Raia wa Nigeria akamatwa na heroin akitokea Tanzania

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,477
15,320
cocaine-suspects.jpg

Odogwu Augustine Ike (kushoto)

Raia mmoja wa Nigeria amekamatwa na kilo 2.150 a heroin akitokea Tanzania. Odogwu Augustine Ike (57) alikamatwa juzi Jumatano katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abuja akitokea Tanzania na ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia. Amedai alisafirisha dawa hizo baada ya kuhaidiwa kupewa Naira 600,000 za Kinigeria ambazo ni sawa na Tsh. 4,270,237/-. Mnigeria huyo ana mke na watoto wanne.

NOTE: Kiasi ktk TZS kisomeke 4,270,237/-

Vyanzo: Two caught with cocaine, heroine as international traffic moves to Kaduna airport
‘I inserted 386 grammes of cocaine in my anus for N1m’ - Vanguard News
 
kuna mnigeria mwingine alikamatwa uwanja wa kia na dawa za kulevya, nadhani mwaka jana au juzi alihukumiwa kifungo cha maisha.
 
...[HASHTAG]#EMT[/HASHTAG]...inavyoelekea bado kuna watu wanatoka na madawa ya kulevya kwa militia viwanja vyetu hapa tanzania...
MARA nyingi kumkamata mtu anaye safirisha unga kwa njia ya tumbo inataka akili sana...
Kwa kumsoma msafiri....

Ova
 
Makonda anabezwa wakati hali ni mbaya...taifa letu linaanza kuwa na sifa mbaya kimataifa
Kuna mijitu usipochunga inakufanya uwashangilie washirika wao kumzomea Makonda. sasa akifuatiliwa utajikuwa anakwambia alianzia kanisa la mtumishi wa Mungu.
 
Nimemkumbuka Makonda mbabe wa vita, bila shaka ukifuatilia kwa undani namna alivyokamatwa itakuwa alitoka nchini kwetu siku ya ijumapili ambapo asubuhi alikuwa akisali kwa nabii tambo asiye na uwezo wa kufufua hata PANYA muigizaji.
Nchemba yuko kimya midomo imewekwa plasta
 
Back
Top Bottom