Raia wa China Kizimbani kwa kutaka kumpa rushwa Mkuu wa mkoa wa Geita

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,438
3,333
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Geita imemfikisha mahakamani raia wa China kwa kosa la kumshawishi mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel ili ampe rushwa ya Sh1milioni.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Ijumaa Desemba 7, 2018 na Mkuu wa taasisi hiyo mkoani Geita, Thobias Ndaro inasema mshtakiwa huyo, Cheng Li ni mfanyabiashara wa madini.

Inaeleza kuwa alifikishwa mahakamani jana Novemba 6, 2018 mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya Hakimu Mkazi Geita, Jovith Kato.

Akisoma mashtaka mwendesha mashtaka wa Takukuru, Dennis Lekayo amedai mahakamani hapo kuwa Oktoba na Novemba, 2018 mshtakiwa alimshawishi Gabriel kwa njia ya ujumbe wa simu akitaka kumpatia Sh1milioni kila mwezi.

Ilielezwa mahakamani hapo kuwa katika kuonyesha amedhamiria kutoa rushwa alituma ujumbe mwingine akimshawishi kumpelekea kiasi hicho cha fedha na majani ya chai kutoka China.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa baada ya ujumbe huo, mkuu huyo wa mkoa alitoa taarifa Takukuru ambao waliweka mtego uliofanikisha kumkamata mshtakiwa akiwa ofisini kwa Gabriel akijiandaa kutoa rushwa ya Sh1milioni na majani hayo ya chai.

Mshtakiwa amekwama makosa na yuko nje kwa dhamana huku kesi hiyo ikiahirishwa hadi Desemba 20, 2018.
 
Kweli wachina ni maskini,Mkuu wa mkoa vs Majani ya chai hahah.


Siyo masikini, ni kwamba wametusoma wametujua kulikotunavyojijua, wanatuona ngedere tu, hiyo ni dalili kuwa kuna watendaji wanavipokea hivyo na huo ni mwendelezo tu, jiulize swali, mtanzania anaweza kudiriki kutoa rushwa China!? Seriousness katika mambo ya msingi haipo hapa kwetu, kama sheria zingekuwa kali huyo mchina asingethubutu hata kufikiria kutoa hiyo rushwa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom