Raia wa Tanzania waruhusiwa kuingia nchini Kenya bila kukaa karantini

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Kenya imetoa orodha ya nchi 147 ambazo raia wake wataruhusiwa kuingia nchini humo bila kukaa karantini

Katika orodha ya sasa, Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa nchi hizo ambapo katika orodha ya awali Tanzania haikuwepo

Awali nchi hiyo ilikuwa inalazimisha raia wanaotoka nchi zenye hatari kubwa ya maambukizi ya CoronaVirus kukaa karantini kwa sababu za kiusalama

1600187011398.png
1600187025294.png
 
Chonde chonde TCAA. Msiruhusu Kenya Airways kutua Tanzania kabla ya kuondoa utata uliopo kwenye ubia kati ya Precision Air na Kenya Airways kuhusu miruko, Kama Kenya Airways itaruhusiwa, basi Air Tanzania na Precision Air ziruhusiwe pia kutua Kenya kwa uwiano ulio na usawa, vinginevyo. Ngondo iendelee kuwa ngondo hadi kieleweke.🧐
 
Hii nimeipenda!!!
ILA tusisahau kuwa, imewezekana baada ya Tanzania Kuzuia ndege yao ya KQ kuja hapa kwetu hadi waweke hali rafiki ya Watanzania kwenda Kenya. Kenya inategemea Tanzania kwa wasafiri kutoka ukanda huu kwenda Nje hivyo hawana jinsi.
NA BADO TUNASONGA.
 
Back
Top Bottom