Raia wa China Kizimbani kwa kutaka kumpa rushwa Mkuu wa mkoa wa Geita


Influenza

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Messages
226
Likes
280
Points
80
Influenza

Influenza

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2018
226 280 80
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Geita imemfikisha mahakamani raia wa China kwa kosa la kumshawishi mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel ili ampe rushwa ya Sh1milioni.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Ijumaa Desemba 7, 2018 na Mkuu wa taasisi hiyo mkoani Geita, Thobias Ndaro inasema mshtakiwa huyo, Cheng Li ni mfanyabiashara wa madini.

Inaeleza kuwa alifikishwa mahakamani jana Novemba 6, 2018 mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya Hakimu Mkazi Geita, Jovith Kato.

Akisoma mashtaka mwendesha mashtaka wa Takukuru, Dennis Lekayo amedai mahakamani hapo kuwa Oktoba na Novemba, 2018 mshtakiwa alimshawishi Gabriel kwa njia ya ujumbe wa simu akitaka kumpatia Sh1milioni kila mwezi.

Ilielezwa mahakamani hapo kuwa katika kuonyesha amedhamiria kutoa rushwa alituma ujumbe mwingine akimshawishi kumpelekea kiasi hicho cha fedha na majani ya chai kutoka China.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa baada ya ujumbe huo, mkuu huyo wa mkoa alitoa taarifa Takukuru ambao waliweka mtego uliofanikisha kumkamata mshtakiwa akiwa ofisini kwa Gabriel akijiandaa kutoa rushwa ya Sh1milioni na majani hayo ya chai.

Mshtakiwa amekwama makosa na yuko nje kwa dhamana huku kesi hiyo ikiahirishwa hadi Desemba 20, 2018.
 
B

BEHOLD

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2013
Messages
3,073
Likes
4,809
Points
280
B

BEHOLD

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2013
3,073 4,809 280
Huyo raia naye rushwa gani hiyo? Shs 1M!
Watu wanatuma kontena 20 zenye mali siku hizi
 
Sir Khan

Sir Khan

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2018
Messages
2,794
Likes
3,567
Points
280
Sir Khan

Sir Khan

JF-Expert Member
Joined Jul 28, 2018
2,794 3,567 280
S.U.K.U.M.A N.D.A.N.I
 
Capt Tamar

Capt Tamar

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2011
Messages
8,457
Likes
6,003
Points
280
Capt Tamar

Capt Tamar

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2011
8,457 6,003 280
Afungwe miaka 40 tu!! Anamuhonga Rais wa wilaya majani ya chai?tena ya kichina? Si dharau kwa watanzania hii? Tena muongezeeni na mitano kwa kosa la kuleta mazarau kazini!! Nguruwe kabisa!
 
Chapa Nalo Jr

Chapa Nalo Jr

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2010
Messages
6,641
Likes
3,600
Points
280
Chapa Nalo Jr

Chapa Nalo Jr

JF-Expert Member
Joined Dec 8, 2010
6,641 3,600 280
Hata mimi ninge mripoti, kihela gani hicho, hiyo ni hela ya watendaji wa vijiji

Huyo RC naye mnafiki tu, ingekuwa hela ya maana hata shetani asingepewa taarifa
 
henry kilenga

henry kilenga

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Messages
796
Likes
501
Points
180
henry kilenga

henry kilenga

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2015
796 501 180
Ufipa watasema asamehewe maana anatangaza utalii
 
KingY

KingY

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2018
Messages
3,072
Likes
4,477
Points
280
KingY

KingY

JF-Expert Member
Joined May 22, 2018
3,072 4,477 280
hii ni dharau rushwa ya 1m. na majani ya chai hahahaha bora mkuu amechomoa. yaani kamdharirisha sana majani ya chai bora hata angemuhonga suti
huyu ni boya kweli kweli
 
zipompa

zipompa

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2014
Messages
4,253
Likes
7,280
Points
280
zipompa

zipompa

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2014
4,253 7,280 280
= kamdhalilisha

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
we shule ulienda kusomea kurekebisha makosa ya kimaandishi na si kufikiria ki mantiki.

kukosoa una 100% ila kufikiri ki akili una 3%
 
mng'ato

mng'ato

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2014
Messages
11,300
Likes
10,551
Points
280
mng'ato

mng'ato

JF-Expert Member
Joined Oct 27, 2014
11,300 10,551 280
Hata mimi ninge mripoti, kihela gani hicho, hiyo ni hela ya watendaji wa vijiji

Huyo RC naye mnafiki tu, ingekuwa hela ya maana hata shetani asingepewa taarifa
Kuna yule jamaa alimhonga Lukuvi akapelekwa mahakamani sijui aliishia wapi.
 
marxlups

marxlups

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Messages
10,123
Likes
4,606
Points
280
marxlups

marxlups

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2011
10,123 4,606 280
Kweli wachina ni maskini,Mkuu wa mkoa vs Majani ya chai hahah.

Siyo masikini, ni kwamba wametusoma wametujua kulikotunavyojijua, wanatuona ngedere tu, hiyo ni dalili kuwa kuna watendaji wanavipokea hivyo na huo ni mwendelezo tu, jiulize swali, mtanzania anaweza kudiriki kutoa rushwa China!? Seriousness katika mambo ya msingi haipo hapa kwetu, kama sheria zingekuwa kali huyo mchina asingethubutu hata kufikiria kutoa hiyo rushwa.
 

Forum statistics

Threads 1,237,176
Members 475,465
Posts 29,280,395