RAIA MWEMA: SIRI za Lowassa, Msekwa, nje nje... Ni kikao chao cha faragha Lumumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RAIA MWEMA: SIRI za Lowassa, Msekwa, nje nje... Ni kikao chao cha faragha Lumumba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 4, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Waandishi Wetu
  3 Aug 2011
  Toleo na 197

  [​IMG]

  • Ni kikao chao cha faragha Lumumba
  • Zawahusisha Rostam, Chenge
  • Kikwete awaokoa kiaina, sasa ‘wapumulia mashine’


  KILE kilichoelezwa kuwa kilikuwa ni siri kati ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Pius Msekwa na watuhumiwa waliotakiwa kujitoa ndani ya uongozi, zimeanikwa katika kikao cha Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu ya chama hicho (NEC) kilichowajadili mwishoni mwa wiki.
  Mbali ya kubainishwa kwa siri za kikao cha faragha kati ya Msekwa na watuhumiwa hao, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, aliipa meno zaidi Sekretarieti ya chama hicho kwa kupuuza maneno ya baadhi ya wanaosema kwamba inakivuruga chama hicho tawala.
  Watuhumiwa hao, Mbunge wa Igunga Rostam Aziz, ambaye tayari amejitoa na wenzake; Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa na Andrew Chenge ambaye ni Mbunge wa Bariadi Magharibi, walikutana na Msekwa kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam na kati yao hakuna aliyekuwa tayari kuzungumzia kilichozungumzwa.
  Ni Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Kikwete, ambaye alitoa siri hiyo katika kikao cha Kamati Kuu alipotuliza baadhi ya wajumbe wa kikao hicho cha juu cha chama hicho waliotaka watuhumiwa hao watimuliwe mara moja.

  Kikwete alitoa siri hiyo akimtuliza Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais mstaafu, Mzee John Malecela, aliyeonekana kikaoni kuanza kufanikiwa kushawishi wajumbe kushinikiza Kamati Kuu iwafukuze moja kwa moja, akina Lowassa na Chenge, kabla kikao kijacho cha Halmashauri Kuu. Kikwete awaokoa kina Lowassa
  Kwa mujibu wa mtoa taarifa wetu, Kikwete, akionekana kama kusoma nyuso za wajumbe, alieleza kuwa ni busara zaidi kusimamia uamuzi wa NEC uliowapa muda wa kujivua gamba watu hao kuwa mwisho ni kikao kijacho cha Halmashauri hiyo Kuu.
  Katika kile kinachoweza kuelezwa kuwa kufichuka kwa sehemu ya siri ya Msekwa moyoni, Kikwete alimgeukia Msekwa akiuliza; “hivi si walikwambia wanaomba muda wa kutafakari?” Naye msekwa alijibu “ndiyo”.
  Kilichokuwa kikirejewa na Kikwete katika swali lake kwa Msekwa ni kilichojadiliwa kwenye kikao kati ya Makamu huyo Mwenyekiti na Lowassa, Chenge na Rostam ambao alikutana nao kwa nyakati tofauti katika ofisi ndogo za CCM, Lumumba Dar es Salaam.
  Kwa mujibu wa maelezo hayo ya Msekwa, imebainika kuwa katika mazungumzo ya faragha, Lowassa, Chenge na Rostam walipobanwa waliomba muda zaidi wa kutafakari kabla ya muda wa mwisho waliopewa kufika.
  Katika hilo, Kikwete anatajwa kuwashawishi wajumbe kuwapa muda zaidi kama ilivyokubaliwa faragha, na wasipoamua kama mwenzao Rostam, hatua nyingine zitafuata.
  Tayari baadhi ya wajumbe walionekana kukubaliana na uamuzi wa kuwatimua wanasiasa hao wawili waliogoma kujitoa hadi sasa baada ya mwenzao Rostam Aziz kufanya ‘uamuzi mgumu’ wa kuachia nafasi zote ikiwamo ubunge, kabla ya Rais Kikwete kuokoa jahazi.
  Chenge, Lowassa bado hawajaamua
  Baada ya kimya cha muda mrefu, Chenge ameibukia mjini Dodoma akichangia bajeti ya Wizara ya Ujenzi, alipowataka wapiga kura wake kupuuza yale aliyoyaita maneno ya mitaani kumhusu, akizima tetesi za hivi karibuni kwamba alikwishajiondoa katika nafasi zake za uongozi kutekeleza maamuzi ya kikao cha NEC kilichopita.
  Kwa upande wake, Lowassa amekuwa akitoa matamshi ya chini chini kuonyesha kutokuwa tayari kujitoa; huku akiahidi kutoa tamko rasmi ‘wakati mwafaka’ utakapowadia, baadhi ya watu wakitabiri kishindo kutoka kwa mwanasiasa huyo anayetajwa sana kuwania nafasi ya urais kumrithi Kikwete mwaka 2015.
  Kikwete aipa nguvu Sekretariati mpya
  Katika kikao hicho cha CC, Rais Kikwete alirudia kuipa nguvu Sekretarieti ya chama hicho kwa kuwapinga moja kwa moja wanaoibeza wakiwamo baadhi ya wenyeviti wa mikoa ambao wamekuwa wakisema inapotosha uamuzi wa NEC.
  Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari, Rais Kikwete alitamka ndani ya kikao cha Kamati Kuu akisema; “there are some stupid guys (wajinga fulani),” wanaosema Sekretariati hiyo inakivuruga chama kwa namna wanavyosimamia utekelezaji wa uamuzi wa NEC; hasa wa kujivua gamba.
  Katika kile kinachoweza kutafsiriwa moja kwa moja kuwa ni kuwapuuza baadhi ya viongozi wanaodai kuwa Sekretariati imekuwa ikisimamia uamuzi wa kujivua gamba, kinyume cha matakwa ya Halmashauri Kuu, Kamati Kuu imeipongeza Sekretariati hiyo.
  Hatua hiyo inatajwa kuwa ni pigo kwa baadhi ya viongozi wa sasa wa chama hicho, wakiwamo wanaopaswa kujiuzulu nafasi za uongozi katika chama hicho - Chenge na Lowassa; huku Rostam naye akijiuzulu kwa kulalamikia Sekretariati hiyo akisema inaendesha siasa uchwara.
  Wengine katika orodha ya kuishambulia Sekretariati hiyo na hasa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ni John Guninita, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM-Dar es Salaam na Hamisi Mgeja Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga, wote wakitajwa kuwa karibu na viongozi wanaotakiwa kujiuzulu.
  Taarifa kutoka ndani ya kikao cha Kamati Kuu zinaeleza kuwa Rais Kikwete ni kati ya viongozi walioweka wazi msimamo wao kuhusu mwenendo wa Sekretariati, akimtaja kwa jina Nape Nnauye.

  Chanzo chetu cha habari kinamnukuu Rais Kikwete ambaye ndiye Mwenyekiti wa kikao hicho kilichotanguliwa na kikao cha Kamati ya Maadili ya Usalama, akiwaita watu wanadai kuwa Sekretariati hiyo haitekelezi uamuzi wa NEC kwa usahihi, kuwa ni wajinga fulani na kusisitiza kuwa amevutiwa sana na utendaji wao akitumia maneno ya Kiingereza.... “I am very impressed.” Malecela ‘amgonga’ Rostam
  Vyanzo vyetu vya habari vinaeleza kuwa Malecela ambaye wiki kadhaa alikuwa nje ya nchi kwa matibabu, alifanya mashambulizi ya hoja dhidi ya Rostam, akisema si mtu wa kulalamika kufanyiwa siasa chafu ambazo ameziasisi binafsi kiasi hata cha kuathiri raslimali za chama.
  Akitaja mifano ya wazi inayogusa mwenendo wa uchumi wa CCM, Malecela ananukuliwa na vyanzo vyetu vya habari akisema CCM ilikuwa ikimiliki hisa katika kampuni moja kubwa, lakini baadaye katika mazingira yenye mafumbo, mmiliki wa hisa alibadilika, na kwamba hali hiyo ndiyo iliyopata kujitokeza katika baadhi ya vyombo vya habari nchini vilivyopata kuwa katika sehemu ya umiliki wa CCM.
   
 2. W

  We know next JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  CCM, hayo maamuzi yao ndiyo yanayoiyumbisha hata Serikali, nadhani ifike wakati sasa, CCM wakubali yaishe. Suala la kujivua Gamba ni shughuri nzito. Ikiwa kama itafuatwa kwa maana yake halisi, sidhani kama CCM itakuwa salama.
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Aug 4, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wakati mwingine ni bora sana JK akae kimya kuliko kusema lolote..
  Yeye ndio alisema Chama kinajivua magamba leo tena anamwambia Mzee Msekwa kwamba watuhumiwa waliomba muda watafakari!... yaani chama kinajivua magamba kutokana na jinsi magamba wenyewe watakavyo fikiria..Halafu tena anaisifia sekretariet kwa maamuzi yake ni maamuzi yapi hayo ikiwa sekretariet inataka wajiuzulu haraka kisha yeye anasema magamba wapewe muda zaidi kutokana na makubaliano na Msekwa!..
  I mean huu uswahili wa kuzunguka zunguka watu utakwisha lini na lini maanake simwelewi kabisa au - Ndivyo Tulivyo?
   
 4. B

  Biscuit Member

  #4
  Aug 4, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  enajua magamba mengine ni magumu ,yaani ni lazima utumie maji ya moto ndipo gamba liondoke na ikishidikana chuna kabisa ,sasa tatizo ccm nyezo za kukoka moto ajili ya kuchemcha maji hawana na hata kunyoa visu vimebaki butu so hadi mdudu awfie
  biscuit
   
 5. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,092
  Likes Received: 504
  Trophy Points: 280
  JK anahangaika sana namna gani amwokoe comrade wake aghalabu wa zamani but it is so difficult.Poor JK!
   
 6. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,092
  Likes Received: 504
  Trophy Points: 280
  Kwa trend hii sitashangaa iwapo JK atapigana kufa na kupona kumsaidia EL kugombea uraisi kupitia CCM come 2015,na kwa jinsi nilivyomsoma JK ni mgumu sana kukata tamaa kwa lile alokusudia kulifanya,it may take ages but lifanyike so lets wait and see...
   
 7. z

  zamlock JF-Expert Member

  #7
  Aug 4, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  ah ah ah ah ccm wanalo
   
 8. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  JK ni kana kwamba ana mambo anataka kuyafanya ila anaogopa macho ya watu!
  Baba ndo wakati wa kufanya maamuzi magumu huu sasa
   
 9. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2011
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Hili gazeti lina play na hii saga kinafiki sana, ni gazeti lenye agenda isioeleweka ktk siasa za nchi, binafsi naliona ni mmoja wa lobbying group kwa watawala in the name of media, maoni yangu binafsi naliona raia mwema kama political group, undercover leading machine ambayo kwayo agenda si nchi na maendeleo ya kweli bali watu na visasi zaidi hali hii inanipa shida sana kuuona uzalendo wa kweli ndani ya raia mwema, napenda this day trends na mwanahalisi hakuna biasness
   
 10. z

  zamlock JF-Expert Member

  #10
  Aug 4, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  ah ah ah ah ccm wanalo
   
 11. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #11
  Aug 4, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  <br />
  <br />

  Watu wanadhani urais ni kuruka na jet na ku-cruise na BMW.
   
 12. Edmond

  Edmond JF-Expert Member

  #12
  Aug 4, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ngoya tusubiri epsode inayofuata
   
 13. Edmond

  Edmond JF-Expert Member

  #13
  Aug 4, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ngoja tusubiri epsode inayofuata
   
 14. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #14
  Aug 4, 2011
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  sisiem ya akina gen. shimbo!....

  sisiem yenye viongozi wanaotumia zao korofi
   
 15. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #15
  Aug 4, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nini maana ya statement ya Macela kuwa ccm ilikuwa na hisa kwenye company kubwa ila Rostam akaziiba na kubadilisha jina. Au ndo hisa za Voda ni za magamba wamedhurumiwa? Hata huwa siamimi kama RA hisa zoe zile ni za kwakwe.
   
 16. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #16
  Aug 4, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  ccm yetu tunaitakaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 17. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #17
  Aug 5, 2011
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  FDR umesema kweli kabisa. Nimelifuatilia hili gazeti kwa muda sasa, kwa kweli nimeliona ni kama la watu wenye visasi. Kwa kweli lisipojiangalia litapoteza kabisa wasomaji. Naomba akina Ulimwengu na political group lake waache agenda waliyoifanya wakiwa kwenye gazeti la Rai ya kutupandikizia Kikwete kuwa atakuwa kiongozi bora. Waombe msamaha kwa hilo badala ya kuendeleza personal vendetta.
   
 18. H

  HADJ DROGBA Member

  #18
  Aug 5, 2011
  Joined: Dec 16, 2009
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acheni ubw..ge nyinyi hili ni gazeti la ukweli,mkilisema hivi hili gazeti vipi mwanahalisi la sasa?hebu fuatilieni mwanahalisi na raia mwema kuhusu walivyo cover kile kikao cha uvccm then muone nani anayumbisha watu na nani mkweli,maudhui ya kile kikao au mkutano ilikua kuunga ama kupinga hatua iliyochuliwa na kamati kuu pamoja na nec ya ccm kuamua chama cha mapinduzi kijivue gamba,kilichotokea kwenye ule mkutano ni uvccm kuunga mkono kujivua gamba,lakini kubenea alivyocover ile story ya ule mkutano wala hiyo ajenda mama hakuizungumzia badala yake kakimbilia kuwanukuu Msomali Bashe,Mmasai nani sijui yule mwenyekiti wa uvccm arusha..na wengine wa kundi la mtaka urais kwa nguvu..lakini soma raia mwema uone walivyoandika na kuelezea kwa ufasaha nini kilichojiri huko,nani alisema nini kutoka kila upande na mwisho maamuzi ya kikao yalikua yepi.....rais mwema bado wanafanya kazi nzuri,mwanahalisi ndio wanayumba,anae nuna anune anae cheka acheke huo ndio ukweli
   
Loading...