RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Raia wawili wa Uholanzi wamekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa kutaka kusafirisha jumla ya tumbili hai 61
Walikuwa wanataka kuwasafirisha kuelekea nchini Albania.
Jeshi la Polisi limethibitisha kuwakamata raia hao. Hali hii imepelekea Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof Jumanne Magembe kumsimamisha kazi Mkurugenzi msimamizi wa wanyama pori Charles Mulokozi kwa kutoa vibali vya kusafirisha wanyama kwenda nje.
Kuhusu kumsimamisha kazi Mkurugenzi msimamizi wa wanyama pori Charles Mulokozi, Waziri Magembe amesema "Jana usiku tumekamata ndege ambayo ilikuwa inasafirisha nyani, inaonekana ni biashara inayofanywa kwa hiyo amesimamishwa kazi, uchunguzi ufanywe ili tuone hili jambo la kusafirisha wanyama nje ya nchi limefanywa kiasi gani na ni nani anafanya.