hapa ni jambo la kawaida sana.
Kama kuna mwenye kumbukumbu nzuri atakumbuka mwaka 2007 wakenya walifanya uchaguzi na kisha kuna tofauti zikajitokeza.
Mkapa alikwenda kule na kujaribu kuwapatanisha, pia hata Kikwete alikwenda pale, na wakenya walionyesha nidhamu kwa viongozi hawa.

Sasa nashangaa kwa baadhi ya wakurupukaji hapa JF wameanza kuandika uharo wao ili mradi tu nao waonekane walichangia mada...


Panapofika kwenye maswala muhimu basi act like ur not stupid...
 

August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
7,530
3,079
Hivi hawa manyang'au bado hamjajua wanachokihitaji?
hapa ameongelea umuhimu wa kubadilisha katiba na sio kwamba ccm wachaguliwe au chadema au cuf, ila uzuri wake utaweza kuzuia au kupunguza tatizo la vita vya wenyewe kwa wenyewe, kama wao kenya walivyo-experience au sasa hivi ivory coast wanavyo chakachuliwa na Gagbo
 

nsimba

JF-Expert Member
Oct 7, 2010
782
55
let the fact be the fact!! uhuru wa kushauri. Hoja ya Odinga ni sahihi. Tuendako tutakuwa na machafuko kama katiba haijawajengea imani watz wote.Hilo ndo funzo la Kenya, na Odinga ambaye anaitakia mema tz hataki tufike huko
 

Thesi

JF-Expert Member
Aug 8, 2010
998
281
Kama kuna mwafrika atakumbukwa na historia kuanza vuguvugu la ukombozi awamu ya pili Afrika kutoka vyama kandamizi za Kiafrika ni Raila Amolo Odinga a.k.a Agwambo. Huyu ni jebali lililotumia mbinu zote za kisiasa kumng'oa madarakani kiongozi aliyeogopwa sana Kenya Daniel Arap Moi na chama chake cha KANU na wakenya wakamsaidia kuwatupa kwenye kaburi la SAHAU.

Odinga anaongea manake anajua athari za kung'ang'ania katiba zilizopitwa na wakati. Ameanza kupambana Moi kuwapa wakenya katiba mpya wakamwingiza Kibaki madarakani. Kibaki alivoona madaraka matamu kataka kung'ang'ania hiyo katiba ya zamani kwa kubadilisha vitu vichache. Odinga ailifanya kampeni ya kuipinga akitaka katiba ya kisasa kuleta maendeleo kwa wakenya wote na wakenya wakaipiga chini Kibaki aliahibishwa na kuamua kumfukuza kwenye serikali ya Rainbow coliation.
Hakuchoka ameendelea na mapambano ya katiba mpaka imepatikana iliyo nzuri ingawa siyo katika kiwango alichokitaka lakini wakenya sasa wanatembea kifua mbele barani Afrika kama watu wanaoweza kuona mwangi wa neema na maendeleo kwa vizazi vijavyo.

Anajua kitua anachokiongea manake mpaka sasa licha ya Kenya kutawaliwa na siasa za kikabila uongozi umeanza kuheshimu watu na mafisadi sasa matumbo joto. Kufuatia kuteuliwa kwa mwanaharakati Prof Patric O. Lumumba kuwa mkurugenzi wa tume ya kupambana na ufisadi kama TAKUKURU hakuna tena maficho tena kwa mafisadi.
Hapa Tanzania viongozi kama hawa tunao wachache sana ingawa bado hawana rekodi ya Raila. Dr. Slaa ni aina ya viongozi kama Raila wanaochukia maovu ambao tukiwatumia vizuri tunaweza kufika mbali.

Mnaokosoa Odinga kumtaka Kikwete abadilishe katiba mnakosea manake hamjui alivompambanaji wa haki na utawala bora. Dr Slaa na wanaharakati wengine wameamsha vita nya katiba mpya, Odinga kasema na Obama nae mwisho mtamsikia anasema. Nnacho maanisha ni kuwa hakutakuwa na sehemu ya kukimbilia kukwepa dai la katiba mpya muda sio mrefu.

Katiba tunahitaji na ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi ila vyama vya wizi kama CCM hawaitaki manake itawafungua watu macho kukataa upuuzi wao.
 

Old ManIF

Senior Member
Dec 1, 2010
104
2
Odinga badala ya kuharakisha kuwafikisha walioshiriki mauaji ya Kenya mahamani, anajidai kujali zaidi growth ya Tanzania.
Siungi mkono hii tabia mpya ya viongozi wa kitaifa wa kenya kujifanya wadau wa uongozi wa Tanzania.


Hivi hapa kunatatizo gani? kiongozi wa nchi jirani kutoa ushauri wake kwetu. Tukizingatia kuwa yeye alisaidiwa na Mwl Jk, na kwenye mgogoro wao viongozi wetu waliwasaidia. Na jaribu kufikr, angetumia staili ya mwl Jk ya kuzisaidia Nchi za kiafrika zenye migogoro mngesema je? Ninavyoona mimi TZ tunamgogoro wa kikatiba na hapa kasema tu, na ni product ya Mwl, hapo vipi?
 

We can

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
678
46
Kila mtu, Tanzania, Afrika au kokote duniani ana haki ya kutushauri. Mbona sisi tuliwashauri wengi. Afrika kusini ni sehemu ya juhudi zetu. Msumbiji, Angola, Zimbabwe, nk ni sehemu ya juhudi zetu. Sehemu zingine tumelazimika kupeleka hata jeshi kushinikiza haki ya walio wengi: Uganda na Anjuani. Odinga is right.
 

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,882
Mimi nadhani kama PM , kama jirani nk alitoa ushaurii ambao una manufaa this has nothing to do with Kenyans kuwa wajanja nk .He knows what it takes to get it right sasa ushauri kama mzuri uchukuliwe tuache kubeza kila kitu toka kwa wakenya jamani .
 

Mwikimbi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,762
804
tumekusikia siye wenye masikio, lakini viongozi wenzako hapa TZ wameziba masikio yao kwa pamba, tusaidie kuzibua pamba hizi toka kwenye masikio yao, labda kwa maandamano kama kenya, Mungu akubariki ewe Raila amolo Odinga uzidi kusaidia kizazi hiki
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom