Raia wanaposhinikizwa kupisha maendeleo.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Raia wanaposhinikizwa kupisha maendeleo....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jun 26, 2012.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Hii ni nchi ya ajabu sana ambayo kila kukicha inakuja na mikakati ya kufukarisha raia wake kwa visingizio vya wapishe maendeleo kama vile raia siyo sehemu ya hayo maendeleo............................. Matokeo yake raia husukumwa nje ya maendeleo kwa maana ya huduma muhimu na kupunjwa fidia ya thamani khalisi ya mtaji aliouwekeza kwenye shughuli zake kama vile nyumba, shamba na maendeleo mengineyo........................ La ajabu kabisa huyo mwekezaji anayepishwa huwa halazimishwi na sera/sheria kuwafidia waathirika wake kwa hasara ya kunyimwa kivuno cha matarajio yajayo ya waathirika......athariza kimazingira, uchumi, afya n.k hujitokeza....zikiwemo hasara ya kukosa huduma muhimu ambazo sasa yabidi wazifuate mbali na gharama nyinginezo ambazo sasa zinakuwa zimebinafsishwa kwa huyu mwekezaji....................na kuwa faida ambayo mwekezaji hata anakuwa hajaipanda..... kwa hiyo huvuna asichopanda wala kustahili.....na mwaathirika huwa amesahaulika kabisa!!!!!!!!!!!!!!!! Ushauri Tunahitaji sera ambazo zitamtambua raia mwathirika kama sehemu ya huo uwekezaji mpya ili aendelee kuvuna na kumpunguzia makali ya kupisha maendeleo......kumtambua apewe hisa naye awe sehemu ya umiliki wa huo uwekezaji na kwahiyo hajapisha maendeleo bali naye amekuwa sehemu ya maendeleo kama kweli yapo! Tusipofanya hivyo kwa kuwapa hisa watu wetu kwenye mitaji ya maendeleo tajwa...ina maana baada ya miaka kama 20 hivi ijayo sehemu kubwa ya raia wetu watakuwa wakimbizi wa kiuchumi ndani ya nchi yao................ Kwa minajili ipi tuaafiki na khali hiyo?
   
 2. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hoja yako.
   
 3. Rogie

  Rogie JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 6,310
  Likes Received: 3,058
  Trophy Points: 280
  Umeongea jambo la msingi sana..serikali kwakweli nahisi haiwatendei haki raia wake..kuna tukio moja la kuhamisha wananchi lilifanywa Dodoma hivi karibuni..dah inasikitisha sana..mama analia anasema "mimi sijalipwa chochote lakini hawa mabwana wamevunja nyumba yangu" na ukiangalia ni nyuma ambayo inaonekana amejibana sana mpaka kuipata..
  Mimi siku zote naamini kuwa kiongozi ni lazima uwe na utu na uadilifu sn..M.Mungu hakuwapa madaraka ili wajinufaishe wao na familia zao..kila chozi linalodondoka litalipwa mbele za Mungu..vilio la watz haviwezi kupita hivi hivi tu..
  Sera wanazoziweka ni kuwanufaisha jamaa zao..kila kitu ni tatizo TANZANIA hii..
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Rogi ni kuwa ubinafsi umezidi.........................angalia machimbo ya madini raia anagundua mgodi khalafu serikali inakuja na kudai ni nyara ya taifa ambayo kutapeli huo wanamnyang'anya na baadaye kumilikisha mgeni ambaye tena wanampa mkataba asilipe hata kodi..............na kumwongezea mvumbuzi umasikini na taifa kwa ujumla kwa sababu mwekezaji huyo kwa kupewa ruzuku ya kodi huliachia taifa mashimo na hutumia miundo mbinu zetu bila ya kutulipa fidia....................achilia mbali tija kubwa anayoipata kwenye mgodi.................nchi hii ya kwetu kamwe haiendi popote pale..........
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Ndallo .......dhuluma inatisha na sioni wa kututetea..........kila mmoja naona anahangaika na mkate wake usiku kukicha................
   
 6. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #6
  Jun 26, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Sheria ya Ardhi namba 4 ya 1999. 2)
  Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya 1999.3)
  Sheria ya Mahakama za Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi namba 2 ya 2002.4) Marekebisho ya sheria ya Ardhi namba 2 ya 2004.5) Marekebisho ya sheria namba 11 ya 2005 sehemu ya nne.
  Sheria ya Ardhi namba 4 na Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 zilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1999 na kuanza kutumika rasmi mwezi Mei mwaka 2001.
  Sheria ya Mahakama za utatuzi wa migogoro ya ardhi ilipitishwa mwaka 2002 na kuanza kutumika rasmi mwezi Oktoba 2003.
  Misingi Mikuu ya Sheria Hizi ni:• Ardhi ni mali ya umma na imekabidhiwa kwa Rais kwa niaba ya Watanzania wote.


  Naona utata hapo............
   
 7. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #7
  Jun 26, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Ni ukweli mchungu...
   
 8. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Rutashubanyuma kwa watawala wanaona wananchi sio haki yao kuwa sehem ya maendeleo
  Wala hawana haki na kile wanachodai kumiliki
  Maana ardhi wananyang'anywa kupisha wawekezaji wenye mitaji
  Wakigundua madini wanaambiwa si haki yao kuyachimba wanakabidhiwa wageni kuendelea kuyafaidi na wale wananchi wanaozunguka maeneo yale wanaachwa bila kitu zaidi ya kujengewa tudarasa tuwili na kadispensary wanaambiwa hayo ndio maendeleo yao
  Wamezungukwa na migodi na mbuga za wanyama zinazozalisha mabilioni ya pesa ila wanaishi kwenye nyumba za tembe maana kinachozalishwa pale kinawafaidisha watawala na wageni wao na familia zao
  Wao wanaishia kunyueshwa maji machafu ya sumu na kuua hata tule tumifugo walikoachiwa
  nafikiri kwa maneno hay mwananchi si sehemu ya maendeleo maana yanamwacha mbali sana na yeye hakuna anacchoona cha maendeleo zaidi ya kuteseka
   
 9. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #9
  Jun 26, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mimi nilikuwa kwenye machimbo ya madini misigiri singida mwaka 1997 na jamaa wengi tu niliwakuta wakichimba pale ila juzi nilisikia wakitimuliwa kumpisha mmiliki mwenye leseni.hapo ndo naposhangaa alipewa leseni lini na yeye ni nani?
   
 10. m

  mamajack JF-Expert Member

  #10
  Jun 26, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  wanafanya yote hayo kuhakikisha watanzania tunaendelea kuwa na matabaka,maana watanzania wengi ni wale wa hali ya chini,umaskunu wetu huu siku ukipungua au kuisha,tutweza kuhoji mambo muhimu yanawape nafasi ya kujilimbikizia mali.hilo ndo lengo kubwa.hebu fikiria,watu wamejenga,watoto wanasoma huduma za afya na nyingine wanaweza kuzipata japo si kwa ubora.then wanahamishwa wanapelekwa mbali ambao mtoto ili afike shule,lazima apande magari matatu au manne,wazazi hawaezi kufanya biashara yoyote ili waweze kupata iyo pesa ya kumpa mtoto,lazima ataacha shile na idada ya wajinga itaongezeka.viongozi wetu ni wabinafsi sana.hata ule utu tulopewa na Mungu kwao haupo kabisa.
   
 11. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Hoja zako zimeshikamana vizuri kweli kweli.
  Kama viongozi wanaochaguliwa direct na wananchi ndio wangekuwa wanasimamia maamuzi ya namna hii sidhani kama haya yangekuwa yanatokea, viongozi wanaofanya maamuzi ya kizembe namna hii ni administrative ambao ni wateule wa ama viongozi tuliowachagua sisi wenyewe au wateule wa wateule wa wateule wa wateule wa viongozi tuowachagua wenyewe kwenye mabox ya kura.

  napendekeza kwamba, kwenye mchakato wa uaandaji wa katiba mpya tuhakikishe kwamba ama viongozi wanaoteuliwa na viongozi waliochaguliwa kwa sanduku la kura wasiwe na mamlaka ya kuteua viongozi, na pia tuongeze idadi ya viongozi wa kuchaguliwa kwa sanduku la kura au tuamue maamzi fulani fulani yafanyike baada ya kupigiwa kura badala ya kupigia kura viongozi pekee.
   
 12. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #12
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,981
  Likes Received: 6,632
  Trophy Points: 280
  Umbumbu na upole wa watanzania umekuwa mtaji kwa walafi na mafisadi wa nchi hii kwa manufaa yao na familia zao. Mia
   
 13. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #13
  Jun 26, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  MamaJack, Unafikiri wanafanya makusudi, wengi hawajui madhara ya maamzi yao hasa pale wanapokuwa wamepewa mlungura au wanategemea mlungura, viongozi na watawala wetu wengi sana naweza kusema kwa uhakika mkubwa sana, zaidi ya asilimia tisini hawajui kabisa kabisa wajibu wao kwa watanzania na wengi sana wamekwishasahau kwamba hata nafasi walizonazo ni kwa niaba yetu sisi.

  Serikali yetu imekuwa ikiongozwa na watu wenye upeo mdogo sana na ni wajinga kabisa wa madhara ya maamuzi yao ya kisiasa, kiuchumi na kijamii na moja ya kitu kinachochoa hali hii ni kuwa na mfumo ambao wao wenyewe haelewi mantiki yake, mipaka na madhara yake.
   
 14. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #14
  Jun 26, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Mimi nadhani umbumbu mbaya zaidi ni ule wa viongozi wetu, kwa nini mtu anakubali kuchukua nafasi ya uongozi kwenye jamii wakati hana uwezo wa kuwajibika katika nafasi hiyo, nawafananisha viongozi wetu na watoto wadogo, watoto wadogo hawajui, hawajui au hawawezi nini, wao ujua wanaweza kufanya kila kitu na wanajua kila kitu na ni kwa sababu mambo yao wanayafanya kwa instinct.

  Ni mbaya zaidi kwamba, viongozi ni mbumbumbu na wanaoongozwa majority ni mbumbumbu pia, matokeo ndio kama hayo sasa
   
 15. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #15
  Jun 26, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Unamaanisha kwamba, uonevu wote unaofanywa kwa kuhamisha wananchi kutoka kwenye makazi yao huwa yana approval ya president?
   
 16. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #16
  Jun 26, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Unaweza kutafsiri hivyo, kwani amekabidhiwa kwa mamlaka ya umma, huo umma ni kina nani? na je wakati wanapotwaa ardhi kwa manufaa ya umma huo umma unashirikishwa vipi kwenye hayo "manufaa"
  Kama alivyosema Rutashubanyuma kunahitajika mabadiliko kwenye hizi sheria, tuangalie upya hizi sheria za umiliki wa ardhi
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #17
  Jun 26, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Unaweza kutafsiri hivyo, kwani amekabidhiwa kwa mamlaka ya umma, huo umma ni kina nani? na je wakati wanapotwaa ardhi kwa manufaa ya umma huo umma unashirikishwa vipi kwenye hayo "manufaa"
  Kama alivyosema Rutashubanyuma kunahitajika mabadiliko kwenye hizi sheria, tuangalie upya hizi sheria za umiliki wa ardhi
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #18
  Jun 26, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Sasa tuziangilieje ndugu yangu, sababu hata tukipiga kelele na watawala wakaamua kuturidhisha kwa kuanzisha mchakato wa kuzibadilisha huo mchakato utapoanzia mpaka utakapoishia sisi hatutashiriki sana sana tutakuwa hapa JF kujifahamishana namna wabunge wanavyochangia kwenye mswada wa mabadiriko ya ardhi bla bla bla bla bla.

  Mimi nadhani tuangalie kama ni feasible economically kuwa tunapiga kura kuridhia ama kutoridhia sheria fulani fulani kisha rais atazisign kwa niaba yetu, ama sivyo kwa umbumbu walionao viongozi na watawala wetu wanaweza kuishia kubadirisha lugha tu basi, nakumbuka mwaka jana kuna mtawala kutoka wizara ya ustawi wa jamii kama sikosei akiwa kwenye kongamano la wazee alisema serikali inasubiri africa kusini wamalize mchakato wa kutengeneza sheria ya mafao kwa wazee ili waitumie kutengeneza yetu, nilikuwa na katoto kangu tunaangalia TV ilibidi niizime haraka sana kasielewe yule jamaa alikuwa anamaanisha nini.

  Pia, jana nilikuwa napitia sheria za kodi za Kenya na Uganda nimekuta zote zinafanana na yakwetu, nikabaki najiuliza inamaana sheria yetu ya kodi wakati inakopiwa kutoka kenya au uganda au kokote kule hao wacopiji hawakukumbuka kwamba tuna assets za kuwa na tax treatments na political tax motives tofauti kabisa na za kenya pamoja na uganda?

  Ninaimani kubwa sana, hata kwenye sheria ya ardhi kama itafanyiwa mabadiriko makubwa haitatofautiana na ile iliyopo kenya na huo ndio utakuwa mwanzo wa kutuingiza kwenye matatizo ya ardhi kama ya uko.
   
 19. T

  Tata JF-Expert Member

  #19
  Jun 26, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,745
  Likes Received: 662
  Trophy Points: 280
  Haya mambo yamekuwepo siku nyingi. Wewe jiulize wenyeji waliokuwepo mitaa ya posta mpya walienda wapi na walifidiwa vipi baada ya serikali ya mkoloni kutwaa hilo eneo kwa ajili ya kuliendeleza. Au jiulize wale wenyeji asilia wa Bukoba mjini waliokuwa na mashamba yao ulipo uwanja wa mpira wa Kaitaba walielekea wapi na walifidiwa vipi baada ya hilo eneo kuporwa kwa ajili ya kujenga uwanja? Je wana hisa kwenye huo uwanja au kwenye vitega uchumi vilivyoanzishwa maeneo waliyokuwepo kabla? Tatizo nadhani siyo watu kuhamishwa ila ni jinsi nzuri ya kuwaandalia malipo stahiki yatakayowawezesha kuendelea na maisha huko waendako. Hii haijalishi kabila, rangi, uraia wala dini ya mununuaji wote wanatakiwa kulipa fidia stahiki kwa wenyeji asilia.
   
 20. D

  Davie Member

  #20
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Tanzana ni nchi pekee ambayo mwekezaji anaonekana ni wa muhimu kuliko raia wake...
  ndio maana huwezi kushangaa ukiona polisi wakitumika kulazimisha raia kupisha eneo wnalokaa ili tu kumfurahisha mwekezaji..
   
Loading...