Raia wa China kizimbani kwa nyara za mamilioni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Raia wa China kizimbani kwa nyara za mamilioni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 10, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  RAIA wa China, Li Guibang (42) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka matano likiwemo la kusafirisha nyara za serikali zenye thamani ya Sh milioni 165.5.

  Akisoma mashitaka mbele ya Hakimu Augustina Mmbando, Wakili wa Serikali, Zuberi Mkakati alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo mwaka juzi Dar es Salaam na Zanzibar.

  Katika shitaka la kwanza, ilidaiwa kati ya Juni 19 na Agosti 21 mwaka juzi, mshitakiwa alikamatwa akiwa na kilo 2,005.6 za pembe za ndovu zenye thamani ya Sh milioni 165.5 bila kuwa na leseni.

  Ilidaiwa katika shitaka la pili kuwa kati ya Mei 9 na Juni 9 mwaka juzi, mshitakiwa alikamatwa akisafirisha nyara hizo kinyume cha sheria kwenda kwenye kampuni ya Hong Kong Investment and Trading iliyopo Vietnam.

  Ilidaiwa pia kuwa mshitakiwa alisafirisha nyara hizo kwenda kwenye kampuni ya Hai Phong Investment bila ya kuwa na kibali.

  Wakili Mkakati alidai kuwa katika shitaka la nne mshitakiwa alisafirisha na kuuza nyara za serikali nje ya nchi bila kuwa na kibali.

  Mshitakiwa hakuruhusiwa kujibu mashitaka kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo na kurudishwa rumande hadi Januari 24 mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena.
   
Loading...