Raia wa Uholanzi amzaba vibao mwalimu mbele ya wanafunzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Raia wa Uholanzi amzaba vibao mwalimu mbele ya wanafunzi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Power G, Mar 12, 2012.

 1. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Raia mmoja wa Uholanzi, Marise Koch, amemfanyia kitendo cha udhalilishaji Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Marera iliyopo kata ya Rhotia Wilayani Karatu mkoani Arusha kwa kumpiga vibao mbele ya wanafunzi na walimu wenzake.

  Taarifa ambazo NIPASHE imezipata na kuthibitishwa na viongozi wa Idara ya Elimu Wilaya ya Karatu na Jeshi la Polisi, zinasema kutokana na udhalilishaji huo, raia huyo wa Uholanzi ameshafunguliwa jalada lenye namba KRT/RB/835/2012 katika kituo cha polisi Karatu kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Marera, Emmanuel Ginwe, alisema alipigwa vibao viwili na Koch baada ya kuwakuta walimu wa shule hiyo wakipanga ratiba ya shule. Ginwe alisema tukio hilo lililotokea Februari 14, 2012 majira 4:30 asubuhi ambapo Koch ambaye anafadhili shule hiyo kwa kukarabati majengo ya shule, ofisi, nyumba za walimu na kompyuta ndogo za wanafunzi kufanyia michezo na kujifunzia kuandika alifika shule hapo kutembelea kama kawaida. Alisema baada ya kufika shuleni hapo, alikuta walimu wakipanga ratiba ya shule na kuanza kuhoji kwanini walimu hawajaingia madarasani kufundisha wanafunzi ambapo alijibiwa kuwa wamepewa maelekezo ya kuandaa ratiba ya shule na baada ya kumaliza kazi hiyo wataingia madarasani kufundisha.

  Hata hivyo majibu ya walimu hao hayakumridhisha Koch na kuamua kwenda ofisini kwa Mwalimu Mkuu na kuanza kumfokea kwamba yeye anafadhili vitu vingi, lakini kumbe walimu hawafundishi na kuanza kukusanya kompyuta zake ndogo kwa lengo la kuzichukua. Mwalimu Mkuu wa shule hiyo hata hivyo alimsihi asichukue kompyuta hizo, lakini alikataa na alipoona anazuiliwa, alipiga vibao mwalimu huyo huku akiendelea kuzikusanya komputa na kumnasa tena vibao tena mwalimu mkuu na kuchukua kompyuta zake 70 kati ya 93 zilizokuwepo na kuondoka zake.

  "Nimedhalilishwa sana mbele ya walimu, wanafunzi na mke wangu ambaye ni mwalimu, namshukru Mungu wakati ananipiga vibao japo ni mwanamke sikuweza kujibu mapigo," alisemwa Ginwe.

  Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Karatu, Peter Simwanza, alisema kitendo hicho ni cha kiudhalilishaji

  Source: NIPASHE

  My Take: Misaada inatudhalilisha sana watz tujaribu kuiepuka na kujaribu kutumia rasilimali zetu wenyewe kujiletea maendeleo.
   
 2. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Tanzania tunadhalilishwa jamani,yote haya ameyaleta JK kwenda kwake ng'ambo kuhemea kama Rais anahemea wewe hata ukipigwa ngumi huna pa kukimbilia. lakini nasi tuache uvivu
   
 3. king'amuzi

  king'amuzi JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Pole sana mwalimu, lakushangaza badala ya kushitakiwa hapa utasikia amepewa adhabu ya kuondoka nchini mara moja.Hapa ndipo uzalendo unapofia kujali wageni kuliko wazawa
   
 4. SIMBA WA TARANGA

  SIMBA WA TARANGA JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 992
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safi sana mzungu, ingewezekana ungewazaba walimu wote. Badala ya kufundisha eti wote mnapanga ratiba.
   
 5. isambe

  isambe JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 2,053
  Likes Received: 881
  Trophy Points: 280
  punda haendi bila mateke!!!safi saana mama wa kizungu
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Sawasawa alivyofanya huyo mama, nyie hamkuona wakati wa kupanga ratiba ila wakati mnatakiwa muwe mnafundisha?

  Kafanya sawasawa, hilo ndio tatizo la Watanzania, sababu nyingi na kufanya mambo bila mipango, mtoto analetwa na wazazi anajuwa anakwenda kusomeshwa kumbe waalimu "wanapanga ratiba", pengine ukute kawakuta wanasukana, hiyo ya kupanga ratiba wanazuga tu.

  Waandishi wa habari wa huko nendeni mkajuwe mama kakikuta nini, tupate upande wa pili wa habari hii.

  Mimi namuunga mkono huyo mama.
   
 7. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #7
  Mar 12, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Wazungu wanawake kwa makofi!
  Ulikuwa unaleta ubabe na kukatalia komputer zako?

  Mh pole mwalimu muache kutega mfundishe watoto wapasi
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Mar 12, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Halafu huko si ndio kwa kina dokta?
   
 9. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #9
  Mar 12, 2012
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Kwanini cku JK akiwa nje huku akijinadi kwa madaha ya Tanzania tegemezi asizabwe nae makofi au mangumi kbs?
   
 10. M

  Mpigaji JF-Expert Member

  #10
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Amejitakia mwenyewe,kama alitaka kuchukua kompyuta zake wangemwacha aende zake!Umasikini wetu usitufanye kuwa watumwa katika nchi yetu!LOL!
   
 11. M

  Mpigaji JF-Expert Member

  #11
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Inaelekea unaweza hata kula matapishi ya mzungu!
   
 12. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #12
  Mar 12, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Sisi watz tuna matatizo,kwani ratiba huchukua muda gani?si wangepanga baada ya vipindi?au wale ambao hawakua na vipindi muda huo wangeendelea kupanga ratiba,halafu wale wanapotoka kwenye vipindi wanaendelea nayo kisha hawa wengie wakaingia kwenye vipindi vyao muda unapofika?kisha mwisho wa siku wanamaliza na kushare kilichopatikana.Sisi watzee ni wavivu sana,halafu visingizi huwa haviishi.Hiyo ndyio dawa,ijapokua sheria haziruhusu,maana ukiruhusu itakua ni fujo tupu,kila mtu atamzaba mwenzie vibao ,hata kwa kisingizio chake.
   
 13. Kitumbo

  Kitumbo JF-Expert Member

  #13
  Mar 12, 2012
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 547
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hapo kwenye red unaonyesha ni jinsi gani ubongo wako unavyoujaza ujinga na utegemezi wa kufikiri. angalia usije ukaacha hata kusomesha watoto wako ukitegemea JK yupo!
   
 14. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #14
  Mar 12, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,105
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 160
  Safi sana ananikumbuka mkuu wa wilaya ya bukoba alioamishwa alivyokuwa anazunguka mashuleni kuchapa walimu bakora sababu badala ya kufundisha wapo wanaendesha bodaboda na kulewa.ratiba ya kufundisha inapangwa mapema si muda wa kufundisha ndio mnapanga ratiba.mi ningekuwa ningempiga mtama kabisa.tena bora alivyochukua hizo computers zake akawape shule nyingine.walimu wawe wanajali muda si kila siku wanapanga ratiba
   
 15. uttoh2002

  uttoh2002 JF-Expert Member

  #15
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,681
  Likes Received: 2,740
  Trophy Points: 280
  Uforauni huu, umepigwaje makofi na mwananke usirudishe? Tena Wa Kizungu? Aibu tupi!


   
 16. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #16
  Mar 12, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Umeona eeh, na si ajabu walikuwa wanasogoa tu na si kupanga ratiba. Hizi shughuli zinatakiwa kufanywa kipindi cha likizo; ingawa siungi mkono kupigwa vibao, lkn kuchukua vitu vyake namsupport.
   
 17. SIMBA WA TARANGA

  SIMBA WA TARANGA JF-Expert Member

  #17
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 992
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lazima wewe utakuwa mwalimu, tena wa sayansi kimu.
   
 18. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #18
  Mar 12, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Wa Tz tumezidi uvivu na uzembe
   
 19. M

  MERCYCITY JF-Expert Member

  #19
  Mar 12, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 348
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 60
  Wana Jf tuwe wakweli. Kwanini watoto wetu wanafeli. Huyu mzungu kaona ubabahishaji wa hawa waalimu na hana pa kuwasemeha kwa sababu system yote ndiyo hivyo. Akaamua kuhukumu mwenyewe. Je tunamuona mzungu kafanya kosa. Kosa lake nini wakati baadhi ya watoto wetu wanafika darasa la saba hawajuhi kuandika. Tuache ushabiki tujiangalie wenyewe. Huyu mzungu alitaka wawe madarasani kufundishwa. Hii si kwa faida yetu?. Sasa kama hii serikali yetu kama haiwezi kuwatoa watu wazembe mpaka wageni wanatusaidia si ni aibu. Serikali imeshindwa kuwatoa mafisadi walioiba pesa na wanajulikana sasa yeye mzungu hafanyeje. Huyu mzungu alikuwa anafkisha ujumbe kwa jamii yetu kwamba kuna uozo mwingi kwenye idara zetu za serikali. Viongozi fanyeni kazi kusafisha kwa sababu hawa wazungu wanatuona mataahira tu watu wasioweza kufikiri.
   
 20. M

  Mpigaji JF-Expert Member

  #20
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwani wewe Sayansi Kimu haikusaidii?Chukulia aliyechapwa makofi ni Baba yako Mzazi!
   
Loading...