Raia Mwema: Wanawake 40 wajitokeza TAKUKURU kutoa ushahidi wa unyanyasaji wa kingono na ubakaji wa Ole Sabaya

Dogo mshamba sana kwanza hajui biashara wenzake wanaunda kampuni za kijanja sio kwa majina yao halafu wanahakikisha kampuni zinapata zabuni na kuhakikisha zinalipwa kwa wakati ndio business zinasonga yeye anavuruga biashara za watu kizembe
 
Mwenyezi Mungu fundi sana. Bila kumchukua yule dhalimu huyo mhuni Sabaya angeendelea na dhuluma na udhalimu wake kwa miaka mingi sana.
Moja kati ya tuhuma zinazomkabili aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ni unyanyasaji wa kingono. Sabaya anadaiwa kulazimisha ngono wanawake mbalimbali, kuwachukua kwa nguvu anapokutana nao kwenye klabu za usiku, na kuwapeleka hotelini kufanya nao ngono kwa lazima. Jumla ya wanawake 40 wamejitokeza kutoa ushahidi, limeripoti gazeti la Raia Mwema.

Kati ya wanawake hao wapo wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu katika mikoa ya Arusha na Kilimnjaro. Kati ya wanafunzi hao wawili wanadai kulawitiwa baada ya kutekwa na walinzi wa Sabaya walipokutana nae night club. Mmoja kati ya walinzi amekiri kuwapeleka wasichana hao kwa Sabaya lakini amekanusha tuhuma za ulawiti.

"Tuliagizwa kuwachukua lakini sikujua mahusiano yao na Mhe.Sabaya wala sikujua kama walikubaliana kukutana. Nakiri kuwapeleka kwake lakini kuhusu kulawiti siwezi kutoa ushahidi maana sikuwa naye ndani" mmoja wa walinzi wa Sabaya ameieleza timu maalumu (task force) inayochunguza suala hilo kwa kushirikiana na TAKUKURU.

Sabaya anadaiwa kufanya vitendo hivyo katika hoteli mbalimbali za kifahari jijini Arusha na amekuwa akiondoka bila kulipa. Baadhi ya hoteli zimekiri kumdai Sabaya baada ya kupata huduma mbalimbali ikiwemo malazi na chakula lakini amekua akindoka bila kulipa. CG Hotel wanamdai 8.7M, Grand Melia 14.8M, Marves Hotel 3.4M, na Massai Land 9M.

Sabaya ambaye yupo mahabusu tangu May 25 mwaka huu, anatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote ikiwa ataonekana ana kesi ya kujibu.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP Salum Hamduni jana alisema "Ni kweli tunamshikilia tangu jumanne ya wiki iliyopita kwa mahojiano ya tuhuma mbalimbali za matumizi mabaya ya madaraka na rushwa. Akionekana ana kesi ya kujibu atafikishwa mahakamani"

My Take
Chanzo cha haya yote ni John Magufuli. Yeye alidhani anamkomoa Mbowe kumbe anagongewa watanzania wanyonge
 
Watu wa Arusha wanamfahamu vyema Sabaya. Alipokuwa mwenyekiti tu wa UVCCM Arusha watu walinyooka.
Yeye kuingia hotelini na demu halafu asilipe ni kitu cha kawaida. Aliwadhulumu kwerii kwerii wenye mahotel.
Ukimdai anatoa kitambulisho cha TISS kuwa yeye ni UNDERCOVER.
 
"Moja kati ya tuhuma zinazomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ni unyanyasaji wa kingono. Sabaya anadaiwa kulazimisha ngono wanawake mbalimbali, kuwachukua kwa nguvu anapokutana nao kwenye klabu za usiku, na kuwapeleka hotelini kufanya nao ngono kwa lazima. Jumla ya wanawake 40 wamejitokeza kutoa ushahidi TAKUKURU.

Kati ya wanawake hao wapo wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu katika mikoa ya Arusha na Kilimnjaro. Kati ya wanafunzi hao wawili wanadai kulawitiwa baada ya kutekwa na walinzi wa Sabaya walipokutana nae night club. Mmoja kati ya walinzi amekiri kuwapeleka wasichana hao kwa Sabaya lakini amekanusha tuhuma za ulawiti.

"Tuliagizwa kuwachukua lakini sikujua mahusiano yao na Mhe.Sabaya wala sikujua kama walikubaliana kukutana. Nakiri kuwapeleka kwake lakini kuhusu kulawiti siwezi kutoa ushahidi maana sikuwa naye ndani" mmoja wa walinzi wa Sabaya ameieleza timu maalumu (task force) inayochunguza suala hilo kwa kushirikiana na TAKUKURU.

Sabaya anadaiwa kufanya vitendo hivyo katika hoteli mbalimbali za kifahari jijini Arusha na amekuwa akiondoka bila kulipa. Baadhi ya hoteli zimekiri kumdai Sabaya baada ya kupata huduma mbalimbali ikiwemo malazi na chakula lakini amekua akindoka bila kulipa. CG Hotel wanamdai 8.7M, Grand Melia 14.8M, Melvis Hotel 3.4M, na Massai Land 9M.

Sabaya ambaye yupo mahabusu tangu May 25 mwaka huu, anatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote ikiwa ataonekana anazo tuhuma za kujibu.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP Salum Hamduni jana alisema "Ni kweli tunamshikilia tangu jumanne ya wiki iliyopita kwa mahojiano ya tuhuma mbalimbali za matumizi mabaya ya madaraka na rushwa. Akionekana ana kesi ya kujibu atafikishwa mahakamani". "

Copied and paste from Malisa GJ Facebook page

Swali langu:-
Hivi ni kweli JPM hakujua hizi tuhuma za Sabaya?

Kama alijua akakaa kimya basi na yeye si sehemu ya tatizo hili?

Asanteni sana Wakuu.
Ndiyo maana mtu kama Mimi ninayejali uadilifu na ubinadamu siwezi kushabikia yule Dictator kabisa mpaka niingie kaburini.
 
Back
Top Bottom