Raia wa Uholanzi amzaba vibao mwalimu mbele ya wanafunzi

ningekuwa uyo mzungu ningewakata mitama,bakola na kuchapa walimu wote ambao muda wa kufundisha ndio wanapanga ratiba
 
Saafi sana mama wa kiholanzi. Tunaomba uende na ikulu kwani kuna bogas mmoja mvivu sana utusaidie kumkata vibao. Kazi yake kusafiri safiri na kuombaomba tu.
 
Elimu kwanza ratiba baadae.Kazi ya kupanga ratiba inatakiwa kufanywa na mwalimu wa taaluma.Acha mzungu ashitakiwe kwa kumpiga raia makofi(kwa kuwa amevunja sheria) LAKINI ametufundisha kuwa makini na majukumu yetu ya kikazi
 
kwakweli hii ni aibu double double.
tumezidi kuwa omba omba hadi tunachapwa vibao sbb wanaotusaidia wanatuona wanyonge kiasi cha kuweza kuweza kutufanya lolote watakalo.
Pili tunatia aibu kwa uvivu wetu,hivi ina maana walimu watatu wakipewa kazi ya kuandaa ratiba ya shule hawawezi.
Yaani uandaaji wa ratiba ya shule usababishe ratiba zote za ufundishaji zisimame.
Ndo mana wazungu wanaamini kwamba ngozi nyeusi ndo tuna IQ ndogo kuliko rangi nyingine zote.Hili tukio ni aibu sana.
 
uyu mwalimu mkuu mbona katuangusha kwa nini hakumpa makofi uyu mzungu!
Huu unyanyasaji ndani ya ardhi yetu lazima uishe.
Kitendo kama icho can only be done to me nkiwa ughaibuni na sio nchini kwangu never never never
Kwa taarifa yako mwalimu imekula kwako as uyo mzungu ataambiwa arudi kwao habari itaishia apo
 
kwakweli hii ni aibu double double.
tumezidi kuwa omba omba hadi tunachapwa vibao sbb wanaotusaidia wanatuona wanyonge kiasi cha kuweza kuweza kutufanya lolote watakalo.
Pili tunatia aibu kwa uvivu wetu,hivi ina maana walimu watatu wakipewa kazi ya kuandaa ratiba ya shule hawawezi.
Yaani uandaaji wa ratiba ya shule usababishe ratiba zote za ufundishaji zisimame.
Ndo mana wazungu wanaamini kwamba ngozi nyeusi ndo tuna IQ ndogo kuliko rangi nyingine zote.Hili tukio ni aibu sana.


Hata sisi tunaamini hivyo, tuliwaita Wazungu, tukimaanisha "wa Mungu". Tukajiita Waafrika tukimaanisha "Wa Afrit" na tuko proud kujiita kizazi cha afrit. Na tunaona raha tukiwaita wenzetu kizazi cha Mungu.
 
Hawa waalimu wamevuna walichopanda!

Na bado wengine pia wamenyanyasika nao wengine watafuata kuzabwa makofi kwa vile Karatu ipo katika njia ya watalii, shule nyingi nyingi zimekuwa zikipata misaada/zawadi mbalimbali kutoka kwa watalii.

Mara nyingi wazungu watapenda kujua matokeo ya misaada yao.
 
Sasa hili la kuchukuwa misaada yake maana yake nini? Huyo 'muholanzi' nae ni limbukeni tu! ...huo msaada wake ulilenga waalimu au wanafunzi? Sasa kwa sababu amefadhili ndio anataka kuingilia hata namna ya uendeshaji wa vipindi? Ndio mambo haya haya tunayaona hata katika soka hapa kwetu....mtu akifadhili basi anataka yeye ndiye aamue wachezaji wa kusajili (anataka afanye kazi ya coach/manager!).

Kama hakuna ratiba, walimu watafundisha kwa utaratibu upi (si kutakuwa na collisions!?) - hata kama ni kweli pengine ratiba hiyo ilipaswa kupangwa kabla ya shule hazijafunguliwa...lakini alipaswa kwanza kujua kwa nini haikupangwa kipindi hicho (ingawa hili kimsingi haimuhusu mfadhili!).

Yote haya ni kwa sababu ya ujinga na umasikini ambao CCM imeshindwa kuuondoa!
 
mwalimu mkuu imekula kwake maana mwisho wa siku atakua addressed "yule mwalimu aliyepigwa vibao na mzungu".
ungeajua hawa wapuuzi wanavyotunyanyasa tukiwa kwao hata asingethubutu kusema anamshukuru Mungu...if it was me huyo mzungu sijui ningemng'ata au sijui nongempiga roba!!!!
 
Hii kazi ya ualimu sasa imekuwa ni ya kudhalilishana sana,sasa huyu mholanzi watamshitakia nini?maana sheria zetu ni double standard.yule mkuu sijui wa mkoa au wilaya aliyewashikisha walimu chini akawalamba bakora sawasawa alifanywa nini? subiri tuone.
 
Ilikuwaje ratiba iandaliwe na walimu wa shule nzima badala ya Mwalimu wa Taaluma? Huyo Mama wa Kizungu kawakumbusha majukumu yao hao walimu. Atakuwa alikuta wanaunga stori, kama kweli angewakuta wote wanahangaika na manila kadi asingetoa kichapo. Hathivyo, namshauri siku moja ajaribu kwenda kutoa kichapo kule wilaya ya Tarime, hapo atafahamu kilichompeleka Afrika.
 
Hata sisi tunaamini hivyo, tuliwaita Wazungu, tukimaanisha "wa Mungu". Tukajiita Waafrika tukimaanisha "Wa Afrit" na tuko proud kujiita kizazi cha afrit. Na tunaona raha tukiwaita wenzetu kizazi cha Mungu.
nilikuwa sijui maana ya mzungu kumbe ni wa Mungu!!! ama kweli sie tulijilaani wenyewe
 
yaani angepiga mitama kabisa na vichwa ..yaani kazi ya kukaa mtu mmoja kukaa kwenye computer afungue excell wanarundikana wote kupanga ratiba....PIGA MAKOFI PUMBAFUU
 
Raia mmoja wa Uholanzi, Marise Koch, amemfanyia kitendo cha udhalilishaji Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Marera iliyopo kata ya Rhotia Wilayani Karatu mkoani Arusha kwa kumpiga vibao mbele ya wanafunzi na walimu wenzake.

Taarifa ambazo NIPASHE imezipata na kuthibitishwa na viongozi wa Idara ya Elimu Wilaya ya Karatu na Jeshi la Polisi, zinasema kutokana na udhalilishaji huo, raia huyo wa Uholanzi ameshafunguliwa jalada lenye namba KRT/RB/835/2012 katika kituo cha polisi Karatu kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Marera, Emmanuel Ginwe, alisema alipigwa vibao viwili na Koch baada ya kuwakuta walimu wa shule hiyo wakipanga ratiba ya shule. Ginwe alisema tukio hilo lililotokea Februari 14, 2012 majira 4:30 asubuhi ambapo Koch ambaye anafadhili shule hiyo kwa kukarabati majengo ya shule, ofisi, nyumba za walimu na kompyuta ndogo za wanafunzi kufanyia michezo na kujifunzia kuandika alifika shule hapo kutembelea kama kawaida. Alisema baada ya kufika shuleni hapo, alikuta walimu wakipanga ratiba ya shule na kuanza kuhoji kwanini walimu hawajaingia madarasani kufundisha wanafunzi ambapo alijibiwa kuwa wamepewa maelekezo ya kuandaa ratiba ya shule na baada ya kumaliza kazi hiyo wataingia madarasani kufundisha.

Hata hivyo majibu ya walimu hao hayakumridhisha Koch na kuamua kwenda ofisini kwa Mwalimu Mkuu na kuanza kumfokea kwamba yeye anafadhili vitu vingi, lakini kumbe walimu hawafundishi na kuanza kukusanya kompyuta zake ndogo kwa lengo la kuzichukua. Mwalimu Mkuu wa shule hiyo hata hivyo alimsihi asichukue kompyuta hizo, lakini alikataa na alipoona anazuiliwa, alipiga vibao mwalimu huyo huku akiendelea kuzikusanya komputa na kumnasa tena vibao tena mwalimu mkuu na kuchukua kompyuta zake 70 kati ya 93 zilizokuwepo na kuondoka zake.

“Nimedhalilishwa sana mbele ya walimu, wanafunzi na mke wangu ambaye ni mwalimu, namshukru Mungu wakati ananipiga vibao japo ni mwanamke sikuweza kujibu mapigo,” alisemwa Ginwe.

Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Karatu, Peter Simwanza, alisema kitendo hicho ni cha kiudhalilishaji

Source: NIPASHE

My Take: Misaada inatudhalilisha sana watz tujaribu kuiepuka na kujaribu kutumia rasilimali zetu wenyewe kujiletea maendeleo.

Alitakiwa ku-retaliate in microseconds! i.e. tit for tat
 
Hapo ni sawa kabisaa! watu hawataki kufanya kazi! wanataka kufadhiliwa! mfadhili anawakuta wamekaa ofisini wanapiga story! hawataki kufundisha! Kwani nini asikasirike? Ndugu zangu Watanzania wenzangu ifike mahali sasa tujikomboe tufanye kazi kwa bidii>Tizama walimu hawa hawana huruma wakuwafundisha watoto! hata kuchangia dawati la shule! Mzungu anatoa computer! anakarabati majengo ya shule! halafu awakute walimu mmejikusanya ofisini mnapiga gumzo kwa kizingizio cha kuanda ratibu! "TUBADILIKE NDUGU ZANGU"
 
Mbona kuna yule kiongozi wa chama na serikali miaka ya nyuma kwenye mkutano alimpiga kofi mwananchi..
Kati ya huyu na huyo mzungu nani anaafadhali
 
Back
Top Bottom