Raia Mwema: Wanawake 40 wajitokeza TAKUKURU kutoa ushahidi wa unyanyasaji wa kingono na ubakaji wa Ole Sabaya

Taarifa kutoka Takukuru zinaonyesha kwamba mpaka muda huu Jumla ya Wanawake 40 wakiwemo wanafunzi wa vyuo na Sekondari wamejitokeza kutoa ushahidi wa namna walivyobakwa na kufanyiwa ukatili mwingine wa Kingono na Mtukufu Ole Sabaya (namba inaweza kuongezeka).

Inadaiwa kwamba Sabaya akishalewa kwenye Bar yoyote alikuwa anang'ang'ania mwanamke yeyote aliyemtaka na kuondoka naye kwenye Hotel yoyote na kumfanyia ukatili alioutaka huku akilindwa na Polisi na Mabaunsa wake.

Tutaendelea kuwaletea uhalifu wa huyu jamaa kwa kadri unavyotufikia bila kuedit chochote .

Endelea kututegea sikio.
---

Hatari !!
 
Hapa kuna namna, wanawake 40,hapana kama pesa anayo anabakaje wanawake 40,mbona hakuna hata bwana mmoja wa mwanamke aliyelalamika, hao wanawake wanafanya nini bar mapaka wabakwe? Mwanamke kubakwa then akashitaki, wengi hujasiri huo hawana.
 
J3 anapanda kizimbani kili,j5 anapanda kizimbani manyara,then dom,dar yani atajiua kwa stress mashtaka yake yanafika buku
 
Hili tukio la Sabaya CHADEMA mmelivalia njuga, mnalifanya limekuwa kama la kisiasa sana.

CHADEMA mko desperate sana, yaani Mnavuruga kabisa
Sio kweli kama wewe unavyofikiri,pamoja na kufanya figisu Hai kuhakikisha chadema inakufa,alifanikiwa ingawa sio siasa hizo,na Siasa za maji taka.

Watanzania wote walioumizwa ndio wanaoshikia bango, kula bata tourist hotels bila kulipia kisa mkuu wa wilaya!!!!!
 
Hivi Ole Sabaya alikuwa muumini wa dini ipi? Inaonekana hakuwa na hofu ya Mungu hata chembe. Kwa kuangalia/ kusikia haya anayodaiwa kuyafanya enzi za utawala wake.
 
Hapa kuna namna, wanawake 40,hapana kama pesa anayo anabakaje wanawake 40,mbona hakuna hata bwana mmoja wa mwanamke aliyelalamika, hao wanawake wanafanya nini bar mapaka wabakwe? Mwanamke kubakwa then akashitaki, wengi hujasiri huo hawana.
Wewe mkeo akilawitiwa utajitokeza kuutangazia umma? Stupid
 
You have a brain please use it appropriately!
Hapa kuna namna, wanawake 40,hapana kama pesa anayo anabakaje wanawake 40,mbona hakuna hata bwana mmoja wa mwanamke aliyelalamika, hao wanawake wanafanya nini bar mapaka wabakwe? Mwanamke kubakwa then akashitaki, wengi hujasiri huo hawana.
 
Taarifa kutoka Takukuru zinaonyesha kwamba mpaka muda huu Jumla ya Wanawake 40 wakiwemo wanafunzi wa vyuo na Sekondari wamejitokeza kutoa ushahidi wa namna walivyobakwa na kufanyiwa ukatili mwingine wa Kingono na Mtukufu Ole Sabaya (namba inaweza kuongezeka).

Inadaiwa kwamba Sabaya akishalewa kwenye Bar yoyote alikuwa anang'ang'ania mwanamke yeyote aliyemtaka na kuondoka naye kwenye Hotel yoyote na kumfanyia ukatili alioutaka huku akilindwa na Polisi na Mabaunsa wake.

Tutaendelea kuwaletea uhalifu wa huyu jamaa kwa kadri unavyotufikia bila kuedit chochote .

Endelea kututegea sikio.
---

Inabidi hao mapolisi wote waliokuwa wanalinda huo uchafu (kama ni kweli) wachukuliwe hatua kali za kisheria. Kama wanalinda mbakaji anapobaka na wao ni wabakaji. Hatukubali waachiwe au tudanganywe danganywe.
 
Mimi sio mwanasheria, ilakama anafanya ukatili wa kijinsia kingono, akiwa amelewa, sabaya atashinda mcha kweupe manake utetezi utakuja kuwa ni akili ya pombe sio akili yake, je akiwa katika akili ambayo haina pombe huwa anabaka na kufanya ukatili wa kijinsia?
Dah kwa hii akili bro unatia huruma Sana...
 
Hatari !!
Simulizi toka Kisongo

Sehemu ya Pili...

Anasimulia John Mallya

Jumatano tarehe tisa Juni, 2021 siku takribani ya nne tangu atupwe gerezani, Lengai bado hajapata uhakika kama ameshayazoea makazi yake mapya au la!

Kuta nzito zenye machata ya wahuni waliowahi kupita zimeandikwa kwa mkaa, chaki za rangi na vitu vyenye ncha kali; milango ya nondo za kale, lakini bado imara sana, inayofunguliwa na kufungwa kwa kelele; askari jela wanaopiga doria muda wote wakiwa na bunduki aina ya AK 47; makufuli makubwa ambayo yanazuia mihangaiko isiyo na lazima ya wafungwa na mahabusu; pamoja na miongozo ya mara kwa mara inayotoka kwa Mnyampala wa selo, Abdallah Mzimbwa a.k.a Chunusi, vyote kwa pamoja, vinamkosesha raha kabisa mahabusu huyu mpya.

"Humu ndani hapazoeleki", anajiambia mwenyewe akiwa amekaa pembeni ya rafiki yake mpya Bwana Loyid Lenanu maarufu kwa jina la Masai ndani ya Gereza Kuu Arusha. Akiwa angali amekaa anakumbuka jambo lililo msikitisha, nalo ni ujumbe aliopewa na mgeni wake aliyemtemblea juzi jumapili.

Juzi yake "Visitors Day", Lengai alipata kutembelewa na mtu mmoja tu, Prisca Ole Idamat aliyekuja kumletea Malapa ya rangi nyekundu, sabuni za kuogea, taulo ambalo lilikataliwa kuingia pale mlangoni na askari Jela Surgent Paul na vilevile alimletea chakula akipendacho-mbuzi choma na ugali wa sembe, alimletea pia na ujumbe wa kusikitisha.
Lengai anaikumbuka siku ya juzi. Anakumbuka kila zawadi aliyoletewa na zaidi anakumbuka ujumbe uliopasua sehemu yote ya moyo wake uliojaa mashaka.

Taratibu anainamisha uso wake katikati ya magoti yake na anaanza kulia. Lenanu a.k.a Masai anamshika kichwani, anamkumbusha kuacha kulia. Lengai anajikaza, kwa kutumia sweta anafuta chozi lake lile la jicho moja tunalolijua wote. Anakumbuka maelekezo ya Masai.

Jumamosi asubuhi Masai alimfuata Lengai na kumpa darasa la haraka (orientation) kuhusu maisha ya gerezani:

"Kaka humu usioneshe hisia zako.Ukionekana unalia utampata wa kukubembeleza. Na ukibembelezeka inaweza kuwa mbaya sana kwako hapo badaye. Hata ukicheka basi cheka kwa kiasi. Ukicheka kwa kujiachia kuna wahuni watapenda meno yako... itakuja kuwa tabu"

..."Vilevile usipende kuogea sabuni za kunukia zinavutia mabazazi. Umenisikia kaka?", aliulizwa japo hakujibu kitu.

Anawakumbuka mabaunsa wake aliotoka nao Takukuru na baadaye mahakamani. Hawaoni ndani ya ngome kuu, lakini angalau sasa anajua walipo.

Masai amempa elimu kwamba ndani ya Gereza Kuu Arusha kuna sehemu nne: Sehemu ya kwanza mara tu unapoingia upande wa kushoto ni Gereza la wafungwa na mahabusu wa uhalifu wa kivita wa Rwanda waliohukumiwa na Mahakama ya Kimataifa iliyoshughulikia mauaji ya Kimbari ya Rwanda iliyopo Arusha. Hapo hakuna mfungwa Mtanzania! Wengi ni Wanyarwanda. Ni jela yenye magodoro na wafungwa wanakula vyema na wanapata haki ya kukutana kimwili na wenzi wao.Kwa ufupi ni jela yenye viwango vya kimataifa.Sehemu ya Pili panafahamika zaidi kama Ethiopia, mazingira yake ni ya kiwango cha Tanzania hasa. Humo ndimo walipo mabaunsa wa Lengai.Sehemu ya tatu ni Ngome Kuu ambapo ni nafuu zaidi kulinganisha na Ethiopia, na sehemu ya nne ni eneo la mahabusu na wafungwa wanawake.

Akiwa bado kwenye hali ya kukosa raha, roho yenye wasiwasi na akili inayojaribu kwa bidii kuzoea mazingira, mara Surgent Paul anamwambia anahitajika kwenye ofisi ya Mkuu wa Gereza. Kabla hajajua anaitiwa nini na Ofisi ya Mkuu wa Gereza iko upande gani, ana'amrishwa ainuke kwa sauti ya ukali. Kabla hajasimama sawa sawa anasukumwa asonge kulia.Anageuka akipepesuka; kwa siku nne mfululizo hajala akashiba, hajalala akapumzika, hajazoea mazingira, ana kiwewe, wasiwasi, mashaka na nafsi iliyojaa tabu. Anasukumwa tena aongeze mwendo na kujigonga ukutani. Anatembea akijitathimini kwa namna alivyopoteza uzito mwingi kwa siku chache. Anatikisa kichwa anasikitika.

Ni mara ya kwanza anasogelea ofisi ile. mapigo ya moyo yanaongezeka anaposogelea mlango na kuona wanaume wawili waliovalia suti nyeusi na mashati meupe. Kabla ya kuingia anapewa amri ya kuchuchumaa na anapigwa kwa nguvu begani akiwa pale chini.

"Surgent Paul ni Askari Jela shupavu na anayeonekana kutumia muda wake mwingi wa ziada kunyanyua vitu vizito", Lengai anajiambia akilini mwake akiwa pale chini.

Paul anasogelea mlango na kuomba ruhusa ya kumuingiza Lengai ofisini kwa Mkuu, lakini Msaidizi wa Mkuu anamtaka asubiri.

Mapigo ya moyo ya Lengai yamefika hatua ya kusabisha shinikizo la damu.Hali ya hewa ya baridi la saa 5 asubuhi katika msimu huu wa baridi kali imeshindwa kuzuia jasho la mwili mzima linalomtiririka kwa kasi. Anajisikia dhaifu na miguu yake inashindwa kubeba uzito wa mwili aliobaki nao.Anatamani akae chini, lakini anajua Surgent Paul atampiga mabuti. Basi anashusha mikono yake kusaidia miguu yake, na sasa amekaa mithili ya chura.

Baada ya dakika tatu wanaitwa ndani. Bila kusalimiwa anataarifiwa kuwa atatolewa nje ya magereza kwa kibali Cha mahakama kwa mahojiano zaidi na maafisa wa vyombo vya usalama.

Lengai anashusha pumzi! Anahema, wasiwasi bado haujamuisha ila sasa umebadilika! Wananipeleka wapi? kunihoji nini? Wataniongezea mashitaka? Anajiuliza moyoni na anajua hawezi pata jibu. Anapotoka kwenye lango la Gereza anafungwa pingu na kupandishwa kwenye gari lenye ulinzi madhubuti. Maswali yanazidi kupasua kichwa chake na kwa mara nyingine anakumbuka ujumbe alioletewa na Dada yake- Prisca.

Itaendelea.....

johnmallya2021
All characters in this publication are fictitious and any resemblance to real persons, living or dead is purely coincidental.
 
Back
Top Bottom