Raia wa Misri afundisha kiswahili chuo kikuu, Misri

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,298

Lugha ya kiswahili ni moja kati ya lugha zinazoendelea kukua kwa kasi na kusambaa duniani huku mataifa mengi yakianza kujikita katika lugha yenye utamu katika mazungumzo.

Lugha ambayo inavutia na kumshawishi mzungumzaji kuitumia mara nyingi kutokana na ladha tamu ya lugha hiyo.

Mohammedi Yousri ni raia wa kimisri aliezaliwa na kukulia nchini misri.
akiwa amezaliwa katika desturi na mila za kuifahamu lugha ya kiharabu lakini kutokana na mapenzi yake yakutaka kufahamu lugha za kimataifa alijikuta akiingia katika uwanja mzito wa kukifunza lugha hii ya kiswahili na hatimae kuifahamu hadi kuja kuwa mwalimu katika chuo kikuu.

Katika harakati zake za kuifahamu lugha hii alijikuta akiamua kutembelea Afrika ya mashairiki ili kukuiza lugha yake

yafuatayo na mahojianio mafupi ambayo niliobahatika kufanya nae akiwa nchini Misri lakini kutokana na mawasiliano nipende kuwaomba radhi kuwa sitoweza kuleta mahojiano yote kwa kuwa hayakumalizika ila panapo majaaliwa nitawaletea nusu ya mahojiano hayo ila naahidi kuwa siku nyingi tutazungumza nae kwa kirefu zaidi iwapo tutapata mawasiliano mazuri.
nilianza kwa kumuuliza.

MIMI MALENGA - kwanini uliamua kujifunza kiswahili ?

MOHAMEDI-Kuna sababu nyingi, ya kwanza kiswahili ni lugha rahisi na tamu sana wowote akiisoma ataipenda, na ya pili ni lugha ya nchi muhimu barani afrika hasa nchi za afrika mashariki kama t.z na kenya na uganda na ruwanda na burundi, na raia ya nchi hizo ni wema sana na wana tabia nzuri kabisa na niliwapenda niliposafiri t.z , ya tatu ni misri inapaswa kuimarisha zaidi uhusiano wake baina ya nchi hizo na mwanzo wa jambo hilo ni lugha , kwani lugha ni msingi wa kila uhusiano na hii ni wajibu wangu mm mwalimu wa lugha ya kiswahili na asili yangu ni mmsiri kuwaelemisha wanafunzi hapa chuo kikuu umuhimu wa lugha ya kiswahili ili wanafunzi hawa baadaye kushiriki katika maendeleo ya mahusiano ya misri na nchi hizo

MIMI MALENGA -Ulitumia muda kujifunza kiswahili na mpaka kukielewa ?

MOHAMMED- Mm niliaoma kiswahili kwa muda wa miaka minne.. nilielewa kiswahili na nilianza kuandika na kuongea baada ya mwaka mmoja.. ili kiwango changu wakati huu huu kilikuwa chini , nilijitahidi na nilisoma kwa bidii ili kufika katika kiwango unachokiona sana hivi kupitia miaka ya chuo kikuu na nilifiki kiwango cha juu kabisa baada ya safari yangu kule t.z nilisoma sana na niliongea kiswahili sana .. kama unavyojua lugha sio maneno ya kuandika tu bali ni kuongea na mazungumzo na anayeelewa lugha anapaswa kuitumia katika mazungumzo maalumu


MIMI MALENGA-Kwa hapa Tanzania wengi bado wanaamini kiswahili siyo lugha ya biashara ama lugha inayolipa kama kingereza,je imani hiyo mnayo watu wa Misri ama mnachukuliaje ama kwa huko Misri kuna fursa ya kibiashara kwa wanaozungumza kiswahili ?

MOHAMEDI-Tazama.. kila lugha ina umuhimu wake, na unaweza kuwa na kitu hujui thamani yake, hali hii ni kama lugha, labda kwangu mm au watu wa misri nafikiri kama mm naongea kiswahili naweza kufanya buashara yangu kule tanzania au nchi yoyote humu afrika mashariki , naongea kiswahili vizuri na ninayo biashara yangu maalumu nitaweza kushinda kule, hii ni kwa mfano, na watanzania au waswahili kwa ujumla wanaweza kufanya kazi hapa misri kama mwalimu wa kiswahili au unaweza kufanya biashara yako hapa ukiwa unajua kiarabu
-
MIMI MALENGA-Uliwahi jaribu kuomba kazi ya kufundisha kiswahili katika nchi za Afrika mashariki ama sehemu nyingine duniani ?

MOHAMEDI-Nakwambia mm sasa hivi ni mwalimu wa lugha ya kiswahili katika chuo kikuu maalumu hapa misri, ila natamani kufanya kazi katika nchi yoyote katika afrika mashariki na kuendeleza katika mastar yangu ma masomo ya baada ya chuo kikuu , nikipata fura nitaishika kwa nguvu

MIMI MALENGA-Kwa hapa Tanzania lugha ya kingereza huanza kufundishwa katika shule za sekondari ama upili,na lugha nyingine za kigeni kama kifaransa na kispania hufundishwa katika college,vipi kiswahili katika nchi ya misri huzna kufundisha katika kiwango gani cha shule ?

MOHAMEDI-Hapa shuleni hakuna kufundisha kiswahili.. ila katika kiwango cha vyuo vikuu kuna, kiswahili hufundishwa hapa misri katika viyuo vitatu, cha ain shams , cha alazhar, cha kairo, ni majina ya vyuo kikuu hapa misri.. ila katika shuleni kuna hufundishwa lugha nyingi kama kiingereza na kijerumani na kifaransa na kitaliano na kispania

MIMIMALENGA-Ipi changamoto gani mnazokutana nazo wakati mkendeleza lugha ya kiswahili katika kufundisha kiswahili ?

MOHAMEDI-Changamoto.. changamoto, nadhani changamoto pekee sana hivi ni ya vitabu, vipo vitabu ila vitabu vya kisasa vya kufundisha lugha ( kozi ) kama vitabu vya kijerumani na kiingereza, ila viko vingi na nilipata vingi sana nilipokuwa kule Tanzania.
kwa maoni na ushairi wasiliana nami kwa simu namba +255624010160 au barua pepe ya iddyallyninga@gmail.com
 
Takwimu njema sana,na inaonekana kuwa wasiokuwa waswahili ndio wanaokipenda zaidi kiswahili kuliko sisi,na ishara njema kuwa kiswahili kinasambaa duniani
 
Kumbukumbu za Chuo kikuu huria cha Tanzania zinaonyesha kuwa asilimia kubwa ya masters na PhD za kiswahili zinazotolewa pale wanaopata wengi ni wanafunzi kutoka Libya .hii inaonyesha ni namna gani kiswahili kinakuwa
Nadhani hawasomi tu kama sisi hiyo kwao ni strategy
refer sababu kuu ya kuanzishwa NGOs Europe na Amerika 1900's
 
Kama Mrisho alienda kuiwakilisha Kenya kama nchi inayoongea kiswahili sembuse huyo mmisri?
 
Takwimu njema sana,na inaonekana kuwa wasiokuwa waswahili ndio wanaokipenda zaidi kiswahili kuliko sisi,na ishara njema kuwa kiswahili kinasambaa duniani
Tatizo BAKITA haitoi walimu wa Kiswahili kwenda kufunza nchi za nje ilhali Tz kuna walimu wengi wa Kiswahili wanaohitaji kufunza nje ya nchi. Tatizo li wapi ndugu Ninga?
 
Kama Mrisho alienda kuiwakilisha Kenya kama nchi inayoongea kiswahili sembuse huyo mmisri?

Kumbuka yeye ni muarab na siyo wa asili ya kiswahili,yeye kufundisha kiswahili ni ishara ya kuku kwa kiswahili katika mataifa mengine.
Mtanzania ni wajibu wake kufundisha kiswahili nje lakini si ajabu kwa kuwa hiyo ni lugha yake
Hiyo ndio tofauti .

Ajabu ni mtanzania kushindwa kufundisha kiswahili na asiye mtanzania kufundisha kiswahili
 
Tatizo BAKITA haitoi walimu wa Kiswahili kwenda kufunza nchi za nje ilhali Tz kuna walimu wengi wa Kiswahili wanaohitaji kufunza nje ya nchi. Tatizo li wapi ndugu Ninga?
Labda bado thamani ya kiswahili inaonekana kuwa ni ndogo sana na ndio maana hata sisi wenyewe sasa hivi tunajikita sana katika kuamini lugha za kigenikuliko kugha yetu
chukulia mfano leo,mtu anezungumza kingereza ndie anaeonekana kuwa msomi na yule asofahamu kingereza ndie anaedharaulika
 
Labda bado thamani ya kiswahili inaonekana kuwa ni ndogo sana na ndio maana hata sisi wenyewe sasa hivi tunajikita sana katika kuamini lugha za kigenikuliko kugha yetu
chukulia mfano leo,mtu anezungumza kingereza ndie anaeonekana kuwa msomi na yule asofahamu kingereza ndie anaedharaulika
Inatia uchungu sana. Ngoja tuone awamu ya tano italeta mageuzi gani ktk hii lugha aali ya Kiswahili.
 
KUMBUKA YEYE NI MUARAB NA SIYO WA ASILI YA KISWAHILI,YEYE KUFUNDISHA KISWAHILI NI ISHARA YA KUKU KWA KISWAHILI KATIKA MATAIFA MENGINE.
MTANZANIA NI WAJIBU WAKE KUFUNDISHA KISWAHILI NJE LAKINI SI AJABU KWA KUWA HIYO NI LUGHA YAKE
HIYO NDIO TOFAUTI .
AJABU NI MTANZANIA KUSHINDWA KUFUNDISHA KISWAHILI NA ASIYE MTANZANIA KUFUNDISHA KISWAHILI
Sioni la ajabu hapo. Kuzungumza lugha fulani haina maana ya kuwa unaweza kufundisha lugha hiyo. Kuna Wabongo nawajua wako Marekani wakifunza Kiingereza katika vyuo vikuu.
 
Sioni la ajabu hapo. Kuzungumza lugha fulani haina maana ya kuwa unaweza kufundisha lugha hiyo. Kuna Wabongo nawajua wako Marekani wakifunza Kiingereza katika vyuo vikuu.
ndio hakuna ajabu hapo hata kidogo ila tunazungumzia kiswahili na ukuaji wake,hata siku moja usithub utu kuzlinganisha lugha ya kiswahili na kingereza katika kusambaa kwake ni vitu vilivyoachana mbali sana.
 
Wakenya kibao wanafundisha kiswahili China vyuo vikubwa na wanakebehi watz kwa kiswahili kibovu kingereza kibovu! Tubaki tu kupambana na hali zetu! Tuna uzalendo wa redio
 
Wakenya kibao wanafundisha kiswahili China vyuo vikubwa na wanakebehi watz kwa kiswahili kibovu kingereza kibovu! Tubaki tu kupambana na hali zetu! Tuna uzalendo wa redio
ndio hakuna ajabu hapo hata kidogo ila tunazungumzia kiswahili na ukuaji wake,hata siku moja usithub utu kuzlinganisha lugha ya kiswahili na kingereza katika kusambaa kwake ni vitu vilivyoachana mbali sana.
Toa sababu za kutolinganisha katika suala tunalolizungumzia.
 
Toa sababu za kutolinganisha katika suala tunalolizungumzia.
ukienda kuomba kazi katika usaili mkubwa unafanyika kwa lugha gani ?
iwapo wewe ni msomi mwenye degree na ukafeli kuongea kingereza mbele za watu,hao watu wanakuchukuliaje ?
lugha ya kibiashara ni ipi ?
ni viongozi wangapi duniani wanaongea kiswahili angalau kwa ufasaha kidogo ?
kwanini kila uchaguzi wa bunge la Afrika mashariki,wagombea huomba kura kwa kingereza ?
unakumbuka kwanini yule mbunge alipokosea kingereza watu walimcheka ?
unakumbuka yule kiongozi alipokosea kingereza wanajamii walimcheka ?
hebu tafakari kwanini elimu ya chuo kikuu ukiacha kiswahili inatolewa kwa kingereza ?
hauwezi linganisha upanukaji wa lugha ya kiswahili na kingereza.
pia nashangaa sana,wewe katika uzi huu shida yako ipo wapi ?
 
Back
Top Bottom