Raia wa kawaida nitafunguaje kesi dhidi ya mtu anayevunja Katiba ya Tanzania?

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,203
23,020
Ni swali ambalo frankly speaking sina jawabu lake la moja kwa moja.

Wabobezi wetu wa masuala ya Constitutional Law watusaidie. Alternatively, kama kuna uzi wowote humu jamvini unaotoa mwongozo katika hili please share.

Mimi na wenzangu kadhaa tumedhamiria kwa dhati kabisa kufungua kesi dhidi ya mmoja wa wakuu wa mihimili yetu mitatu ambaye ameamua kwa makusudi kabisa (yeah, ni kwa makusudi kwa sababu anajua kuwa anakiuka katiba lakini he doesn't give a s**t). Kwa mawazo yake, I think, anaamini hakuna mtu yeyote mahali popote wakati wowote atakayeweza kumfanya chochote nchi hii.

Najua kuna watu watasema "mtafungua kesi katika mahakama zipi, hizi hizi za kibongo au?". Hilo lisikusumbue - tuachie sisi tuliodhamiria kufungua kesi hii muhimu sana.

We mean business this time!
 
Inawezekana kufungua kesi mahakama kuu kwa hilo suala lako, huko ndiko utapata maelekezo, kwasababu kesi za aina hiyo mara nyingi zimeshapelekwa mahakamani zikatolewa maamuzi.
 
Kuna kipengele kwenye Katiba ya JMT kinazungumzia hayo mambo ngoja nikitafute.
I wonder kwa nini hakitumiki ilihali tunao manguli wengi tu wa sheria nchi hii wakiwemo TLS.

That's why sisi kina maamuma (laymen) tunalazimika kuingia ndani ya game fasta!
 
Wakuu wa mihimili yote mitatu wamejiwekea kinga ya kutoshtakiwa, labda kama ni mauwaji wasipokuwa kazini.
 
Lakini jamaa ana kinga ya kutokushtakiwa pale anapotekeleza majukumu yake ya kibunge.
 
Kama anaona hawezi kuguswa inamaa hata huko mahakamani atashinda na itakuwa shida zaidi kwenu.

Hebu vaa 'kofia ya kitaa', najua utapata jibu tu!
 
Lakini jamaa ana kinga ya kutokushtakiwa pale anapotekeleza majukumu yake ya kibunge.
alipomchapa bakora hadharani mpinzani wake kisiasa alikuwa na kinga gani? kesi ya jinai ile siku anaacha uspika anarudi uraiani tunapekua faili lake.
 
I wonder kwa nini hakitumiki ilihali tunao manguli wengi tu wa sheria nchi hii wakiwemo TLS.
That's why sisi kina maamuma (laymen) tunalazimika kuingia ndani ya game fasta!
Sorry, hicho kipengele kinahusu interpretation ya sheria Special Constitutional Court Article 126 mambo ya muungano kati ya Bara na Visiwani, sio mambo ya Bara peke yake kama unavyotaka.
 
Ndugai atengwe na watanzania wote - ni mvunjaji mkuu wa katiba katika historia ya nchi yetu.
 
Tunaongelea suala nyeti la uvunjaji wa katiba but uzi umepooooaa. Anyways.

Nishagundua ndiyo maana Watanzania tutaendelea kukanyagwakanyagwa na kusulubishwa na walio madarakani.

Hatupendi kabisa kujihusisha na approaches zenye suluhisho linalolenga kuondoa mizizi (root causes) ya matizo yetu.

Tunapenda zaidi kuzodoana na kuparurana kama wanachama wa vicoba.

Kwa mentality hii, nchi hii hawa wahafidhina wa CCM watatutawala milele!
 
Back
Top Bottom