Raia wa Uingereza ndio Mgonjwa Wa Kwanza wa Mafua ya nguruwe TZ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Raia wa Uingereza ndio Mgonjwa Wa Kwanza wa Mafua ya nguruwe TZ

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Jul 10, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  KIJANA mmoja [17] raia wa nchini Uingereza amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kugundulika kuwa ana ugonjwa huo katika Uwanja wa Ndege wa jijini Dar Kijana huyo aliwasili katika viwanja hivyo akiwa anatokea nchini humo na alikuwa anaelekea nchini Kenya na kulazimishwa kushuka nchini kutokana na hali yake ilivyokuwa tete ili awahi kutibiwa. Kijana huyo aligundulika Julai 2, mwaka huu na Maafisa Afya wa Uwanja huo baada ya kumuona hali ya kiafya hairidhishi na kijana huyo kudai na kuwaambia anasumbuliwa na mafua. Hatua iliyofuata walichukua sampuli ya vipimo kwa kijana huyo na kugundulika kuwa ana ugonjwa huo na kumkimbiza katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu. Taarifa za kuthibitishwa kuwepo kwa mgonjwa huyo zilithibitishwa jana na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii. Dk. Aisha Kigoda wakati alipokuwa akitoa taarifa hizo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Dk. Kigoda amesema kuwa mgomjwa huyo amelazwa katika wodi maalumu iliyotengwa maalumu kwa wagonjwa hao endapo watapatikana. Hata hivyo amesema kijana huyo anaendelea vizuri na wananchi wasiwe na wasiwasi kwa kupatikana na maambukizi kutoka kwa mgonjwa kwa kuwa aliwahiwa kupatiwa matibabu. Hivyo aliwataka wanachi kuwa makini sana katika kipindi hiki na kumuwahisha mgonjwa mara moja endapo ataonekana ana dalili za ugonjwa huo. Pia amewataka wananchi wanaotumia nyama ya nguruwe wazingatie kanuni za afya na kuichemsha vizuri kabla hawajaila japo ugonjwa huo hauambukizwi kutokana na kula nyama hiyo. http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=2466878&&Cat=1
   
Loading...