Raia wa China wakamatwa kwa kumcharaza viboko mfanyakazi aliyefika ofisini kwa kuchelewa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
b61c155e624bb9c86272eb6dbefeb0c5

Raia wanne wa Uchina wamekamatwa na polisi baada ya video kusambaa katika mitandao ya kijamii ikiwaonesha wakimchapa viboko Mkenya.

Inasemekana kwamba Wchina hao wafanyakazi wa mgahawa mmoja uliopo jijini Nairobi, alinaswa akimchapa mfanyakazi Raia wa Kenya kupitia kamera kwa madai ya kufika kazini akiwa amechelewa.

Jumapili, Mkurugenzi wa Idara ya upelelezi wa makosa ya jinai (DCI) amesema watu wanne raia wa Uchina wamekamatwa baada ya kuripotiwa kuwa mfanyakazi mmoja wa kenya ameshambuliwa.

Idara ya upelelezi wa makosa ya jinai Kenya kupitia mtandao wa Twitter imeandika,

”Baada ya taarifa katika baadhi ya vyombo vya habari zinazomuonesha mwanamume mwenye asili ya Asia akimshambulia mwanamume mmoja ambaye inasemekana ni mfanyakazi wa hoteli hiyo, asubuhi ya leo wapelelezi wamefika katika hoteli ya Chez Wou eneo la Kileleshwa kuchunga kisa hicho.”

Wapelelezi wa DCI walifanikiwa kumkamata mshukiwa Deng Hailan, raia wa uchina anayefanyakazi katika hoteli hiyo kama mpishi mkuu lakini hana kibali cha kufanyakazi Kenya.

Wengine waliokamatwa ni raia watatu wa Uchina wanaofanya kazi katika mgahawa huo kwa mahojiano zaidi lakini pia inadaiwa kwamba kuna baadhi yao hawana vibali vya kufanya kazi Kenya ama wameingia kwa visa za utalii.

Pia miongoni mwa waliokamatwa ni Yu Ling, keshia katika hoteli hiyo ambaye ana visa ya utalii lakini hana kibali cha kufanyakazi.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya video kusambaa katika mitandao ya kijamii inayomuonesha raia mwenye asili ya Asia akimchapa viboko mhudumu wa hoteli moja raia wa Kenya katika mgahawa wa Chez Wou uliopo eneo la Kileleshwa, Nairobi wiki iliyopita.

Raia wa kenya wameonesha hasira zao na kudai hatua ya kisheria ichukuliwe.

Aidha, ubalozi wa Uchina Nairobi, umeonekana kuunga mkono hatua iliyochukuliwa na serikali ya Kenya baada ya kuashiria kwamba wameona video ya kuchapwa viboko kwa raia wa Kenya iliyowekwa katika mtandao na runinga ya K24, na kuandika ujumbe ufuatao kupitia mtandao wake wa Twitter.

Jumapili, polisi walivamia hoteli hiyo na kuwakamata wafanyakazi wanane raia wa kenya na raia wanne wa Uchina kwa mahojiano. Inasemekana kwamba mtu aliyeshukiwa kutekeleza kisa hicho alitakiwa kufika kwenye ofisi za uhamiaji lakini hakufanya hivyo.
 
Kenyans! Kenyans! Are you in Africa or part of those provinces in PRC? Shame on you Kenyans. This is my anger over you for allowing such stupidity flourish in an African state.

There was a Chines, a motorcycle seller who disgraced the President. Then some whites closing a road, a no go road for Kenyans. The other time we had a similar discussion over here, comparatively presenting this behaviour of over appreciation of white-skinned in Kenya. They do enjoy excessive immunity over Africans.

The land is still a property of foreign people. While the young Nation like South Africa is rising to reclaim their land, Kenyans are going down, down to this level! I am writing in pain seeing this situation in an African free state. No other reason than that behaviour of everyone wishing to live like Europeans, Americans or anyone by all means. This is, now the results.

Very very sorry!
 
Kenyans! Kenyans! Are you in Africa or part of those provinces in PRC? Shame on you Kenyans. This is my anger over you for allowing such stupidity flourish in ana african state.

There was a Chines, a motorcycle seller who disgraced the President. Then some whites closing a road, a no go road for Kenyans. The other time we had a similar discussion over here, comparatively presenting this behaviour of over appreciation of white-skinned in Kenya. They do enjoy excessive immunity over Africans.

The land is still a property of foreign people. While the young Nation like South Africa is rising to reclaim their land, Kenyans are going down, down to this level! I am writing in pain seeing this situation in an African free state. No other reason than that behaviour of everyone wishing to live like Europeans, Americans or anyone by all means. This is, now the results.

Very very sorry!

Nimeshindwa kusoma uharo wote huu, umeambiwa jamaa wamekamatwa wote waliokuwemo na wasiokuwemo ili kusaidia kwenye uchunguzi, ulitegemea nini kingine kifanywe, wachinjwe au vipi.
Kwa nchi inayofuata utawala wa sheria, kwa tukio la mtu mmoja kumjeruhi mwenzake, hatua za kisheria huchukuliwa kwa mtuhumiwa kukamatwa na kuwaslishwa mahakamani na ndio kilichofanyika hapa.
Uchunguzi utafanywa na kubaini nini haswa kilitendeka, maana mwenye hoteli naye ametoa tamko kwamba hao wawili walikua wanacheza kamari, kwamba wakawekeana dau la shilingi 300, kwamba huyo jamaa anaweza akastahimili viboko, na ndio maana wanaonekana wanacheka cheka, ukitazama kwenye video mwanzo mwanzo kabla ya kiboko, huyo Mkenya anaonekana ni kama anamthubutu Mchina.
Kwa kifupi kitaeleweka baada ya hatua za kisheria kukamilika ili haki itendeke bila uonevu.
Ubalozi wa China pia umetolea tamko hili suala, inaonyesha limechukuliwa kwa uzito gani.
 
MK254,
Kama huwezi kusoma unajadili yote haya kwa nini? Kwani ni mara ya kwanza Wachina kuwadhalilisha? Unategemea sheria imtie hatiani mtu munayechapana viboko nyumbani? si ndiyo hayo sasa inaandikwa ni kamali,
 
Wawarudishe uchina haraka nawao wakachapwe na kupambana na Corona Virus...
 
MK254,
Kama huwezi kusoma unajadili yote haya kwa nini? Kwani ni mara ya kwanza Wachina kuwadhalilisha? Unategemea sheria imtie hatiani mtu munayechapana viboko nyumbani? si ndiyo hayo sasa inaandikwa ni kamali,

Umefanya busara kuhariri na kutoa yale matusi, nilikuambia hatuwezi tukawachinja, lazima sheria ichukue mkondo wake, jamaa amekamatwa na kuwasilishwa mahakamani, taratibu zinafuatwa za kuhakikisha haki inatendeka bila uonevu.
 
Wahindi pamoja na ukuda wao wote kwa wafanyakazi wao weusi lakini ni nadra sana kufanya hizi grave mistakes ili waangukie mikononi mwa polisi.
 
Jirani mwanaume shababi kabisa umenining'iniza pumbu unakubali kulala chini kisha kutandikwa kaa mtoto wa shule? Speaking of Them Fags…
Nimeshindwa kusoma uharo wote huu, umeambiwa jamaa wamekamatwa wote waliokuwemo na wasiokuwemo ili kusaidia kwenye uchunguzi, ulitegemea nini kingine kifanywe, wachinjwe au vipi.
Kwa nchi inayofuata utawala wa sheria, kwa tukio la mtu mmoja kumjeruhi mwenzake, hatua za kisheria huchukuliwa kwa mtuhumiwa kukamatwa na kuwaslishwa mahakamani na ndio kilichofanyika hapa.
Uchunguzi utafanywa na kubaini nini haswa kilitendeka, maana mwenye hoteli naye ametoa tamko kwamba hao wawili walikua wanacheza kamari, kwamba wakawekeana dau la shilingi 300, kwamba huyo jamaa anaweza akastahimili viboko, na ndio maana wanaonekana wanacheka cheka, ukitazama kwenye video mwanzo mwanzo kabla ya kiboko, huyo Mkenya anaonekana ni kama anamthubutu Mchina.
Kwa kifupi kitaeleweka baada ya hatua za kisheria kukamilika ili haki itendeke bila uonevu.
Ubalozi wa China pia umetolea tamko hili suala, inaonyesha limechukuliwa kwa uzito gani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom