Raia wanavyowapa wanasiasa mtihani mgumu bila kujua

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,428
Wakati fulani wanasiasa hulazimika kufanya mambo tete, ila mara nyingi hata wao wenyewe wanakuwa hawayapendi, hayawafurahishi na yanawakosesha usingizi ila inawapasa kufanya na kuigiza kama wanafurahia kwa sababu ya 'Customer needs'.

Mwanasiasa ni sawa na mtoa huduma mwingine yoyote tu, huwezi kutoa huduma kama haina wahitaji, hata iwe nzuri kiasi gani utakwama na mwishowe utajikuta ukilazimika kuacha kutoa huduma unayotoa au kutafuta huduma ambayo mteja wako anataka ndio ummpe (hata kama ni mbaya).

Kama mteja wako anasuuzika roho yake akiona unamdhalilisha mtu mwingine kwa mfano, kama unataka kumfurahisha mteja, inabidi utafute mtu umdhalilishe na mteja ajue umefanya hivyo. Usipofanya hivyo utapotea kwenye ‘game’

Kama mteja anataka kusikia majungu , na wewe unataka kumshika, mpe majungu, vinginevyo tafuta kazi nyingine yakufanya.

Kama mteja anataka kudanganywa, mdanganye, vinginevyo hatakukubali, na kama lengo lako ni kukubalika utakuwa umekwama. N.k

Mtiririko huu unaendelea hivyo kwenye kila jambo na mwishowe kusababisha mzunguko wa tatizo “Problem cycle” Mwananchi anasema yupo alivyo kwa sababu wanasiasa si watu wazuri, mwanasiasa anasema anafanya afanyavyo kwa sababu ya wananchi.

Wakuu,Watanzania wengi tuna mitizamo hasi karibu kwenye kila kitu na hapo ndio msingi wa shida nyingine zote unapoanzia. Matatizo mengi katika nchi yanasababishwa na raia na sio viongozi wa kisiasa. Kiongozi ni sawa na dereva ambaye kakodishwa anaenda wanakoenda abiria (haijalishi sana kama anapenda kwenda huko au laa).

Mara nyingi wanasiasa husoma upepo wa raia wanavyofikiri na kuenda nao. Kwa hiyo kitu pekee kinachoweza kuleta uhakika wa kesho iliyo bora, ni raia kubadili mitizamo na tabia kwenye mambo ya msingi vinginevyo, hakuna namna ya kukomesha mzunguko unaotajwa hapo juu.
 
Ukweli huu unaweza usiwapendeze wengi lakini moja ya njia zinazoweza kutusaidia ni kuambiana ukweli
 
Nafikiri ipo haja ya raia kuhamasishana wenyewe kwa wenyewe na kupeana elimu kujiepusha kuwaweka viongozi wao kwenye hii 'ethical & practical dilemma' kwa sababu mwisho wa siku inaumiza wote wote na wote wanaishia kuishi Maisha yasiyo na furaha.

Tujisahihishe.
 
kwa mfano kuna jambo ambalo una uhakika kwamba lina madhara mabaya sana mbeleni, lakini unajua ukiwaambia watu(wateja wako) hawatakuunga mkono, na wewe unachotaka ni uungwaji mkono, unawaambia wasikuunge mkono (ufeli) au unawaambia 'hakuna shida!' hata kama unajua mbeleni itawagharimu vibaya mno (Halafu wakuunge mkono na hivyo uwe umefikia lengo)?

Na kinyume chake ni sahihi pia.

Katika mazingira kama hayo, wakulaumiwa ni nani?
 
Back
Top Bottom