Raia wa Colombia aachiwa huru baada ya kukaa gerezani kwa kesi ya dawa za kulevya kwa miaka nane Tanzania

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,213
24,076
Bogotá Colombia 13 OCT 2022
Dar es Salaam 13 Oct 2022

Raia wa Colombia hatimaye ataachiwa baada ya plea bargain US$ 25,000 baada ya kusota katika gereza jijini Dar es Salaam kwa miaka nane tangu mwezi Julai mwaka 2014 hadi mwezi October 2022.

Ndugu na jamaa zake waliendesha kampeni kubwa juu twitter juu ya 'kuonewa' kwa Andres Filipe Ballesteros kufunguliwa kesi asiyoijua, lakini upande wa kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya walikuwa na ushahidi wa kutosha usio na shaka kuhusu Andres Filipe Ballesteros.

Maandamano ya wabeba mapango nchini Colombia yakiichagiza serikali yao imuokoe kutoka gerezani Tanzania yalipamba moto na wizara husika nchini Colombia kuanza kuanzisha mazungumzo na ofisi ya mundesha mashtaka Tanzania ili kujua ukweli.

Maafisa wa wizara ya sheria Colombia waliweza kufungua channeli za kidiplomasia kuwasilisha US$25,000 sawa na TShs. 50,000,000 kwa vyombo vya sheria Tanzania kuwezesha kumtoa gerezani Andres Filipe Ballesteros arudi nyumbani kwao Colombia .

1672075382381.png


Andres Filipe Ballesteros Uribe alikamatwa mwaka 2014 nchini Tanzania ktk kiwanja cha ndege cha kimataifa cha JNIA jijini Dar es Salaam Tanzania akiwa ameficha madawa katika mvunguko wa suruali kiunoni na pia ktk mkanda aliovaa.

TOKA MAKTABA :
JULY 2014

RAIA WA COLOMBIA AKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA​




Mkuu wa Kikosi cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa akionesha Cocaine zilizokuwa zimefichwa katika mkanda wa suruali aliyokuwa amevaa raia wa Colombia, Andres Filipe Ballesteros Uribe (28), mara baada ya kukamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Alianza safari yake Julai 2014 nchini Columbia, kupitia Addis Ababa kuja Tanzania huku akibainisha kwamba hiyo ni njia mpya ya usafirishaji wa dawa hizo haramu.

“Hawa jamaa wanajaribu kubuni mbinu mpya kama huyu kijana alikuwa amefunga unga wa cocaine kama zilivyokuwa zikifungwa pipi na akazimeza… mpaka sasa ameshatoa pipi 13 kwa njia ya haja kubwa na anaendelea kutoa.



Source: W Radio Colombia
 
Jamaa alifanikiwa kuuhadaa umma wa Colombia kuwa hakukamatwa na mzigo na hivyo maadamano makubwa kutaka aachiwe mara moja jijini Bogota Colombia yalipamba moto.


21 October 2022
Bogota, Colombia


Andres Filipe Ballesteros Uribe akiwa amewasili mtuhuru Bogota Colombia akiongea Kiswahili na kutoa salaam za shukrani mbele ya wazazi na jamaa waliowezesha kuachiwa huru



This 36-year-old compatriot was deprived of his freedom in a jail in Africa and his family had to pay a fine of Colombian $120 million(pesos) .
Source : el Tiempo
 
14 October 2022

JAMAA NA MARAFIKI HAWAKUAMINI KAMA US$25,000 ZA PLEA BARGAIN ZITAWEZESHA AWE HURU WALIAMINI WAMEPIGWA


Watu wa karibu wa Andres Filipe Ballesteros Uribe waliowezesha fedha za faini ya kukubali mashtaka zitaliwa na watu walio katika mfumo wa nchi hii ya Afrika walishakata tamaa jamaa yao ataozea jela miaka mingi.

Hapo ilikuwa tarehe 14 October 2022 wakati wakizungumza kesi hii katika kituo tajwa cha television ya Columbia kuhusu wamepigwa hizo fedha za faini au la.

Wajamaa zake waliamini 'ametekwa' na kundi la maharamia nchini Tanzania katika bara la Afrika
 
Kwani alikwisha hukumiwa? Inadaiwa kakamatwa na ushahidi kamili, nini sababu ya kesi kushindwa kuendeshwa na kufikia hukumu?

Swali zuri na ndiyo maana kunasababisha minong'ono na uvumi kesi isiposikilizwa katika muda muafaka kisheria huku ushaidi upo.
 
Kama mtu alikanatwa na unga miaka yote hiyo kwanini hukumu yake haikutekelezwa
Changamoto inakujaga kwenye kidhibiti,je kidhibiti muda wote ulikuwepo...
Ndomana nchi za wenzetu ukikamatwa na madawa kesi huenda chapchap?

Ova
 
21 December 2022

MADAWA YA KULEVYA (HEROIN KILO 584.55, TANI 2 ZA BANGI) ZATEKETEZWA DAR ES SALAAM, TANZANIA


Source: wasafi media

2019
9 October 2019
MAMLAKA YA KUDHIBITI NA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA NCHINI TANZANIA KUSHIRIKIANA NA MAHAKAMA, JESHI LA POLISI, IDARA YA USALAMA WA TAIFA , MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERILIKALI NA BARAZA LA TAIFA LA MAZINGIRA WAMETEKEZA KILO 120.91 ZA MADAWA YA KULEVYA AMBAPO ZOEZI HILO LIMEFANYIKA KATIKA KIWANDA CHA TWIGA CEMENT WAZO HILL, TEGETA JIJINI DAR ES SALAAM.



Source : Nassari TV
 
Back
Top Bottom