Raia zaidi ya 13,000 wameyahama makazi Sudan Kusini

Display Name

JF-Expert Member
Feb 11, 2014
410
500
Raia zaidi ya 13,000 wayahama makazi yao nchini Sudan
Raia zaidi ya 13,000 wameyahama makazi yao kutokana na mapigano ya hivi karibuni Sudan Kusini.

Ripoti hiyo imetolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa na wakimbizi (UNHCR).

Msemaji wa UNHCR Babur Baloch, katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva amesema kuwa zaidi ta raia elfu tano wa Sudan Kusini wamehamia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huku wengine zaidi ya elfu nane wakiwa wanahama kutoka eneo moja kwenda jingine bila ya kutoka nje ya nchi.

Wengi wanaoyahama makazi yao wameripotiwa kuwa ni watoto,wanawake na wazee.

Idadi kubwa ya watu wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na mapigano yanayoendelea Sudan ya Kusini.

TRT

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom