Hii ni strategy ya ccm kuwaondoa watanzania kwenye mijadala ya msingi ya katiba mpya, ukosefu wa umeme kwa zaidi ya miezi miwili, na hali ya kukosekana maji katika jiji la Dar es Salaam.

Watanzania akili zao ni fupi sana
We ni mkenya?
 
Kama ambavyo kichwa cha habari kinaeleza, ni mwendo wa kutafuta haki zilizocheleweshwa kwa muda mrefu. Sasa Bwanamdogo kumfuata jamaa yake Sabaya.

View attachment 2010908
====

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote kujibu tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka.

Taarifa hiyo imeandikwa kwenye gazeti la Raia Mwema toleo la leo (Novemba 15,2021), ambapo inaelezwa kwamba, maombi ya kumfungulia kesi Paul Makonda, yamepelekwa na Mwanasheria wa kujitegemea ambaye jina lake halijawekwa wazi.

Raia Mwema limeeleza kwamba katika Mwanasheria huyo ameomba kibali cha Mahakama kumshitaki Makonda kutokana na makosa anayodaiwa kuyatenda wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kinyume cha Sheria namba 96.

Mwanasheria huyo ameomba Makonda afikishwe kortini pia kujibu tuhuma za kuingilia maudhui ya matangazo ya kituo cha televisheni cha Clouds, alipoenda katika ofisi zao, usiku wa Machi 17,2017.

Paul Makonda alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam tangu mwaka 2016 alipoteuliwa na aliyekuwa Rais wakati huo, Hayati Dkt John Pombe Magufuli. Mwaka 2020 Paul Makonda aliondolewa katika nafasi hiyo ikiwa ni baada ya kutangaza nia ya kugombea Ubunge katika jimbo la Kigamboni.

Iwapo Paul Makonda atafikishwa Mahakamani, atakuwa kiongozi wa pili kukabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka katika kipindi cha hivi karibuni, kwani aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya alishafikishwa Mahakamani kwa makosa hayo na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.
Muda haujafika tu.
 
Kosa linaloitwa matumizi mabaya ya madaraka ni gumu kulitolea ushahidi mbele mahakama ya haki bila kuonyesha kuwa alitumia madaraka hayo kujinufaisha yeye binafsi na familia yake.

Akitumia madaraka hayo kukutisha linaweza liswe kosa la jinai bila viongezi vingine.
ongeeni tu M A T A G A ... hakuna mkate mgumu mbele ya chai
sabaya anakula miaka 30 shimoni huyu nae BASHITE atakula mvua ya kutosha haswaaa
 
ongeeni tu M A T A G A ... hakuna mkate mgumu mbele ya chai
sabaya anakula miaka 30 shimoni huyu nae BASHITE atakula mvua ya kutosha haswaaa
Na "Gaidi" naye siku akipigwa mvua 30 msianze ngonjera za eti mahakama haina uhuru...
 
Porojo tu hizi

Huyo ni Kipenzi cha mama hicho
JamiiForums464585178_480x578.jpg
Mahakama_Kuu_Kanda_ya_Dar_es_Salaam_imeruhusu_kufunguliwa_kwa_kesi_ya_jinai_dhidi_ya_aliyekuwa...jpg
 
Back
Top Bottom