Kizimbani pale pamejengwa kwa ajili ya watu wala siyo nyani.

Na kila mtu ni mteja wa hapo katika muda tofauti wala hutakiwi kumcheka mtu ambaye yupo kwenye hilo eneo.
Hii busara inapatikana kwa watu wachache saana
Hongera saana
 
Gazeti lisiloaminika!! Wanataka alimradi kumpanikisha bashit. Wamshtaki kwa kuchafua majina ya watu kuhusu madawa alipe mabilioni afilisikie mbali
Laana ya Gwajima hiyo!!!! yule jamaa alimsema Bashite ata shuka vuuuu!!! ''si mtaona!!!'' daaa!! imekuwa kweli! hivi kile kimdomo cha gwajima inawezekana kikawa na mungu wa kweli!!! gwajima muondolee mwenio hiyo mzigo wa laana!
 
Kizimbani pale pamejengwa kwa ajili ya watu wala siyo nyani.

Na kila mtu ni mteja wa hapo katika muda tofauti wala hutakiwi kumcheka mtu ambaye yupo kwenye hilo eneo.
mpaka na wamiliki vizimba wa leo!! siku ya siku ni wateja pale eee !!loool!!
 
Unapigiwa saluti na bado umepanda juu ya ngazi.
FB_IMG_1637083272929.jpg
 
Bashite acha uzuzu kimbilia Rwanda kwa Kagame huyo no mjomba wako hawezi kukutupa..ni kaka ya mwendazake.
ou paup...
Hawa jamaa wanataka kukupa miaka si chini ya 7 hadi 15 ukizubaa..una tuhuma nyingi sana...kalagabaho.
 
Kama ambavyo kichwa cha habari kinaeleza, ni mwendo wa kutafuta haki zilizocheleweshwa kwa muda mrefu. Sasa Bwanamdogo kumfuata jamaa yake Sabaya.

View attachment 2010908
====

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote kujibu tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka.

Taarifa hiyo imeandikwa kwenye gazeti la Raia Mwema toleo la leo (Novemba 15,2021), ambapo inaelezwa kwamba, maombi ya kumfungulia kesi Paul Makonda, yamepelekwa na Mwanasheria wa kujitegemea ambaye jina lake halijawekwa wazi.

Raia Mwema limeeleza kwamba katika Mwanasheria huyo ameomba kibali cha Mahakama kumshitaki Makonda kutokana na makosa anayodaiwa kuyatenda wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kinyume cha Sheria namba 96.

Mwanasheria huyo ameomba Makonda afikishwe kortini pia kujibu tuhuma za kuingilia maudhui ya matangazo ya kituo cha televisheni cha Clouds, alipoenda katika ofisi zao, usiku wa Machi 17,2017.

Paul Makonda alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam tangu mwaka 2016 alipoteuliwa na aliyekuwa Rais wakati huo, Hayati Dkt John Pombe Magufuli. Mwaka 2020 Paul Makonda aliondolewa katika nafasi hiyo ikiwa ni baada ya kutangaza nia ya kugombea Ubunge katika jimbo la Kigamboni.

Iwapo Paul Makonda atafikishwa Mahakamani, atakuwa kiongozi wa pili kukabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka katika kipindi cha hivi karibuni, kwani aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya alishafikishwa Mahakamani kwa makosa hayo na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.
Du yame kuwa hayo
 
Ni uzushi tu. Makonda kijana mwanamapinduzi wa chama cha mapinduzi ana adui wengi waovu. Uongozi wake kuwabaini wauza madawa ya kulevya na kusababisha wengi kutupwa lupango au kuishiwa mtaji wao wa kuharibu vijana katika jamii umewaacha na hasira na kisasi.

Jamii haitegemei ccm hii inayodai bado ni chama cha mapinduzi itawaacha vijana wake kama Makonda kunyanyaswa na wauza madawa ya kulevya na maajenti wao. Vinginevyo umma watatia sahihi kukiondoa ccm kama cha cha mapinduzi.
Mlikuwa mnasema hivyo kwa sabaya, sasa hivi yupo nyuma ya nondo na amebakiza miaka 29 na miezi 10
 
Back
Top Bottom