Samahani wapendwa..nmeona kitu hiki sehemu nikaona nije kupata uhakika..huku kisima cha habari za kina..
Serikali kupitia Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma, tarehe 13/6/2016 imetoa waraka wenye kumbukumbu nambari CFC 26/205/01 'B' 46 kwenda kwa Makatibu wakuu wote, Wakuu wa Idara, Wakurugenzi, Wakuu wa Taasisi za umma na Watendaji wakuu wa wakala wa serikali.
Pamoja na mambo mengine waraka huo unaainisha mambo yafuatayo;
1. Kusitisha ajira zote mpya serikalini.
2. Kusitisha nyongeza zote za mishahara.
3. Kusitisha utoaji vibali kwa watumishi waliokuwa likizo bila malipo kurudi kazini.
4. Kusitisha vibali kwa watumishi wanaoondoka serikalini kwa likizo za bila malipo na kisha kurudi tena serikalini kwa cheki namba za awali.
5. Kusitisha utoaji vibali vya kurudi kazini kwa watumishi wanaochukua likizo bila malipo.
6. Kusitisha utaratibu wa watumishi kuhama ofisi moja kwenda nyingine kwenye mshahara mkubwa zaidi ya ule wa ofisi ya awali.
7. Kusitisha miundo yote mipya ya utumishi.
BAADHI YA ATHARI ZITAKAZOTOKANA NA WARAKA HUU;
1. Hakutakuwa na ajira mpya serikalini kwa sasa hadi itakapotangazwa vinginevyo. Hii ni pamoja na ajira mpya za walimu zilizokuwa zitangazwe kuanzia mwezi uliopita. Kwa hiyo wale ndugu zangu waliohitimu "shahada za ualimu" mwaka jana wanaosubiria ajira wanaweza kutafuta shughuli zingine za kufanya. Ajira zao kwa sasa hazipo. Mpaka itakapotangazwa vinginevyo.
2. Watumishi wa umma hawatakuwa na nyongeza ya mishahara hata kama wakipandishwa madaraja au vyeo (mpaka itakapotangazwa vinginevyo).
3. Watumishi waliokuwa wakitoka serikalini kwenda kufanya kazi kwenye miradi kwa "likizo zisizo na malipo" na hatimaye kurudi tena serikalini kwa sasa hawataruhusiwa.
Hii inaweza kuathiri serikali kwa sababu watumishi hawa walikua wakienda kujifunza uzoefu mpya na kukuza "career" zao, na wakirejea serikalini huongeza ufanisi. Lakini serikali imesema wakichukua "likizo bila malipo" hawataruhusiwa kurudi tena. Means watakua wamejifukuzisha kazi wenyewe.
4. Hakutakuwa na utaratibu wa kuhama ofisi moja kwenda nyingine ndani ya idara za serikali hata kama una sifa na vigezo vya nafasi husika. Yani kwa mfano Badra Massoud alikua Mkuu wa Idara ya mawasiliano na PR pale DAWASCO, akatoka akaenda TANESCO, kisha Wizara ya Nishati, kabla ya kepelekwa MAELEZO. Kuanzia sasa utaratibu huo hautakuwepo tena.
5. Waraka huu utaathiri pia muundo wa ajira katika halmashauri na wilaya zetu. Baadhi ya nafasi katika halmashauri zitafutwa na baadhi ya idara zotaunganishwa kuwa idara moja.
Baadhi ya athari zinazotarajiwa ktk halmshauri na wilaya ni;
(a). Afisa Elimu atabaki mmoja. Hakutakuwa na Afisa Elimu wa Msingi wala wa Sekobdari kama ilivyo sasa.
(b). Nafasi za Afisa elimu michezo, elimu watu wazima, ufundi, na elimu maalumu zitaondolewa. Kazi zao zitafanywa na Afisa Elimu mmoja atakayeshughulikia intervention zote.
(c). Nafasi ya Afisa Habari wilaya/halmashauri kuondolewa.
(d). Idadi ya maafisa Utumishi itategemea na ukubwa wa halmashauri husika.
(e). Nafasi ya Afisa Utamaduni itaondolewa na kazi zake zitafanywa chini ya ofisi ya Afisa Elimu.
(f). Idara ya Maendeleo ya jamii/Ustawi wa jamii itakuwa kitengo chini ya Idara ya Afya.
Mwenye taarifa na haya tujuzane..