Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,397
Mahakama Kuu Divisheni ya Uhukumu Uchumi imemhukumu raia wa Peru, Wallenstein Santillan kwenda jela miaka 20 baada ya kupatikana na hatia ya kuingiza nchini dawa za kulevya aina ya Cocaine gramu 1420.78.
Hukumu hiyo imetolewa leo na Jaji Winfridar Koroso baada ya kusikiliza mashahidi 10 wa Jamhuri bila kuacha shaka wamemuona mshtakiwa ana hatia.
"Mahakama hii bila kuacha shaka imemuona mshtakiwa ana hatia na inamhukumu kwenda jela miaka 20 ili iwe fudhisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo" amesema jaji katika hukumu hiyo.
Kabla ya hukumu hiyo kutolewa upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Tumaini Kweka akisaidiana na Mawakili wa Serikali Tuli Helela na Kija Luzingana, uliomba mahakama kutoa adhabu Kali kwa mshtakiwa.
Kweka amedai kwa kuwa mahakama imemuona mshtakiwa ana hatia itoe adhabu Kali iwe fundisho kwa wageni wenye tabia ya kugeuza Tanzania kama daraja la kupitishia biashara haramu.
- ITV