Raila Odinga, aliyekataa kupokea simu si rafiki yako Magufuli bali ni Rais Magufuli

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
1,379
3,882
RAILA KAMSHAURI MAGUFULI YUPI?

Raila Odinga anadai amempigia Rais wetu Simu kumshauri kuhusu Corona. Anavyodai sijui hajampata kwenye Simu.....

Kitu ambacho Raila anatakiwa kukifahamu ni kwamba Kuna Magufuli wawili, Mmoja ni Rafiki yake ambaye wanaweza kujadiliana naye chochote kwa wakati wowote, Magufuli wa Pili ni Rais wa Tanzania, huyu si mtu bali ni taasisi yenye kila aina ya wataalamu na washauri.

Issue ya Corona si issue anayeishughulikia Magufuli ambaye ni Rafiki yake Raila Bali ni Magufuli ambaye ni Taasisi. Raila anatakiwa atofautishe haya mawili kwanza, aliyepaswa kumpigia Simu Magufuli ambaye ni Taasisi ni Uhuru Kenyata Hawa wapo level Moja.

Kitendo Cha Raila kuvuka mipaka na kuja kushauri Tanzania ni kutuaona kuwa sisi vyombo vyetu haviwezi kutusimamia Wala hatuwezi kujisimamia.

Tanzania imekuwa nchi yenye misimamo yake toka Zamani, tumejirisk kwa mengi hata la kutafutia wengine Uhuru tulijirisk sanaa... Tanzania yenyewe imesema mabeberu yasitukopeshe badala yake watusamehe madeni, Kenya wao wameshaenda kukopa. Hii ni misimamo miwili tofauti....

Tusimame pamoja, Hakuna mtu njee ya Tanzania anayeweza kuipenda Tanzania kuliko sisi wenyewe. Pamoja na Mambo Mengine watanzania tujiamini, sisi sio Goi Goi wa kiwango hicho.

Ukishakuwa Rais hata marafiki zako uliokuwa nao mwanzo huwezi kuongea nao hovyo hovyo, kila kitu kinafanyiwa monitoring, hata hiyo simu aliyopiga Raila inawezekana sio hiyo aliyonayo Sasa. Tumerahisisha mno taasisi ya Urais .... Si rahisi Kama tunavyofikiria.
 
FB_IMG_15895710112556693.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kauli moja hayati mwalimu J.K.N alishawai isema kwenye hotuba zake watu sio wa kuwasikiliza sana baadhi ya maneno yake yalikua haya" mpige mawe huyo , mpige mawe huyo ,muuweni huyo ila wewe usiwasikilize endelea na safari yako n.k" mi naona rais wetu ni mtu makini sana na anajua nini anafanya tumpe muda tu.
 
Huyo ondinga nayeye si_mstahafu. ..itakuwa anawashwa washwa tu. sio bure ..yeye mambo ya tz yana muhusu nini. ..

mpaka dakika hii wote kwa pamoja tunashuhudia kuwa maamuzi ya magufuli kutoiweka nchi katika kizuizi yapo sahihi kabisa kwa wenye akili wameliona hilo...

ndio maana hata huko USA na baadhi ya nchi za ulaya wameshaanza kufikirikia kiachana na lockdown.... hizi nchi za Africa zimekuwa ni bendera fuata upepo wanafuata kila wanacho ambiwa na mabwana pasipo kujali kwamba hayo wanayo yafanya yatakuwa na maslahi kwa wananchi wao ama la. ..... hizo nchi binafsi nazifananisha na mwanamke malaya zingekuwa nchi zao ni jinsia KE Sasa hivi zingeshakuwa na mimba..... period
 
RAILA KAMSHAURI MAGUFULI YUPI?

Raila Odinga anadai amempigia Rais wetu Simu kumshauri kuhusu Corona. Anavyodai sijui hajampata kwenye Simu.....

Kitu ambacho Raila anatakiwa kukifahamu ni kwamba Kuna Magufuli wawili, Mmoja ni Rafiki yake ambaye wanaweza kujadiliana naye chochote kwa wakati wowote, Magufuli wa Pili ni Rais wa Tanzania, huyu si mtu bali ni taasisi yenye kila aina ya wataalamu na washauri.

Issue ya Corona si issue anayeishughulikia Magufuli ambaye ni Rafiki yake Raila Bali ni Magufuli ambaye ni Taasisi. Raila anatakiwa atofautishe haya mawili kwanza, aliyepaswa kumpigia Simu Magufuli ambaye ni Taasisi ni Uhuru Kenyata Hawa wapo level Moja.

Kitendo Cha Raila kuvuka mipaka na kuja kushauri Tanzania ni kutuaona kuwa sisi vyombo vyetu haviwezi kutusimamia Wala hatuwezi kujisimamia.

Tanzania imekuwa nchi yenye misimamo yake toka Zamani, tumejirisk kwa mengi hata la kutafutia wengine Uhuru tulijirisk sanaa... Tanzania yenyewe imesema mabeberu yasitukopeshe badala yake watusamehe madeni, Kenya wao wameshaenda kukopa.... Hii ni misimamo miwili tofauti....

Tusimame pamoja.... Hakuna mtu njee ya Tanzania anayeweza kuipenda Tanzania kuliko sisi wenyewe. Pamoja na Mambo Mengine watanzania tujiamini, sisi sio Goi Goi wa kiwango hicho.

Ukishakuwa Rais hata marafiki zako uliokuwa nao mwanzo huwezi kuongea nao hovyo hovyo, kila kitu kinafanyiwa monitoring, hata hiyo simu aliyopiga Raila inawezekana sio hiyo aliyonayo Sasa. Tumerahisisha mno taasisi ya Urais .... Si rahisi Kama tunavyofikiria.
Magu hajui kabisa diplomacy tuwe makini na naye ni hatari kwa ustawi wa nchi yetu.
 
Similar Discussions

29 Reactions
Reply
Back
Top Bottom