Raia wa Peru ahukumiwa miaka 20 kesi ya uhujumu uchumi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,551
2,000
Mahakama Kuu Divisheni ya Uhukumu Uchumi imemhukumu raia wa Peru, Wallenstein Santillan kwenda jela miaka 20 baada ya kupatikana na hatia ya kuingiza nchini dawa za kulevya aina ya Cocaine gramu 1420.78.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Jaji Winfridar Koroso baada ya kusikiliza mashahidi 10 wa Jamhuri bila kuacha shaka wamemuona mshtakiwa ana hatia.

"Mahakama hii bila kuacha shaka imemuona mshtakiwa ana hatia na inamhukumu kwenda jela miaka 20 ili iwe fudhisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo" amesema jaji katika hukumu hiyo.

Kabla ya hukumu hiyo kutolewa upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Tumaini Kweka akisaidiana na Mawakili wa Serikali Tuli Helela na Kija Luzingana, uliomba mahakama kutoa adhabu Kali kwa mshtakiwa.

Kweka amedai kwa kuwa mahakama imemuona mshtakiwa ana hatia itoe adhabu Kali iwe fundisho kwa wageni wenye tabia ya kugeuza Tanzania kama daraja la kupitishia biashara haramu.

- ITV
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
4,237
2,000
Kwa lile agizo la Rais hawana budi kuziendesha hizi kesi kwa haraka. Maana ushahidi unakuta uko wazi kabisa! Mtu amekamatwa na dawa za kulevya, tena zimetolewa tumboni, lakini unashangaa kesi inachukua miaka kadhaa huku tukiambia upelelezi bado haujakamilika.
 

mwandende

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
4,110
2,000
Na wale MNAO WAFUNGA MAISHA kwa KOSA kama hilo mnatumia SHERIA GN?wengine mnawafunga miaka 20....MAHAKIMU wengine ACHENI ROHO MBAYA kwa watoto wa wenzenu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 

kayaman

JF-Expert Member
Aug 3, 2013
4,014
2,000
Yule mchina ivory queen alieua tembo zaidi ya 400 alihukumiwa 15yrs au alipe fine aende zake ila huyu kujibebea unga wake wanamgunga 20yrs bila hata option ya kulipa fine

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom