Raila kuja Tanzania Jumamosi kuishawishi Serikali juu ya COVID-19

nditolo

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
3,609
4,097
Tanzania tulikuwa wapatanishi na waheshimiwa sana Ulimwenguni. Tulijijengea sifa kubwa sana, yale yote yaliyofanyika na watangulizi leo yamekuwa matope

Imagine Raila kuja Tanzania kumshawishi Rais afuate taratibu za kitaalamu ili kutokomeza ugonjwa. Tumekuwa hatuaminiki kabisa.

Awamu iliyopita ilijenga diplomasia kiasi kwamba kila Nchi kubwa America, China, India zilikuwa zinapishana angani kuja Tanzania kutangaza misimamo na sera zao leo

Uingereza imeondoa raia wake, ili kuwakoa wasije kufia ugenini ikawa aibu kwa Taifa kubwa kama British.

Nashauri tu wataalamu waachiwe na Ndugulile arudishwe ili tutengeneze takwimu vizuri maana huyo mwingine hatumjui halafu hatuna historia yake kikazi. Hapa muhimbili hajui hata malango wa kukingilia.

Tanzania tuko chini kiasi hiki?

Yaani ili kutuonyesha kuwa upinzani sio Ugomvi au vita au Fitina Raila katumwa na Raisi wa Kenya aje apatanishe atuweke sawa.


Hongera sana wa Kenya kwa kutujali.
 
Muda wa kulazimishwa umefika. Hata wao huko Ulaya na Amerika wameichoka serikali ya sisiemu. Wanawajua kuwa hawaambiliki.
 
Hivi aliyewaambia lockdown ndio njia pekee ni nani myie ufipa?
Hapa umezunguka ila point yako ni hiyo...
Wapi mleta mada kataja lockdown? Kenya wenyewe hawana lockdown! Mimi pia siyo muumini wa lockdown ila kuna vitu kama tungevizuia mapema basi leo tusingekuwa tunakuja na sanaa za kila namna kujitetea!
 
Wajinga bado wapo sana nchini!!!
Tutaelewana tu, hiyo jumamosi utajua tu kuwa nani mjinga na yupi mwerevu. Na mkija kwenye anga zetu na jezi zenu mtajua tu kuwa hatuwapendi. Na ndipo mtakumbuka kwanini Lissu alisindikizwa faster kuhamishiwa Nairobi.
 
Sijui kwa nini watu wanadhani lockdown ndiyo best option ya kupambana na hivi virusi.

Option zote mbili ni nzuri na kila moja ina faida na hasara zake. Halafu kama Taifa tuko huru kuamua ni njia gani tuifuate, na kila option haiwezi kumfurahisha kila mtu. hata huko wanakofanya lockdown, kuna watu wanaandamana kupinga.

Tatizo siasa nyingi sana from both sides. JPM kaamua ndiyo kaamua, hata huyo Raila kama lengo ni Lockdown atakula za Uso.
 
Back
Top Bottom