Raila Odinga, aliyekataa kupokea simu si rafiki yako Magufuli bali ni Rais Magufuli

RAILA KAMSHAURI MAGUFULI YUPI?

Raila Odinga anadai amempigia Rais wetu Simu kumshauri kuhusu Corona. Anavyodai sijui hajampata kwenye Simu.....

Kitu ambacho Raila anatakiwa kukifahamu ni kwamba Kuna Magufuli wawili, Mmoja ni Rafiki yake ambaye wanaweza kujadiliana naye chochote kwa wakati wowote, Magufuli wa Pili ni Rais wa Tanzania, huyu si mtu bali ni taasisi yenye kila aina ya wataalamu na washauri.

Issue ya Corona si issue anayeishughulikia Magufuli ambaye ni Rafiki yake Raila Bali ni Magufuli ambaye ni Taasisi. Raila anatakiwa atofautishe haya mawili kwanza, aliyepaswa kumpigia Simu Magufuli ambaye ni Taasisi ni Uhuru Kenyata Hawa wapo level Moja.

Kitendo Cha Raila kuvuka mipaka na kuja kushauri Tanzania ni kutuaona kuwa sisi vyombo vyetu haviwezi kutusimamia Wala hatuwezi kujisimamia.

Tanzania imekuwa nchi yenye misimamo yake toka Zamani, tumejirisk kwa mengi hata la kutafutia wengine Uhuru tulijirisk sanaa... Tanzania yenyewe imesema mabeberu yasitukopeshe badala yake watusamehe madeni, Kenya wao wameshaenda kukopa. Hii ni misimamo miwili tofauti....

Tusimame pamoja, Hakuna mtu njee ya Tanzania anayeweza kuipenda Tanzania kuliko sisi wenyewe. Pamoja na Mambo Mengine watanzania tujiamini, sisi sio Goi Goi wa kiwango hicho.

Ukishakuwa Rais hata marafiki zako uliokuwa nao mwanzo huwezi kuongea nao hovyo hovyo, kila kitu kinafanyiwa monitoring, hata hiyo simu aliyopiga Raila inawezekana sio hiyo aliyonayo Sasa. Tumerahisisha mno taasisi ya Urais .... Si rahisi Kama tunavyofikiria.
Mkaidi hafaidi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom