Raila Odinga adai alikuwa ni Mshauri wa Rais Magufuli na alimshauri hata namna ya kupata fedha kwa ajili ya nchi. Ngoja tuone 2025 hapa nyumbani!

Acha kuongopea watu Raila anaungwa mkono na WAJALUO TUU WAKIKUYU WAKALENJINI HAWATAKI HATA KUMSIKIA tunazifuatilia siasa za Kenya mambo ni UDA NA HUSTLER
 
Alipendwa sana na walio wanyonge ambao ni wengi. Ila ukitaka kujua ubaya wa wanyonge wape nchi au nchi iendeshwe kwa matakwa yao. Baada ya miaka 10 inageuka jangwa, nchi ya umasikini wa kutupwa halafu wanyonge waliokuwa wanakushangilia wanakulaani.

Huamini? Wape wanyonge waitunze ngorongoro na serengeti halafu subiri baada ya miaka kadhaa kama utawaona wanyama na watalii.

Wape maeneo ya makazi yaliyopangwa vizuri yenye miti halafu subiri baada ya muda.

Wafanye matajiri wawe mashetani halafu wakishakuwa mashetani wape kazi wnyonge wajichange kodi ipatikane.

Mifano ni mingi kama huamini.

MWANASIASA ANATAFUTA KURA ZA WANYONGE, UKIPENDWA NA WANYONGE UNA TIKETI YA UONGOZI ILA SASA......
Kwa hiyo point yako ni nini haswa, kwamba wanyonge wasipate mtetezi, wawe ni watu wa kuteseka tu Kama wamachinga na mama lishe ktk awamu hii?!

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
 
Inamaana ndiye aliyeshauri ujenzi wa Chato International Airport na Rusumo Wild Life pia uhamisho bila visa wa wanyama kutoka Serengeti na Ngorongoro!
Kwani alijenga Airport au kuanzisha hizo mbuga kwa ajili ya familia yake?!
Hiyo Chato Airport hata Chadema wanaitumia so I don't see the problem.

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
 
Mgombea urais wa Kenya anayeungwa mkono na wananchi wengi nchini humo mh Raila Odinga amesema yeye alikuwa ni Mshauri wa aliyekuwa Rais wa Tanzania hayati Magufuli.

Raila amesema Magufuli aliweza kumpigia simu hata saa 12 asubuhi ili apate ushauri wake na kwamba alimshauri hata namna ya kupata fedha kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Source: Kenyans. co.ke

My take; Hata hapa nyumbani 2025 Magufuli atakuwa lulu.
Sio anadai ndio ukweli

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Mgombea urais wa Kenya anayeungwa mkono na wananchi wengi nchini humo mh Raila Odinga amesema yeye alikuwa ni Mshauri wa aliyekuwa Rais wa Tanzania hayati Magufuli.

Raila amesema Magufuli aliweza kumpigia simu hata saa 12 asubuhi ili apate ushauri wake na kwamba alimshauri hata namna ya kupata fedha kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Source: Kenyans. co.ke

My take; Hata hapa nyumbani 2025 Magufuli atakuwa lulu.
Raila akiendelea kujinasibisha na magufuli ataukosa uraisi, wakenya wengi wanamwona magufuli ni hayawanni
 
Nimeona hii habari mahala Odinga anajinasibu kuwa mastermind wa Magufuli, labda ndio kwasababu ya ule ukaribu wao.

Huo ushauri wa kupata pesa kwa ajili ya maendeleo ya nchi ni upi? kama ni kukopa bora asingemshauri, au kupora matajiri pesa zao? napo bora asingemshauri.

Naona Raila anamtumia Magufuli kama kete yake ya kugombea urais, najua wakenya walikuwa wanamkubali Magufuli kwasababu ya uzalendo wake na kuwachukia wezi.

Ila sijajua walikuwa wanamfuatilia kwa kiasi gani zaidi ya kumsoma/kumsikia juu juu kwenye vyombo vya habari.
sasa alizikopa wapi wakati mnasema hakua na mahusiano mazuri na wakopeshaji.
 
Kwahyo hata mambo ya kumpiga Tundu Lissu risasi, na kupotea kwa akina ben Saanane na yale ya kupotea kwa 1.5tr yooote kamfundisha yeye baasi wakenya wana bahati ya kuwa na mtu kama yeye
Darasa la Saba kwenye ubora wako. Umekaririshwa mwenyewe, sasa hivi unaropoka tu.
 
Uishi nao kwa akili vipi?! yaani ukubali kuona wananyanyasika na kunyonywa huku ukiwapa matumaini hewa?

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
Unakazana sana na mnyonge kunyanyasika, tafsiri ya kunyanyasika kwa mnyonge isiyomhusu tajiri kama raia ni ipi? Matumaini hewa kwa mnyonge yasiyomgusa tajiri ni yapi?

Serikali inatakiwa ipambane bei za bidhaa ziwe za manufaa kwa nchi, mafuta yawe bei nzuri, maji na umeme viwepo pia miundombinu ikae sawa halafu iwaache raia watafute fedha kihalali na kisha wakusanye kodi kwa haki ili Kila mmoja afurahie jasho lake.

Mnyonge na tajiri wote ni raia na wanaumia au kunyanyasika endapo bei ya mafuta itakuwa juu, miundombinu mibovu n.k ila mnyonge anaumia zaidi sababu HANA PESA.

Kuruhusu machinga wakae kiholela mpaka mbele ya mwenye duka kwa sababu ni wengi na hawana pesa ni kumnyanyasa mwenye duka.

kubambikiza kodi kwa mfanyabiashara mkubwa nje ya kodi halali sababu tu pesa anazo kuliko mnyonge ni kumnyanyasa mfanyabiashara.

Sikia, hakuna mwenye haki zaidi ya mwingine kwenye hii nchi. Tufuate taratibu, haki na sheria tulizojiwekea na si nje ya hapo. Mwenye fedha halali aifurahie pesa yake na mnyonge apambane na hali yake sio kunyanyasa wenye fedha sababu wanyonge ni wengi ni upuuzi.
 
Huyo Raila sijawahi mkubali Toka nilipojuwa ni rafiki wa jiwe nilimwona kama juha kalulu
 
Raila Polepole Ndungai ni watu waliojitolea kujizika wazimawazima na MAREHEMU JIWE
 
Back
Top Bottom