Raia wa Pakistan akamatwa kwa kuingia nchini kinyemela kwa kisingizio kuwa Tanzania hakuna Corona

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,933
25,268
paks.jpg
Idara ya uhamiaji mkoani Kagera inamshikilia mtu mmoja raia wa Pakstan aliyeingia nchini kinyume na taratibu akitokea nchini Uganda Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutangaza Tanzania ni salama na hakuna Corona.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari mjini Bukoba October 8,mwaka huu, Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kagera Kamishina msaidizi Hamza Ismail Shaban amesema kuwa katika utaratibu wao wa kila siku wa kuhakikisha watu wanaoingia na kutoka wanakuwa ni Raia au watu wanaostahili kuwemo nchini, oktoba 7, mwaka huu katika uwanja wa ndege uliopo Bukoba afisa aliyekuwa zamu aliweza kumkamata raia huyo akitaka kupanda ndege kuelekea jijini Dar es Salaam.

“Mkoa wetu kama tunavyojua unapakana na nchi mbalimbali, na ikumbukwe janga la Corona kwa nchi za Afrika Mashariki lilikuwa bado ni tatizo na nchi nyingi zilikuwa zimefunga mipaka yake na wananchi wake walikuwa LOCKDOWN na bwana huyu amekaa Uganda kwa takribani miezi 6 kuanzia mwezi wa tatu na amethibitisha ameshindwa kuondoka Uganda kwasababu ya LOCKDOWN na kuamua kukimbilia kwetu japo ameingia kinyemela kwa njia ambazo sio rasmi” Amesema Kamishina Shaban.

Ameongeza kuwa baada ya Rais Magufuli kuitangazia dunia kuwa Tanzania hakuna Corona na shughuli zinaendelea kama kawaida na kuongeza kuwa raia huyo alipata taarifa hizo na kuamua kukimbilia Tanzania na baada ya kuingia akagundua kuwa hakuna Corona ambapo ameeleza kuwa uwepo wake hapa nchini sio rasmi kwakuwa ameingia kinyemela na anaishi nchini kinyume cha sheria.

Kamishina Shaban ametumia fursa hiyo kuwataka raia wanaotaka kuingia Tanzania kufata taratibu zilizowekwa na nchi yetu pamoja na kuwataka watanzania wazalendo kuhakikisha wanawabaini watu wanaoingia nchini kinyemela na kuwatolea taarifa mahala popote watakapo waona.

“Nitoe rai kwa watanzania wazalendo kuwa wasiwe sababu ya watu ambao sio watanzania au ambao hawana vibali vya kuwa hapa nchini kuingia na kuwahifadhi badala yake watoe taarifa kwa idara ya uhamiaji au kwa viongozi wa serikali mahali walipo, kama tunavyojua nchi yetu tupo kwenye mchakato wa uchaguzi hivyo hatupaswi kuruhusu watu wasiokuwa raia au tusiowajua kuingia hapa pasipokujua lengo lao.” Amesisitiza Shaban.

Kwa upande wake mtuhumiwa huyo amesema kuwa amekuja Tanzania baada ya kukaa LOCKDOWN nchini Uganda kwa takribani miezi 6 kutokana na janga la Corona na aliposikia Tanzania hakuna Corona alijaribu kutumia njia mbadala za kuweza kumfikisha hapa nchini ambapo ameeleza kuwa alikuja kwa gari ndogo aina ya Taxi.

Amesema kuwa amekuwa akija Tanzania mara kwa mara kutokana na biashara zake anazozifanya hapo awali kabla ya nchi nyingi kufunga mipaka yake kutokana na Corona hivyo Tanzania anaijua.
 
Hii habari nami nimeisikia RFA leo asubuhi nimemsikia afisa uhamiaji na pia nimemsikia huyo Mpakistani lakini niseme kuna uliyoyapindisha na huenda umefanya hivyo kwa makusudi kwa lengo lako mahususi,ni kweli Mpakistani amesema alikuwa Uganda na amekaa kule sasa ni miezi sita na amechoka hivyo nia yake ni kurudi kwao Pakistan lakini kule mipaka bado imefungwa hivyo hakuna uwezekano wa kutoka sasa kwakuwa Tanzania mipaka ipo wazi na safari za kimataifa zimeruhusiwa hivyo ilimbidi atoke huko Uganda kwa njia za panya afike Tanzania apate usafiri wa kumrudisha kwao lakini wewe ulivyoandika na unavyotaka ionekane ni kama amekuja kuishi hapa "Eti kwa kuwa hakuna Corona", N.b:Hata kama mnataka kumtukuza huyo mungu mtu wenu msipindishe habari.
Okay, angalau nimeelewa sasa.
 
Sasa si wamruhusu aende kwao. Wakati mwingine tunajipa gharama bure za kuwatunza.
 
Mpakistani tena Katokea border ya uganda


Ngada 100% nina uhakika na kaachwa kwenye mataa na wenyeji
 
Mpakistani tena Katokea border ya uganda


Ngada 100% nina uhakika na kaachwa kwenye mataa na wenyeji
Yuko ontransit wamwache aende zake, tuna uhusiano mzuri wakibaloxi na pakistan, wamkabidhi ubalozini wao watajua pakumpeleka
 
Back
Top Bottom